Uzinduzi rasmi wa kampeni ya Kiuchumi ya Hizb ut-Tahrir /Kenya chini ya kauli mbiu: Msoto wa Kiuchumi : Uislamu ndio Jibu.

Harakati ya Hizb ut-Tahrir Kenya imezindua rasmi kampeni ya kiuchumi itakayodumu kwa mwezi mmoja. Kampeni hii itaanza tarehe mosi ya mwezi mtukufu wa DhulHijja 1442 Hijria sawasawa na  tarehe 11 Julai 2021) na kutamatika  Agosti 11.

Kampeni hii inalenga kuangazia uhalisia wa mfumo wa Kiuchumi wa Kibebari na jinsi ulivyosababishia umma majanga ya kiuchumi. Aidha, inalenga kuweka wazi uhalisia wa mfumo wa Kiuchumi wa Kiislamu na athari yake katika kipindi cha karne 13 pindi Uislamu ulipokuwa na utawala wake wa Khilafah pia na vipi pindi itakaposimama hivi karibuni  kwa Idhini ya MwenyeziMungu SWT itaweza kutatua matatizo ya kiuchumi na mengineyo.

Kwenye kampeni hii, Hizb ut-Tahrir /Kenya itaandaa msururu wa amali ikiwemo mihadhara mbalimbali katika maeneo mbalimbali, mzungumzo ya mitaani, semina na wasomi na mufakirina miongoni mwa amali nyengine.

Mwisho, tunatoa mwito kwa jamii kwa jumla na hasa umma wa Kiislamu kushiriki nasi katika kampeni hii tukufu ambayo ndani yake hatutarajii lolote ila malipo kwa MwenyeziMungu SWT.Twamuomba MwenyeziMungu (Swt) afanikishe kampeni hii na ifanye kuwa ni yenye kuleta kheri kwa Umma wote wa Kiislamu.

Fuatilia Kampeni hii kwa Hashtag:

#Msoto wa Kiuchumi _Uislamu ndio Jibu

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir in Kenya