Muko na Allah, Enyi Watu wa Al-Ghouta

Taafifa kwa Vyombo vya Habari
(Imestafsiriwa)

Zaidi ya mashambulizi ya angani 2000 yalifanywa na jeshi la anga la Urusi (mashambulizi 1150) na jeshi la anga la Syria (mashambulizi 900) na kuangamiza watu na ardhi; yaliangamiza mahospitali, masoko ya mboga na viwanda vya kuoka mikate, yakiuwa mashahidi 900 na kujeruhi raia 2000 wasiokuwa na silaha. Ulimwengu mzima umenyamazia kimya uchinjaji huu wa jambazi wa Damascus na Moscow, katika ukatili wao wa kuendelea kuwamaliza watu watu wa Ghouta, mashujaa waliokataa kumsujudia Firauni, au Nero wa karne hii, Bashar. Lakini Bashar si chochote isipokuwa ni kikaragosi aliyeyapa majeshi ya anga ya Urusi “uhalali” katika uvamizi wao, unaomulika chuki nzito ya Putin kwa Uislamu na Waislamu.

Kimya cha nchi za Kimagharibi, zinazoitwa “jamii ya kimataifa”, kinadhihirisha kushiriki kwao katika ukatili huu muovu. Nchi hizi tayari zilikwisha nyanyua mwito wa, “Katu Haitokei Tena” kuzuia kutokea upya kwa yale yanayoitwa mauaji ya halaiki (ya Ujerumani kwa Mayahudi). Huku mwito huu ukikosa kutabikishwa eneo la Srebrenica-Bosnia mnamo 1995, wakati ambapo majeshi ya kuhifadhi amani ya UM yalipo wasalimisha Waislamu kwa magengi ya wahalifu na kuwapa ruhusa ya kutekeleza mauaji ya halaiki dhidi ya Waislamu 11,000; wala haukutekelezwa nchini Rwanda mnamo 1994 wala nchini Afrika ya Kati mnamo 2016. Wala Myanmar mnamo 2017.

Ndio maana si ajabu kwa Kanali John Thomas wa afisi ya kushughulikia mambo ya umma katika taasisi kuu ya utoaji amri za kijeshi ya Amerika kuliambia gazeti la Daily Beast: “Hizo si kadhia zetu”, “Taasisi kuu ya utoaji amri za kijeshi ya Amerika (CENTCOM) haihusiki na chochote nchini Syria isipokuwa tu kulishinda kundi la wanamgambo la ISIS na baadhi ya mamlaka ya kukabiliana na ugaidi”,

Kumzuia gaidi mkubwa kabisa, Bashar Al-Assad, kibaraka mtiifu kwa Amerika, si sehemu ya mipango ya kijeshi ya Amerika nchini Syria. UM chini ya katibu mkuu katika masuala ya kisiasa Jeffrey Feltman,kwa kuendeleza mchezo wa jambazi huyu, alikiambia kikao cha Baraza la Usalama la UM mnamo 28/2/2018, juu ya hali ya kibinadamu nchini Syria, kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea “kulingania haki na uwajibikaji kwa nguvu”, “wale wanaohusika na msururu wa ugaidi unao athiri maisha ya kila siku nchini Syria… watahisabiwa”,

Ruhusa hii inafafanua taarifa ya Lavrov: “Kuna makundi eneo la Mashariki mwa Ghouta pamoja na Idlib, ambayo yanawasilishwa kama makundi poa na washirika na wafadhili wa Kimagharibi, likiwemo kundi la Ahrar Al-sham na Jaish Al-Islam, yanayo shirikiana na vuguvugu la Ahrar Al-Sham”, akiongeza kuwa serikali ya Syria na Moscow zitaendelea kuyalenga. Ndio. Lavrov analituhumu vuguvugu la Ahrar Al-Sham, linalopigana vita vikali dhidi ya Hay’at Tahrir Al-Sham mjini Idlib kwamba linashirikiana na kundi hili lilobandikwa jina la kuwa kundi la “kigaidi”, ili kuhalalisha kampeni yao ya maangamivu kwa msingi wa sera ya uchomaji ardhi eneo la Ghouta.

Hiyo ndio sababu Urusi wala Umoja wa Mataifa hazikukubali ofa za kundi la Jaish Al-Islam na Failaq Ar-Rahman; kuondoa chembechembe za Hay’at Tahrir Al-Sham kutoka Ghouta. Kuziondoa chembechembe hizi kutaharibu kisingizio cha kupigana na magaidi. Na kuzibakisha ndani kutahalalisha ulipuaji mabomu kwa watoto na wanawake na kulipua mahospitali, masoko ya mboga, viwanda vya kuoka mikate, maduka ya madawa na magari ya dharura ya wagonjwa. Yote haya yako mbele ya macho na masikio ya “jamii ya kimataifa” ambayo inanyanyua bendera ya hadhara na haki za kibinadamu!

Na pia yako mbele ya macho na masikio ya watawala wa Waislamu walioshughulishwa na kuhudumia maslahi ya mabwana zao, wakoloni wa Kimagharibi. Na yako mbele ya macho na masikio ya viongozi wa majeshi katika biladi za Waislamu. Majeshi haya, yanayo nyonya maelfu ya mabilioni ya mali ya Waislamu, ikiwa hawata tekeleza majukumu yao ya kuwalinda Waislamu na kuhifadhi heshima na damu zao, ni lipi lengo la kuwepo kwao?

Mtume (saw) alisema: «مَا مِنْ امْرِئٍ يَخْذُلُ امْرَأً مُسْلِمًا فِي مَوْضِعٍ تُنْتَهَكُ فِيهِ حُرْمَتُهُ وَيُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ إِلَّا خَذَلَهُ اللَّهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ فِيهِ نُصْرَتَهُ وَمَا مِنْ امْرِئٍ يَنْصُرُ مُسْلِمًا فِي مَوْضِعٍ يُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ وَيُنْتَهَكُ فِيهِ مِنْ حُرْمَتِهِ إِلَّا نَصَرَهُ اللَّهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ نُصْرَتَهُ» “Hakuna mtu yeyote atakaye muacha mkono Muislamu yeyote katika hali ambayo utukufu wake unaangamizwa na heshima yake kudunishwa ndani yake, isipokuwa Allah naye atamuacha mkono katika hali ambayo inahitajia nusra ya Allah ndani yake, na hakuna mtu yeyote atakaye mnusuru Muislamu yeyote katika hali ambayo utukufu wake unaangamizwa na heshima yake kudunishwa ndani yake, isipokuwa Allah naye atamnusuru katika hali ambayo inahitajia nusra ya Allah”.   

Ewe Allah sisi ni wanyonge, tupe ushindi.

Dkt. Osman Bakhach
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

H.  21 Jumada II 1439 Na: 1439 AH / 014
M.  Ijumaa, 09 Machi 2018