Taarifa kwa Vyombo vya Habari
(Imetafsiriwa)
“Katika taarifa moja iliyo tolewa mnamo 31/7/2019, Muungano wa Kamati za Wafanyikazi wa Wanawake wa Palestina, mrengo wa wanawake wa Chama cha Kidemokrasia cha Ukombozi wa Palestina, ulipinga msimamo wa Hizb ut Tahrir juu ya mwelekeo wa serikali ya Palestina wa kutabanni sheria inayo ongeza umri wa ndoa wa wanawake wa Palestina hadi miaka 18. Taarifa hiyo iliichukulia rai ya chama hiki kuwa inavuka mipaka ya kanuni za kiakili na mantiki, zinazo kadiria umri wa halali wa kupiga kura na kupata leseni ya kuendesha gari na uwezo wa kufanya maamuzi uwe ni miaka 18, na kupuuzilia mbali madhara ya kisaikolojia, kiafya na kijamii ya ndoa ya mapema chini ya umri wa miaka 18, ambao ni umri wa utotoni, kama unavyo tambuliwa kimataifa kwa wanawake pamoja na wanaume.”
Kwa kutoa maoni juu ya taarifa hiyo, sisi katika Kitengo cha Wanawake cha Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir tunasema yafuatayo:
1- Wale wanaotafuta na kupigia debe umri wa ndoa kuwa miaka kumi na nane, wanaupima umri wa ukomavu na kubaleghe kwa kipimo cha Kimagharibi, ambao ni umri wa miaka kumi na nane, hivyo basi ni kwa nini umri ambao mwanamume au mwanamke anachukuliwa kuwa mtu mzima au mtoto unapimwa kwa mujibu wa nidhamu ya Kimagharibi? Na ni kwa nini uamuzi huu unakadiriwa kuwa sahihi?! Je, taswira ya mtoto kwa Magharibi ni sawa na ya Waislamu? Katika nidhamu ya Kimagharibi na fasihi inayo tokamana nayo, umri wa kubaleghe au “utu uzima” kama wanavyo uita ni miaka kumi na nane, na chini ya umri huo anakadiriwa kuwa mtoto. Lakini, katika Uislamu, umri wa kukalifishwa kwa wanaume unazingatiwa kwa kubaleghe na wanawake kwa kuvunja ungo. Mtu mzima aliye komaa mwenye akili timamu na anaye hesabiwa anakalifishwa na hukmu za kisheria na ni lazima ajifunge kwazo kwa sababu ya matokeo ya thawabu au adhabu. Ukomavu dalili zake zinahusiana na akili au mwili, na kuna wale waliozidi umri wa miaka kumi na nane lakini hawaja komaa, hivyo basi Uislamu hauku ufanya ukomavu kuwa sharti la uhalali wa mkataba wa ndoa.
2- Wanaopigia debe kuwekwa umri wa ndoa kuwa miaka 18 wanazungumzia kuhusu athari za kisaikolojia na kiafya za ndoa ya mapema kwa kusema kuwa viwango vya vifo na madhara ya uzazi kwa mke mchanga vinatokana na ndoa ya mapema. Lakini, hawataji kuwa takwimu hizi hazijadili kuhusu huduma mbaya za afya katika maeneo yale ambayo ndoa za mapema zimeshamiri. Bali, wananasibisha baadhi ya magonjwa ya kiakili na ndoa hizo, huku wakikosa kutaja kuwa hali za kimaisha zilizo lazimishwa na urasilimali, na kulazimishwa kwa utepetevu wa usimamizi kutoka kwa serikali, ndio sababu kuu ya ugumu wa maisha na ukosefu wa uwezo wa kumudu mahitaji ya kimaisha ya makaazi, mavazi na masrufu. Hapa tunawauliza wao kuhusu mahusiano haramu yaliyo enea Magharibi baina ya wale wanaoitwa kuwa watoto, na uzazi haramu wa wasichana wa kati ya umri wa miaka 12 na 18, kina mama wasio na waume katika umri huu!! Je, tabia hii ya kihuria inakubalika na haisababishi madhara ya kimwili na ya kisaikolojia kwao, na haikiuki haki zao kama watoto, bali ndoa ya Kiislamu, inayo hifadhi haki na hadhi, ndio ukiukaji wa haki hizo na ndio sababu ya madhara ya kiafya ya kiakili na kimwili kwao?! Ni uamuzi mbaya ulioje wenu huu.
