Hali Tete ya DRC Congo ni kutokamana na Ukoloni mambo leo

Habari na Maoni

Habari:

Raisi wa DRC Congo Felix Tshisekedi ameshinda tena uchaguzi wa nchi hiyo kwa zaidi ya asilimia 70 ya kura, tume ya uchaguzi ya nchi hiyo ilisema Jumapili tarehe 31 Disemba, huku wagombea wa upinzani na wafuasi wao wakihoji uhalali wa matokeo hayo. Matokeo ya awali ya uchaguzi wa Desemba 20 yalitangazwa katika mji mkuu, Kinshasa, huku kukiwa na matakwa ya upinzani na baadhi ya mashirika ya kiraia kutaka kura zirudiwe upya kutokana na matatizo makubwa ya vifaa (Lojistiki) ambayo walisema yalitatiza   mchakato wa upigaji kura.

Maoni:

Taifa la DRC Congo lina historia ya chaguzi tete ambazo wakati mwengine hugubikwa na vurugu, na kuna imani ndogo miongoni mwa Wakongo wengi katika taasisi za nchi hiyo. Kabla ya matokeo hayo kutangazwa, wagombea wa upinzani akiwamo Moise Katumbi walikataa matokeo hayo na kuwataka wananchi kujipanga upya kwa uchaguzi mwengine. Kwa mujibu wa sheria za Uchaguzi nchini Congo wagombea wanaopinga matokeo wana siku mbili za kuwasilisha madai yao huku  mahakama ya kikatiba nayo ina wiki moja kufikia uamuzi. Matokeo ya mwisho yanatarajiwa Januari 10, na rais ameratibiwa kuapishwa mwishoni mwa mwezi huu.

Licha  ya utajiri wa rasilimali, taifa la Congo ni maskini na limekosa utulivu wa muda mrefu, Limekua likikabiliwa na matatizo mengi makubwa tangu “uhuru” wake kutoka Ubelgiji mwaka 1960. Kuanzia kwa rushwa iliyosheheni hadi utovu wa  usalama, mfumuko wa bei na umaskini yote  yamekua matatizo  ya mara kwa mara. Hata hivyo, nchi hii ina utajiri mkubwa wa maliasili. Ni mzalishaji anayeongoza duniani wa cobalt na mzalishaji wa tatu kwa ukubwa wa shaba – madini yanayotumika katika utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki na magari ya umeme. Nchi hiyo pia ina ardhi ilio na utajiri kwa kilimo na imejaa viumbe hai – Msitu wa Mvua wa Kongo ukiwa wa pili kwa ukubwa duniani

Felix Tchisekedi katu hatoweza kuiokoa Congo kutoka kwa mataifa ya kimagharibi machoyo yenye uchu wa uporaji wa mali. Utawala wake hauna tofauti yoyote kubwa na mtangulizi wake Joseph Kabila katika kuuza utajiri wa nchi kwa mabilionea wakubwa wa kibepari na kuwaacha Wakongo wengi katika lindi la umaskini mkubwa. Utawala wake wa miaka mitano umekumbwa na ufisadi wa hali ya juu, kutoka kwa hongo ndogo ndogo zinazotolewa kila siku kutoka kwa watu wa Congo hadi kashfa kubwa za ubadhirifu unaotikisa kampuni za uchimbaji madini nchini DRC.

 

Hali ya DRC Congo inahusiana sana na ukoloni mamboleo kama mataifa hasa Marekani na Ulaya yakiwa ndio hucheza dori kubwa kimataifa  katika kuchochea migogoro ya nchi hiyo ambayo kimsingi ina utajiri mkubwa wa madini. Marekani imekuwa ikitumia nchi kama Uganda, Burundi na Rwanda kuunga mkono vikosi vya upinzani kuweka Kongo chini ya ushawishi wake. Katika mkutano wa hivi majuzi wiki moja kabla ya uchaguzi, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alimshukuru Tshisekedi na Rais wa Rwanda Paul Kagame kwa uongozi na michango yao katika juhudi hizi. Ulaya (Uingereza, Ubelgiji na Ufaransa) inasukuma nchi kama Kenya, Zimbabwe, Zambia, na Afrika Kusini kudhibiti mipango ya  Amerika.

Wito wa Marekani wa suluhu ya amani kwa mizozo inayohusiana na uchaguzi unaonyesha kwamba anapendelea Tshisekedi kutokana na hofu ya ghasia zinazoungwa mkono na nchi za Ulaya ambazo zimekuwa zikifanya kazi kupitia mawakala wao wa kisiasa kutoka upinzani. Ni muhimu kutaja kwamba Ufaransa na Uingereza zimekuwa zikiwaunga mkono baadhi ya waasi dhidi ya matakwa ya Marekani. Kwa hiyo, mapambano ya maslahi ya kiuchumi kati ya mataifa ya kigeni yameifanya Congo kuwa na nchi inayotawaliwa na vita.

Ukombozi wa DRC Congo ni kupitia kukumbatia Itikadi ya Kiislamu itayotekelezwa na serikali ya Khilafah yenye mfumo mbadala wa Ukoloni wa kimagharibi kiini kikuu  cha majanga yote Duniani. Khilafah juu ya utaratibu wa Mtume (saw) itahakikisha ustawi wa kisiasa, kiuchumi na kijamii kutokana na utekelezaji wake wa itikadi ya Kiislamu na hukumu zake. Zaidi ya hayo, itatumia rasilimali zake kikamilifu katika kuondosha uchochole.

Imeandikwa kwa Niaba ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb  ut Tahrir na

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir Kenya.

01/01/2024