Sera ya Afya Isiojali Afya

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari

Wizara ya Afya imefichua kuwa shilingi bilioni 20 zimepotea kupitia mpango wa Hazina ya Kitaifa ya Bima ya Afya (NHIF) kupitia madai yaliyotengenezwa na upasuaji ghushi, ikiwa ni miongoni mwa visa vyengine vya kilaghai vinafanywa na vituo vya afya. Waziri wa Afya Wafula Nakhumicha, alifichua kashfa hiyo iliyoathiri vituo vya afya, akisema kuwa kati ya hospitali 67 zilizokaguliwa nchini, 27 zimesimamishwa kazi kutokana na hasara ya sh.171 milioni kupitia mpango wa NHIF.

Tungependa kutaja yafuatayo:

Ni dhuluma kubwa kwa maofisaa wa serikali waliopewa dhamana ya kuwakilisha maslahi ya umma, badala ya kufanya kazi ya kuboresha hali ya maisha ya mwananchi wa kawaida wanashindana katika ubadhirifu wa rasilimali za umma.

Kama ilivyo sekta yoyote ya umma katika tawala zote za kibepari,sekta ya afya haisimamiwi ipasavyo kutosha, kwani nia pekee ya ufanisi na utendaji mzuri ni faida. Kwa kuzingatia hili, kimsingi suala la afya halipewi kipaumbele katika uongozi wowote wa kirasilimali. Kwa hivyo, sio lengo la serikali za kibepari kujali raia wakawaida bali hutunza zaidi tabaka maalumu la watu wenye ushawishi mkubwa wa kisiasa na mabwenyenye. Fauka ya haya, sera ya bima ya afya yenyewe ni dhihirisho wazi la Serikali kukwepa jukumu lake la kushughulikia masuala ya umma ikiwa ni pamoja na afya. Bali chini ya sera hii mbovu, mwananchi wa kawaida analazimika kulipia huduma za afya kabla ya kuugua.

Kwa kuwa Kenya inafuata itikadi fisidifu ya Kibepari ambayo imejawa na hamu kubwa ya kujilimbikizia mali kwa njia zote basi “vita dhidi ya ufisadi” kamwe havitoshinda. Mfumo huu umejikita kwenye uchu wa upapiaji wa mali na hauna hata chembe ya uchamungu, hufanya tamaa ya kiulimwengu kuwa kigezo pekee cha maisha ambacho bila shaka ndio hupelekea watu  hasa maofisaa wa serikali kuwa na ari ya kujilimbikizia mali kwa njia za kifisadi.

Uislamu umeiweka sekta ya matibabu kama moja ya mahitaji ya kimsingi kwa umma inayohitaji uangalizi mkubwa. Uislamu hauzingatii  huduma za afya au huduma yoyote ile ya umma kama fadhila ya serikali kwa raia wake, bali umefanya afya kipaumbele ambapo serikali hupaswa kuwajibika kupeana huduma hiyo  kwa raia wake wote.

Ama kuhusu ufisadi unaofanywa na maafisa wa serikali, jambo hili linaweza tu kushughulikiwa ipasavyo kupitia Dola ya Khilafah ambapo kiongozi  wa dola (Khalifah) anatekeleza sheria za Mwenyezi Mungu. Sheria zinazoamua jinsi Serikali inavyokusanya na kutumia rasilimali zake. Aidha, Uislamu umeamuru kwamba mali ya afisa wa serikali inapaswa kubainishwa kabla na baada ya kushika wadhifa huo na baada ya kuiacha.Ongezeko lolote lisilo la kawaida la mali ya kiongozi au afisa yeyote wa serikali huchukuliwa na kuingizwa kwenye hazina ya serikali. (Baitul Mal). Tunasema ni Khilafah) tu juu ya njia ya Utume ndio itamaliza tishio la ufisadi nchini Kenya na ulimwengu kwa ujumla.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi Kwa Vyombo Vya Habari  Hizb ut Tahrir Kenya