Njia ya Mtume (saw) Kuleta Mageuzi

سم الله الرحمن الرحيم

Halqa 14: Kutafuta Nusra Kutoka Kwa Watu Wenye Nguvu Na Mamlaka

Katika Halaqa hii tutaangalia kutafuta nusra kutoka kwa watu wenye nguvu na mamlaka.

Kianzio cha Kuchukua Uongozi

Hakika utafutaji wa Nusra ni katika sehemu muhimu, na ni katika matendo ya hatari ambayo yanabebwa na da’wah; na wanakuwa na majukumu makubwa wale waliosimama na hili jambo, kwa vile wanavyojitolea kwa kiasi kikubwa. Kukubali kwao kuwa watu wa nusra, wameuza roho zao kwa ajili ya Allah, na wakabeba roho zao katika vitengele vyao ili waende Jannah/peponi…! Na hakika kutafuta Nusra ni amri kutoka kwa Allah (swt), nayo ni Taklif kutoka kwake Subhaanahu, inatakiwa iwe na usiri wa hali ya juu, haifai mtu yeyote ajue isipokuwa viongozi pekee.

Na inatakiwa kufanywa kwa njia ya ukamilifu, na ifahamike kuwa hii ni sehemu muhimu ambayo haiwezi kutenganishwa na twariqa ya kubeba da’wah. Haijuzu kwetu kujisahaulisha ama kuiruka ama kushika njia nyengine, na hii yafanana na amali yoyote katika amali za faradhi alizofaradhisha Allah Azza wa Jalla. Kwa hiyo kutafuta Nusra katika da’wah ni mfano wa kusujudu katika swala, sawa kwa sawa, zote zinatimiza faradhi.

Kwa hiyo Rasul (saw) alikuwa na pupa ya hali ya juu katika kutafuta Nusra, akawa Rehma na Amani zimwendee anakwenda peke yake, ama na mmoja wa maswahaba zake akitafuta Nusra kutoka kwa makabila ili wamkubali/wamwamini na wamnusuru kwa waliomfanyia uadui katika jamaa zake na wamzuie na maudhi. Na alikuwa haendi na mtu ila aliyemuamini na anayeficha siri katika maswahaba wake radhi za allah ziwaendee.

Maqureysh wakazidisha maudhi kwa Mtume (saw) na kwa maswahaba zake mpaka wakadhikika, na hakukubakia matarajio ya kunusuriwa na makabila baada ya kukataliwa na Thaqif kutoka Twaif kwa majibu mabaya. Na baada ya kukataliwa na Bani Kinda, na Bani Kalbi, na Bani amir bin Swa’swa’, na Banu Hanifah, Mtume (saw) alipojitambulisha kwao katika msimu wa Hijja, na hakukubakia tamaa kuwa kuna atakayeongoka katika Maqureysh na kuingia katika Uislamu! Na walipoona Muhammad ametengwa, wakazidi kumpa nyongo, Rasul (saw) akaona ukavu wa watu wa Makkah na kuwa mgumu mujtama’h wa Makkah mbele ya da’wah.

Na masiku yakasonga, na Mtume (saw) anazidi kutengwa, na Maqureysh wanazidi chuki dhidi yake, na watu wanazidi kumpa nyongo…! Mtume (saw) pamoja na hayo yote aliendelea kuwa na thiqa juu ya Nusra ya Allah, yeye pamoja na maswahaba zake, Na kuwa Allah atainyanyua dini yake juu ya dini zote, na sisi tuna kiigizo chema katika misimamo mitatu kutoka kwa Mtume (saw) wakati akijitambulisha kwa makabila akitafuta Nusra tutaitaja katika halaqa hii ila twataraji kuelezea kwa ufafanuzi katika halaqat zijazo. In Shaa Allah:

Kwanza: Wakati anajitambulisha (saw) kwa Bani Shiban bin Tha’alaba.

Pili: Wakati anajitambulisha (saw) kwa Thaqif.

Tatu:  Wakati anajitambulisha (saw) kwa Bani Amir bin Swa’swa’

 

Itaendelea katika UQAB Toleo 19…In Shaa Allah.