Manifesto ya vyama: Hali ni ileile kamwe haitobadilika kwani Uislamu umetupiliwa mbali!

Habari na Maoni

Habari:

Mbio za kumsaka raisi wa serikali ijayo zimeshika kasi ikiwa tayari wagombea wa wadhifa wa urais, walioidhinishwa na tume ya usimamizi wa uchaguzi wakizindua rasmi manifesto zao kwa ajili yakupata kura za uchaguzi wa Mwezi Agosti 09. Raila Odinga anayewania kwa mara ya tano kiti cha urais, alizindua manifesto yake mapema mwa mwezi Juni ambayo kimsingi imejikita mabadiliko ya kiuchumi kwa kupitia uenezwaji wa viwanda. Akiahidi kuwa kila Gatuzi katika magatuzi yote 47 kuweko na kiwanda cha uzalishaji. Mpinzani wake wa karibu naib rais William Ruto ambaye kwake ni mara ya kwanza kugombea urais alizindua manifesto yake mnamo Juni 30. Manifesto yake nayo imejikita kwa misingi mitano ikiwemo: kufufua uchumi wa nchi kupunguza gharama za maisha, kuimarisha hali za vijana. Profesa Wajackoya ameteka masikizi takriban pembe zote za nchi pale ali[otaja kwenye manifesto yake kwamba atahalalisha bangi!

Maoni:

Manifesto za vyama vya kisiasa ni ada ya zamani ambapo huweka mkataba wake na wapiga kura. Kama zilivyokuwa manifesto za vyama vya kisiasa vya miaka ya nyuma, manifesto zilizozinduliwa hazina chochote kipya katika Aidilojia. Wanasiasa wa Kidemokrasia ama vyama wana hulka ya kutoa ahadi zisizo kuwa na sura wazi bali hujaza masuala ambayo serikali zote zilizopita hazikuweza kuzitekeleza. Kwa mfano utawala wa sasa unaondoka wa Jubilee kwenye manifesto yake uliahidi kubuni nafasi za kazi milioni 1.3  kila mwaka kwa vijana wasokuwa na kazi lakini wapi! ilikuwa ni ahadi tupu. Uhalisia wa mambo ni kwamba Kampeni za Demokrasia zinadhaminiwa na mabwenyenye mabepari wanaohonga wapiga kura kama chambo na kuwapata mawakala wa kisiasa ambao wakichaguliwa wafanye kila wawezavyo kulinda maslahi yao.

Kuhusu suala la uhalilishwaji wa bangi, hii inaonesha bayana jinsi itikadi ya Kisecular ilivyozalisha wanasiasa wanaotukuza maovu na fikra za kihuni. Kwa kutenganisha Dini na Maisha, usekula umesheheni wanasiasa wanaopelekwa na matamanio na wala sio sharia za MwenyeziMungu (Swt)

Yoyote atakayeshinda uchaguzi huu kwa hakika hatobadilishi kimsingi hali ngumu anayokabiliana nayo raia wakawaida. Hii ni kwa sababu uongozi katika Demokrasia ni urongo na tamaa tu ya  kukidhi maslahi ya kibinafsi wala sio kujali maslahi ya watu. Serikali itakayoundwa itajifunga na sera unyonyaji za mfumo wa Kikoloni wa kirasilimali. Seuze ya hayo, hizi chaguzi za Kidemokrasia hufichua urongo na utapeli uliojikita kwenye kutoa ahadi tupu na kudai kwamba upigaji kura ndio njiya ya kufikia maendeleo na mabadiliko na mustakabali mwema.

Kwa kuwa manifesto zote hizi zimeweka Uislamu mbali katika ajenda ya mabadiliko, hii ina maanisha kuwa hali itabakii hiyohiyo wala haitobadilika.Uislamu una mengi ya kutekelezwa kikamilifu na una njia halisi ya kufikia mabadiliko ya kikweli ambao dunia nzima lazima  ijukumike kuufanyia kazi.

Imeandikwa Kwa niaba ya Ofisi Kuu ya  Habari ya Hizb ut Tahrir na

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari  Hizb ut-Tahrir Kenya

01/07/2022.