Ni Serikali ya Uturuki ndiyo Inayoandaa Msingi wa Mashambulizi ya Kiubaguzi wa Rangi dhidi ya Wanawake na Watoto
Taarifa Kwa Vyombo vya Habari
Jioni ya 5 Oktoba 2019 mwanamume anayeitwa Nadir Kızılbulut alimpiga kinyama mtoto wa miaka 5 Msyria kwa msukumo wa kiubaguzi wa rangi. Pia aliwashambulia mama wa mtoto huyo na dadake wa miaka 15 kimwili na maneno na kumpiga baba yao usoni na kushambulia nyumba yao na kuvunja madirisha. Filamu ya video ya shambulizi hilo ilisambaa katika twitter kwa mwito #Mersin ambayo ilikuwa kileleni kwa masaa. Haikubakia tu tabia ya mtu huyo na ubaguzi wake wa rangi uliopelekea shambulizi hilo bali pia vitendo vya polisi na wasimamizi wa sheria. Mshambuliaji huo wa kiubaguzi wa rangi hakushikwa baada ya malalamishi ya familia hiyo lakini ni baada ya kelele katika mitandao ya kijamii, ilhali baba alitiwa korokoroni. Licha ya kuwepo video ya mashamulizi, mchakato wa kufurushwa ulianzishwa dhidi ya familia ya Wasyria wakiwa na uraia wa Jordan.
Kuna ongezeko kubwa la idadi na mashambulizi ya ubaguzi wa rangi ndani ya Uturuki. Ni siku mbili tu zilizopita, mtoto wa miaka 9 Msyria akittwa Wail Al-Suud, alijinyonga katika mlango wa makaburi katika wilaya ya Kocaeli ndani ya Uturuki kutokana na kutoweza kuvumilia maonevu ya ubaguzi wa rangi aliyoyapata kutoka kwa mwalimu wake na wanafunzi wenzake. Hivi majuzi watu wa Adana walichochewa dhidi ya wakimbizi Wasyria ambao walilaumiwa kwa uhangaisho wa kijinsia uliofanywa na mwanamume wa asili ya Uturuki. Napia ni miezi kadhaa tangu kwa kikundi cha ubaguzi wa rangi ambacho kilimtukana kijana wa miaka 12 Msyria kwa kumshutumu kuwa alimdhulumu binti mdogo. Kufuatia kutukanwa huko, wabaguzi wa rangi wakafurika katika barabara za Instanbul na kuleta vurugu na kuwashambulia Wasyria na wageni wengine. Kando na hayo, neno ‘vurugu’ linaonekana kupindwa kwa kuwa hakuna kattu wale wanaopinga vurugu dhidi ya watoto na wanawake na kulingania haki za watoto na uhuru wa wanawake hawakutamka hata neno wakati wa mashamulizi hayo ya vurugu. Hakuna hata maoni kutoka kwa masekula, wahuria, walinganizi wa ukombozi wa wanawake, wanademokrasia, mashirika na taasisi wala Waziri wa Familia au waziri au makamu wake yeyote wa AKP ambao walitoa ahadi ya mpango mpya wa haki za binadamu.
Wanawake na watoto hawa wasiokuwa na hatia walichagua Uturuki kuwa ndio kimbilio salama walipokuwa wanakimbia vita vya kinyama wakiamini kwamba udugu wa Kiislamu una nguvu zaidi kuliko fungamano la damu. Walitafuta ulinzi kutoka kwa ndugu zao na sio wenzao wa rangi pasina kujua kuwa watawala wa Uturuki wameufunga Uislamu wao tu katika hotuba katika ibada za Ijumaa na Eid, na vitambaa vya kichwani na kubadilisha sehemu ya udugu wa Kiislamu na kuweka utaifa na uzalendo uliochorwa na Sykes-Picot. Ilhali Waislamu wanakwenda mbio kufikia cheo cha kuwa Ansar, sio tu upinzani wa Kemal ambao umetenganisha misingi ya Kiislamu na kuandaa misingi ya kurudisha na kueneza uovu na ufisadi wa ubaguzi wa rangi wa Jahiliyyah bali ni wanasiasa wa sasa wanaotawala wa serikali ya AKP ambao walipiga marufuku mabango ya lugha ya Kiarabu na kuahidi kufurusha wakimbizi 50,000 Wasyria ikiwa ni nyongeza katika maelfu ambao tayari ishawafurusha kiuhalifu na kulifanya suala la ukimbizi kuwa ni sawa na tatizo la ugaidi na madawa ya kulevya kwa kwa sentensi moja.
Enyi Watawala wa Uturuki! Hususan rais, mawaziri na manaibu wa AKP! Siasa hizi za kisekula, kitaifa na zisizokuwa za Kiislamu ambazo mumezibeba, munazilingania na kuzitekeleza kwa mapenzi, sio tu zinawaweka mbali nyinyi wenyewe na Uislamu na udugu wa Kiislamu bali pia wale wanaofuata njia yenu. Na inachochea na kusambaza kwa wale walioingia sumu ya ubaguzi wa rangi na kuwa kama mambwa mwitu dhidi ya watoto na wanawake wasioweza kujilinda. Ukandamizaji na unyama wowote ambao unatokana na nidhamu hii ya kitaifa ya kikafiri na ubaguzi wake wa rangi pia mnao mgao katika hesabu zenu Siku ya Kiyama. Bado hamutambui hilo?
Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw) alisema: «ليس منا من دعا إلى عصبية وليس منا من قاتل على عصبية وليس منا من مات على عصبية» “Sio katika sisi anayelingania ukabila. […]” [Abu Davud, Ibn Majah] Na yeye (saw) pia akasema: «وَمَنْ دَعَا إِلَى ضَلاَلَةٍ كَانَ عَلَيْهِ مِنَ الإِثْمِ مِثْلُ آثَامِ مَنْ يَتَّبِعُهُ لاَ يَنْقُصُ ذَلِكَ مِنْ آثَامِهِمْ شَيْئًا» “[…] “Na yeyote anayelingania katika upotofu, basi atapata madhambi sawa na madhambi ya wale wanaomfuata, pasina na kupunguziwa chochcote kutoka katika madhambi yao.” [Muslim, Abu Dawud, Tirmidhi, Ibn Majah]
Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
H. 12 Safar 1441 | Na: 1441 H / 004 |
M. Ijumaa, 11 Oktoba 2019 |