Uchina Imezidisha Kampeni yake ya Kuwatia Korokoroni Wengi na Kuwafunza Ukomunisti Watoto wa Uyghur Waislamu ilhali Dunia Inatizama
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Utafiti mpya uliochapishwa mapema mwezi huu na ambao ulifanywa na BBC, umeripoti kwamba Uchina iko katika, “kampeni kubwa ya kujenga shule za mabweni kwa kasi mno” ili kuwatia kizuizini kwa nguvu watoto wa Uyghur Waislamu kutoka Turkestan Mashariki ambao wako uhamishoni au wanashikiliwa ndani ya ‘kambi za kuwapa elimu upya’ ambamo hivi sasa ndani yake Waislamu milioni 1 wamefungwa. Lengo la wazi ni utaratibu wa kuwatenganisha watoto Waislamu kutoka kwa familia zao na imani zao za Kiislamu. Kwa mujibu wa ripoti kwa kichwa “Kata Mizizi Yao: Ushahidi wa Kampeni ya Uchina ya Kutenganisha Wazazi na Watoto ndani ya Xinjiang”, iliyoandikwa na Adrian Zenz, mtafiti wa suala la Uchina kuwatia Waislamu wengi korokoroni ndani ya Turkestan Mashariki, utawala wa Uchina umekuwa ukiboresha uwezo wake wa kuwadhibiti na kuwapa mafunzo mapya idadi kubwa ya watoto wa Uyghur kwa kutumia thaqafa yake ya kikomunisti na kwa wakati huo huo imekuwa ikijenga kambi za kuwafungia watu wazima. Ripoti ya Zenz ambayo msingi wake ni nakala rasmi zinazoelezea “kampeni isiyokuwa ya kawaida ya upanuzi wa shule” ndani ya Turkestan Mashariki, ambayo inajumuisha upanuzi wa shule za mabweni, ujenzi wa mabweni mapya na kuzidi kwa idadi kwa kiwango kikubwa mno. Ripoti inasema kwamba ndani ya mwaka 1 pekee, 2017 jumla ya idadi ya watoto waliosajiliwa katika chekechea ndani ya Turkestan Mashariki imezidi kwa zaidi ya nusu milioni huku watoto wa Uyghur na Waislamu wakiwa ni idadi ya zaidi ya asilimia 90 ya walioongezeka. Fauka ya hayo, usajili wa Uyghur katika chekechea imekuwa kwa asilimia 148 ndani ya maeneo ya Uyghur kati ya 2015-18 ikipita usajili wa kawaida wa kitaifa mara 18 huku mtoto mchanga aliyeko korokoroni akiwa na miezi 15 pekee. Zaidi ya hayo, kusini mwa ‘Xinjiang’ pekee mamlaka zimetumiwa dolari bilioni 1.2 kwa kujenga na kuboresha chekechea ambazo zinajumisha ongezeko la idadi kubwa ya nafasi za mabweni. Zenz anasema, “Shule za mabweni zinatoa mazingira mazuri ya kuwamakinisha ujenzi wa kithaqafa kwa jamii ndogo…lengo la muda mrefu ndani ya Xinjiang ni kupelekea kwa maafa ya kithaqafa, yaliyochorwa ili kubadilisha kabisa na kuziweka sambamba nyoyo na akili za kizazi kijacho na mfumo wa Chama cha Kikomunisti.”
Kwa kisingizio cha uongo cha kuzuia ‘misimamo mikali’ na ‘ugaidi’ ambacho serikali ya Uchina imeelezea kuwa ni kujihusisha na vitendo msingi vya Kiislamu kama swala, kusoma Qur’an, kufuga ndevu na kuvaa mavazi ya Kiislamu. Utawala huu wa kidhalimu unazidisha vita vyake vya kimsalaba ili kuweza kukuza kizazi kipya cha Uyghur na Waislamu ambao wako mbali na Dini yao ya Kiislamu, na kuufuta Uislamu kutoka Turkestan Mashariki ‘shule za jela’ ziko kwa lengo sawa na kambi za jela za watu wazima: kuwapa elimu mpya watoto Waislamu kwa kutumia thaqafa ya kikomunisti na kuondosha athari zote za imani ya Kiislamu, kiasi kwamba wawe ni vikaragosi watiifu kwa Chama cha Kikomunisti, watawaliwa wanyenyekevu kwa dola na maadui wa familia zao Waislamu, jamii ya Uyghur na imani ya Kiislamu. Licha ya ‘maafa ya kithaqafa,’ hakuna anayetarajia dola yoyote ndani ya urasilimali uliotawala dunia kuchukua msimamo dhidi ya Uchina ili kuwalinda Uyghur Waislamu, kwa kuwa maslahi yao ya kiuchumi yana uzito zaidi kuliko kusitisha machungu na ukandamizaji wa wanadamu. Tawala oga za Waislamu nazo pia zimeendelea kujiweka karibu na dola hii dhalimu dhidi ya Waislamu, pasina aibu ikijitia hamnazo kuhusiana na kuwatesa Uyghur Waislamu kwa sababu ya kutaka kupata maslahi yao ya kifedha. Vyombo vya habari vya Uchina vimeripoti kwamba wakati wa ziara ya Beijing ya hivi majuzi ya Rais wa Uturuki Erdogan, alipaza sauti na kuiunga mkono Uchina kwa eti vitendo vyake ‘dhidi ya misimamo mikali’ na kupendekeza kwamba nchi hizo mbili zichukuwe hatua za kupigia debe oparesheni za ushirikiano za kupambana na ugaidi napia kusema kuwa, “Ni kweli kwamba watu wa Uchina katika eneo la Xinjiang wanaishi kwa furaha kutokana na maendeleo na ufanisi wa Uchina.” Hii ni licha ya kwamba kuna namba kubwa ya Uyghur walioko uhamishoni ndani ya Uturuki yenyewe, ambao wamekimbia mateso kutoka kwa dola ya Uchina, wengi ambao wamepoteza watoto kwa ‘shule za jela!’ Ukombozi wa Uyghur Waislamu kutoka katika makucha ya ukandamizaji wa utawala wa Uchina utafaulu kwa kusimama kwa dola ya Khilafah kwa njia ya Utume, kwa kuwa hii ni dola ambayo haipigi hesabu za kiuchumi katika vitendo vyake bali ni kutegemea Maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt) pekee. Hii inajumuisha kutekeleza Maagizo Yake (swt) ya kuwalinda Waislamu pasina na kujali gharama ya kifedha. Ni dola ambayo inawakilisha na kulinda kiukweli maslahi ya Uislamu na Waislamu sio kupiga domo tu katika kusitisha dhulma! Mtume (saw) alisema,
«إِنَّمَا الإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Kiongozi ni ngao, nyuma yake mnapigana na kujilinda”
Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
13 Dhu al-Qi’dah 1440 Na: 1440 H / 036
Jumanne, 16 Julai 2019