Njia ya Mtume (saw) Kuleta Mageuzi

بسم الله الرحمن الرحيم

Halaqa ya 8: Maudhi na Adhabu kwa Mtume (saw) na Wabebaji Da’wah

Katika Halaqa hii tutazungumzia mbinu ya nne ambayo waliitumia Muqureshi dhidi ya Da’wah ya Mtume (saw) nayo ni maudhi na adhabu kwa Mtume (saw) na kwa wabebaji Da’wah.

Alivumilia Mtume (saw) shida zote na maudhi akiwa anawalingania waja kwa Allah. Maudhi yakazidi kwa Mtume (saw) na adhabu kwa wanaomuamini, na dori hii ikachukua mda mrefu. Mivutano ya kifikra na mapambano ya kisiasa yakaachukua muda mrefu takriban miaka kumi, Waislamu walipitia sampuli za adhabu.

Asema Allah (swt):

كَمَا أَخْرَجَكَ رَبُّكَ مِنْ بَيْتِكَ بِالْحَقِّ وَإِنَّ فَرِيقًا مِنَ الْمُؤْمِنِينَ لَكَارِهُونَ

Kama Mola wako Mlezi alivyo kutoa nyumbani kwako kwa haki, na hakika kundi moja la Waumini linachukia.

[Al-Anfaal 8:5]

Mtume (saw) alipata maudhi makali tofauti tofauti, ili awache Da’wah, makafiri na mushrikina walipanga njama ya kumuua Mtume (saw). Wakajaribu kumuua mara kadhaa, lakini Mtume (saw) aliendelea na subra na huku akitarajia kwa Allah. Haikudhoofika azma yake wala imani yake kwa Allah haikulainika kwa matatizo yaliyomkuba katika Da’wah, bali alibakia thabit katika mfumo, anawalingania waja kwa Allah kwa azma na thabati, ili apata Radhi za Allah, na ili awe mfano mwema na kiigizo chema kwa Maswahaba, na kwa watakaokuja baada yake mpaka kitakaposimama kiyama.

Amepokea Bukhari kutoka kwa Urwah Radhi za Allah ziwafikie asema: “Nilimuuliza Ibnul ‘Aas Radhi za Allah zimfikie, nikasema: Nipe khabari jambo gani zito ambalo mushrikina walimfanyia Mtume?” Akasema: “Alipokuwa Mtume (saw) anaswali katika chumba cha Kaabah Uqbah Ibnul Muit akamwendea Mtume (saw) akaweka nguo yake katika shingo ya Mtume (saw) akamnyonga kwa nguvu, Abubakar (ra) akaja akamshika mabega yake na kumsukuma kutoka kwa Mtume (saw).”

Akasema Allah (swt):

وَقَالَ رَجُلٌ مُؤْمِنٌ مِنْ آلِ فِرْعَوْنَ يَكْتُمُ إِيمَانَهُ أَتَقْتُلُونَ رَجُلًا أَنْ يَقُولَ رَبِّيَ اللَّهُ وَقَدْ جَاءَكُمْ بِالْبَيِّنَاتِ مِنْ رَبِّكُمْ ۖ وَإِنْ يَكُ كَاذِبًا فَعَلَيْهِ كَذِبُهُ ۖ وَإِنْ يَكُ صَادِقًا يُصِبْكُمْ بَعْضُ الَّذِي يَعِدُكُمْ ۖ إِنَّ اللَّهَ لَا يَهْدِي مَنْ هُوَ مُسْرِفٌ كَذَّابٌ

Na akasema mtu mmoja Muumini, aliyekuwa mmoja katika watu wa Firauni aliye ficha Imani yake: Je, Munamuuwa mtu kwa sababu anasema Mola wangu Mlezi ni Mwenyezi Mungu? Na hali naye amekujieni na hoja zilizo wazi? Na akiwa yeye ni mwongo basi uwongo wake ni juu yake mwenyewe, na akiwa mkweli yatakufikieni baadhi ya hayo anayo kuahidini. Hakika Mwenyezi Mungu hamwongoi apindukiaye mipaka, mwongo mkubwa.

[Ghafir: 28]

Huu ni mfano mmoja tu wa Mtume (saw) kupata shida na maudhi kwa ajili ya daa’wah, na kuna mifano mingi inayotajwa na vitabu vya Seera haitoshi kuelezea kwa ufafanuzi hapa. Licha ya hayo, tutaitaja baadhi yake kwa ufupi sana:

Alipokufa Abu Twalib, jitu jinga moja katika wajinga wa Kikureyshi alimtupia Mtume (saw) mchanga. Mtume (saw) akarudi nyumbani, binti yake mmoja akaja na kumfuta uso wake huku akilia. Rasul (saw) akaketi na kusema: “Ee mwanangu! Usilie, Naapa kwa Allah, Allah atamkinga babako)…!”

Utbah Ibnu Muit alitupa juu ya kichwa cha Mtume (saw) na katika mabega yake uchafu wa ngamia akiwa Mtume (saw) amesujudu.

Abu Jahli alimkuta Mtume (saw) katika Swafaa akamuudhi mpaka Ami yake Mtume Hamzah akakasirika, akaenda msikitini akamkuta Abu Jahli akiwa katika kikao cha Maqureyshi, hakumuongelesha bali alimsimamia kichwani na kumpiga kwa uta mpaka akapasuka, wakasimama wanaume katika Maqureysh wanamzuia Hamzah: Akasema hamzah: “Dini yangu ni Dini ya Muhammad. Nashuhudia kuwa yeye ni Mtume wa Allah…!” Akasilimu papo hapo.

Mtume (saw) alipokuwa anaondoka kwa kabila la Thaqif baada ya kukosasa Nusra, watu wataifa hilo walikaa katika njia safu mbili, alipopita wakawa wanampiga mawe kila anaponyanyua mguu wake mpaka wakamtoa damu. Akapita na ilhali damu inachuruzika…!

Makafirii wa Kikureshi hawakukoma kwa mateso waliomfanyia kabla ya kusimamisha serikali, bali yalifuatia hata baada ya kusimamisha dola, siku ya vita vya Uhud waliyavunja meno yake ya mbele ya Mtume (saw) na kichwa chake kupasuliwa, akasema naye anafuta damu katika uso wake mtukufu: “Vipi watafaulu watu walioupaka damu uso wa mtume wao?!!” Akateremsha Allah (swt):

لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ فَإِنَّهُمْ ظَالِمُونَ

Wewe huna lako jambo katika haya – ama atawahurumia au atawaadhibu kwani wao ni madhalimu

[Aal-Imran:128]

Itaendelea katika UQAB Toleo 13…In Shaa Allah.