3- Wale wanaotaka kuweka umri wa ndoa chini ya pazia la uhuru na haki za wanawake wanafuata ‘Sunnah’ ya nchi za Kimagharibi na taasisi zao zinazo lenga kupigia debe ukombozi wa wanawake wa Kiislamu kutokana na maadili yao ambapo wanaitusi hadhi iliyo hifadhiwa na Uislamu, chini ya kisingizio cha ukombozi wa haki za wanawake. Pia unashajiisha mahusiano kadha wa kadha chini ya kisingizio cha uhuru na kuondoa usimamizi kutoka kwa walii wa wanawake, na kuwapa wanawake uhuru wa kuchagua watakalo. Ulinganizi wa stara na ulinzi kwa wanawake haumo ndani ya kamusi za watetezi wa haki za wanawake, wanao shambulia mahusiano kupitia ndoa katika sheria ya Kiislamu, huku wakisalia kimya na hata kushajiisha mahusiano haramu chini ya kisingizio cha uhuru wa wanawake. Hawapingi mahusiano ya kijinsia baina ya “watoto”, huku wakiikadiria ndoa ya mapema kuwa kosa na kuituhumu kwa ujinga!
4- Uislamu unashajiisha ndoa, na haukuifafanulia au kuilazimishia umri fulani. Mwenyezi Mungu (swt) asema katika Kitabu Chake Kitukufu,
[وَأَنْكِحُوا الْأَيَامَى مِنْكُمْ وَالصَّالِحِينَ مِنْ عِبَادِكُمْ]
“Na waozeni wajane miongoni mwenu na wema katika watumwa wenu.” [An-Nur: 32].
Uislamu unalenga katika ndoa kuleta utulivu na huruma na kuifanya ndani yake kuwa stara ya macho na tupu na kulinda mujtama na mtu binafsi. Vipi basi fahamu hii itadhaniwa kuwa “mila na turathi zilizopitwa na wakati”?
Inajulikana kuwa Uislamu umefanya utoaji ombi na kukubali kuwa nguzo ya mkataba wa ndoa, hivyo hairuhusiwi kumlazimisha mwanandoa yeyote mtarajiwa kabla au baada ya umri wa miaka 18 kuoa au kuolewa, na Uislamu haukuwanyima wanawake haki zao za kufanya kazi au elimu kabla ya ndoa na baada ya ndoa.
Kwa kutamatisha, tunayageukia makundi ya utetezi wa wanawake, na kusema: Umetosha uangamizaji wa vizazi, akhlaqi na maadili! Tunayauliza ni kwa nini yanapaza juu sauti zao dhidi ya Uislamu na hukmu zake kwa kudai kuwajali wanawake na haki zao, huku hatuyasikii yakiwatetea wanawake wanao nyanyaswa ulimwenguni, wanao uwawa, kuteswa na kukamatwa na heshima yao kukiukwa?! Kwa nini yanajifanya – kwa kujua na kutoa jua – kuwa ni ala mikononi mwa serikali za kihalifu katika biladi za Waislamu, nchi wafadhili na taasisi zao katika vita juu ya Uislamu na Waislamu?! Tunawaambia watie akili na kujiepusha kutokana na haya.
Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
4 Dhu al-Hijjah 1440 Na: 1440 `H / 038
Jumatatu, 05 Agosti 2019