بسم الله الرحمن الرحيم
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir:
Vyombo vya usalama nchini Uzbekistan vimewakamata tena wanachama 23 wa Hizb ut Tahrir na kuendelea na taratibu za kesi zao Mei 9 mwaka huu kwa mashtaka yale yale waliyoshtakiwa wakati wa enzi ya dhalimu aliyefariki Karimov, ambayo kwayo walitumia karibu miaka 20 jela na mateso tangu 1999 – 2000 M. Licha ya madai yote yaliyotolewa na Mirziyev miaka iliyopita, ambapo alidai kuwa anapinga mateso na unyanyasaji dhidi ya wafungwa, na kwamba yuko kwenye njia ya kuunganisha uhuru wa fikra na itikadi na kupambana na ukamataji kiholela, tabia ya hivi karibuni ya serikali ya Uzbekistan chini ya uongozi wake inaonyesha kwamba inafuata nyayo za Karimov aliyekufa katika kuwa na uadui na Uislamu na wale wote wanaoulingania, na kuwatesa mashababu wa Hizb ut Tahrir kwa kutumia mbinu za kidhalimu na za kikatili ambazo mtangulizi wake wa uhalifu Karimov ilizitumika hapo awali.
Mashababu walikamatwa kiholela na kwa njia za kinyama na za kikatili kwa haki zao na kuwalazimisha kuungama tuhuma walizobambikiziwa, ambapo waliwaweka mifuko kwenye vichwa vyao na kuweka shinikizo kali juu yao, na walilazimishwa kutia saini maungamo hayo yaliyotayarishwa mapema chini ya tishio la kuletwa mke wa mmoja wao afisini na kumbaka. Na tishio jengine lilikuwa kumleta mtoto wa shababu mwengine anayesoma nje ya nchi, hadi Uzbekistan kupitia ubalozi, na kumleta mtoto wa shababu mwengine katika Afisi ya Mambo ya Ndani ili kumlazimisha kusaini hati ya kukiri, na kumtesa shababu mwengine kwa shoti ya umeme. Pia mashababu wapya 16 walikamatwa katika majimbo ya Tashkent, Andijan, Hawqan, Karshi na Samarkand, na kufikishwa Tashkent na kuchunguzwa, kwa tuhuma zinazohusiana na kufanya vurugu na ugaidi!
Tuhuma za ugaidi na kutekeleza unyanyasaji dhidi ya mashahabu wa Hizb ut Tahrir ni wazi kuwa ni uzushi na uongo. Hizb ut Tahrir na mashababu wake hawafanyi fujo wala ugaidi, na wala hizb haijawahi kufanya hivyo tangu kuasisiwa kwake mwaka 1953 M. Haifanyi hivi sio kwa sababu ya kuogopa kwake tawala hizi au kujaribu kuridhiana na tawala dhalimu, bali kwa sababu inamwabudu Mwenyezi Mungu kwa njia yake ili kuregesha maisha kamili ya Kiislamu, ambayo ni njia ya kifikra na kisiasa ambayo iliifuatwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Kwa hiyo, tawala zote za ukandamizaji na za kipolisi katika nchi za Kiislamu na hata katika nchi za Magharibi hazikuweza kuthibitisha shtaka la ugaidi au vurugu dhidi ya Hizb ut Tahrir na mashababu wake, licha ya majaribio yao ya mara kwa mara. Lakini ni chuki inayofurika kutoka katika nyoyo za watawala wahalifu, ambayo inawasukuma kudanganya macho na masikio yao kutokana na kutaka kulipiza kisasi dhidi wabebaji wa mradi unaokuja wa Kiislamu, mradi wa Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Watawala wa Waislamu, chini ya uongozi wa mabwana zao, viongozi wa uhalifu na ukoloni nchini Marekani, Uingereza, Urusi, Ufaransa na Ujerumani, wanaupiga vita mradi wa Uislamu na kuzikanyaga sheria na kanuni zao wanazozipigia debe na kuzinadi kwa ulimwengu (uhuru, demokrasia, haki za binadamu) linapokuja suala la ubebaji dawah miongoni mwa mashababu wa Hizb ut Tahrir.
Kuregea kwa Mirziyev katika mkabala wa ukandamizaji, ukamataji, na utesaji katika nyayo za Karimov aliyekufa kunaonyesha kwamba jambo hilo ni utekelezaji wa matamanio na sera za viongozi wa kikoloni nchini Urusi na Marekani, na kwamba watawala wetu, kama kawaida yao, hawamiliki maamuzi yao na si chochote ila wafuasi wa vibaraka wa ukoloni.
Sisi katika Hizb ut Tahrir tunauonya utawala wa Mirziyev dhidi ya kuregea kwenye sera ya ukandamizaji na ukatili ambayo utawala wa Karimov uliitumia dhidi ya Uislamu na wabebaji dawah yake. Hii ndiyo njia ya wahalifu na haitawanufaisha, bali itazidisha hasira za Umma juu yake na kujaalia kuangamia kwake, Umma wa Kiislamu sasa unatazamia siku hiyo utakapokombolewa kutokana na ukoloni na kuregea katika sheria ya Mola wake Mlezi, kama katiba, sheria na maisha, na Umma leo uko karibu zaidi kuliko wakati mwingine wowote kufikia lengo na matumaini yake. Hivyo basi, Mirziyev lazima awaachilie huru mashababu wetu mara moja na bila kuchelewa, aache kuwatesa wale wanaobeba ujumbe na kuwa na uadui kwa mradi wa Uislamu, na ajifunze kutoka kwa wale waliokuja kabla yake, hakika mwisho mwema ni kwa wachaMungu hata kama mila yote ya ukafiri itakusanyika pamoja, na Mwenyezi Mungu atainusuru dini yake, hata kama ni baada ya muda kidogo, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema
﴿كَتَبَ اللهُ لَأَغْلِبَنَّ أَنَا وَرُسُلِي إِنَّ اللهَ قَوِيٌّ عَزِيزٌ﴾
“Mwenyezi Mungu ameandika: Hapana shaka Mimi na Mtume wangu tutashinda. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kushinda.” [Mujadala: 21]
Ijumaa, 29 Dhu al-Hijjah 1445 H sawia na 5 Julai 2024 M
Kufuatilia Kampeni kwa Lugha Nyenginezo
Taarifa kwa vyombo vya habari Iliyotolewa na
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
“Utawala wa Mirziyoyev nchini Uzbekistan Unafuata Nyayo za Karimov Aliyekufa, katika Kuwatesa Mashababu wa Hizb ut Tahrir na Kukabiliana na Uislamu”
Ijumaa, 29 Dhu al-Hijjah 1445 H sawia na 5 Julai 2024 M
Ili Kusoma Bonyeza Hapa
#ЎЗБЕКИСТОНДАН_ФАРЁД
#PleaFromUzbekistan
صرخة_من_أوزبيكستان#