Tunawapongeza kwa Munasaba wa Eid ul –Adh-ha

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

Harakati ya Hizb ut-Tahrir Kenya ingependa kutuma salamu za dhati za Id ul-Adha kwa Waislamu humu nchini na wote dunia kwa ujumla. Tunatuma salamu zetu wanaume na wanawake wanaofanyakazi kwa juhudi kubwa katika kusimamisha tena Khilafa ya Pili kwa mfumo wa utume. Kama vilevile tungependa kumtumia salamu zetu Amiri wa Hizb ut-Tahrir Mwanachuoni mkubwa Ataa Bin Khalili Abu al-Rashta kwa munasaba wa kuingiliwa na Idul –Adha.

Idi hii tukufu inakuja huku kiwango cha mfumoko wa bei kimefikia hadi asilimia 7.9 hali iliopelekea bei ya vyakula kupanda maradufu.Kinaya ni kuwa huku raia wakiumizwa na hali hii wanasiasa wa mirengo yote wamejikita katika kuhadaa raia kwenye kampeni za uchaguzi wa Agosti 9 kwamba eti maendeleo ni kutia kura debeni.  Mfumoko ni janga la kutengezwa chini ya mfumo wa Kibepari na utaratibu wake pesa za makaratasi. Kwa kuwa Mfumo wa Kirasilimali na itikadi yake ya Kiilmaania imekataa mfumo utokao kwa Mwenyezi Mungu SWT nao ni Uislamu hivyo  maisha ya wanadamu yapo kwenye dhiki.

Tunaposherehekea Idi hii, twapasa kujikumbusha mtihani mkubwa aliokumbana nao nabii Ibrahim (as) na jinsi alivyokuwa tayari kujitolea. Leo walinganizi wa Khilafah wanapata mateso ya tawala za kidhulma kote duniani. Kwa hakika tupo katika kipindi cha kujitolea  cha kuulingania Uislamu kama mfumo mbadala wa Mfumo uliofeli wa Kirasilimali na hapo ndio suluhisho litapatikana kwa matatizo ya ulimwengu na kuwa na tija kubwa.

Mwisho twamuomba MwenyeziMungu SWT kutakabali  amali zetu njema na atuongoze hadi kufikia Idi nyengine tukiwa ndani ya kivuli cha Khilafah Raashida  kwa mfumo wa Utume itakayo unganisha Waislamu wote duniani chini ya bendera ya Laa ilaha ila llah Muhammad Rasul Allah.

 

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari

Hizb ut-Tahrir Kenya.

in Kenya