Tahnia za Mwanachuoni Mkubwa Ata Bin Khalil Abu Rashtah, Kwa Wanaozuru Kurasa Zake wakati huu adhimu wa Idd ul-Fitr yenye Baraka ya Mwaka wa 1439 H Sawia na Mwaka wa 2018 M

بسم الله الرحمن الرحيم

 (Imetafsiriwa)

Sifa njema zote ni za Allah na rehma na amani zimshukie Mtume wa Allah, na jamaa zake na maswahaba zake na wale wanaomfuata,

Kwa Ummah wa Kiislamu ambao Allah ameukirimu na kuutaja:

كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ﴿

 “Nyinyi ni Ummah bora muliotolewa kwa ajili ya watu. Munaamrishana mema na munakatazana mabaya na munamuamini Allah” [Al-i-Imran: 110]

Kwa wabebaji ulinganizi wema na wenye ikhlasi na wala hatumtakasi yeyote kwa Allah, wanaolingania kwa Allah na kufanya matendo mema:

وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِمَّنْ دَعَا إِلَى اللَّهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِين﴿

“Na ni nani mwenye kauli njema zaidi kuliko yule alinganiaye kwa Allah na kufanya amali njema na akasema, ‘mimi ni miongoni mwa Waislamu’” [Fussilat: 33]

Kwa waheshimiwa wanaozuru mitandao wanaoingia katika kurasa kwa haki na ikhlasi, wakitafuta kheri ndani yazo, Allah awalipeni kheri.

Nawapa tahnia nyote katika sikukuu hii yenye Baraka ya Idd ul-Fitr, na namuomba Allah (swt) azikubali saumu zenu, na awajaaliye miongoni mwa wale watakaookolewa na Moto wa Jahannam katika mwezi huu mtukufu. Pia namuomba Allah (swt) kwamba Idd hii iwe ndio mwanzo wa kheri na Baraka kwa Waislamu, na kwamba katika Idd ijayo tuwe chini ya kivuli cha Khilafah Rashida, bendera ya Raya ya La Ilaha Ila Allah Muhammad Rasool Allah, na jambo hili ni rahisi kwa Allah kulitimiza.  

Mwisho, natuma salamu na dua zangu kwenu nyinyi kupata kheri hii, na Allah azikubali ibada zetu tiifu, na Allah awahifadhi na kuwalinda kutokana na kila uovu.   

فَاللَّهُ خَيْرٌ حَافِظًا وَهُوَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ﴿

“Na Allah ni mbora wa kuhifadhi na Yeye ni Mwingi wa kurehemu.” [Yusuf: 64]

Wassalaam Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakaatuhu

Usiku wa Idd ul-Fitr, 1 Shawwal 1439 H                  Ndugu Yenu,

15/6/2018 M                                                        Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah