Njia ya Mtume (saw) Kuleta Mageuzi

بسم الله الرحمن الرحيم

Halaqa 15: Kujitambulisha Mtume (saw) kwa Banu Shaiban

Katika Halaqa hii tutaangalia ujitambulisha Mtume (saw) kwa Banu Shaiban.

Hakika kujitambulisha Mtume (saw) kwa makabila ili wamnusuru na wamhami ili aweze kufikisha risala/ujumbe wa mola wake, ni amri kutoka kwa Mola wake, na ni sehemu muhimu ambayo haiwezi kutenganishwa na twariqa/njia ya kisheria ya kusimamisha Dola ya Kiislamu.

Na hiyo si rai ya Mtume (saw) bali ni amri ya Mwenyezi Mungu (swt) iliyopangiliwa na sheria na kuja kupitia Wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt). Kwa hiyo ni hukmu ya kisheria na inapasa kujilazimisha nayo kama alivyojilazimisha kwayo Mtume (saw).

Ametoa Abu Naim kutoka kwa ibn Abbas (ra) kutoka kwa Ali ibn Abi Twalib (ra) asema: Allah alipomuamrisha Mtume wake (saw) ajitambulishe kwa makabila ya Waarabu, alitoka nami na Abubakar (ra) mpaka tukafika Mina, tukafika katika kikao cha Waarabu akatangulia Abubakar akasalimia, na alikuwa Abubakar kila mara anatangulia, alikuwa ni mtu mwenye nasaba akasema: Nyinyi ni kaumu gani? Wakasema: sisi ni wa Rabi’ah, akasema: Nyinyi ni Rabi’ah gani? Akaelezea Hadith kwa urefu na katika hiyo Hadith akasema: Kisha nikafika katika mkao wenye utulivu, akatangulia Abubakar akasalimia, asema Ali: Na alikuwa akitangulia kila mara, akawaambia Abubakar: Nyinyi ni kaumu gani? Wakasema: Sisi ni Banu Shaiban bin Tha’labah, akamgeukia Mtume (saw) akasema: Bi abiy anta wa ummiy (kiapo) Hamna watu katika kaumu hii wenye izza zaidi ya hawa…!

Na katika kaumu kulikuwa na Hanii bin Qusayyi, na Muthanna bin Haritha, na Mafruq bin Amr, na Nuuman bin Sharik, akataja Hadith kwa urefu wake mpaka akasema: akasema Rasul (saw) : “Nawalingania kwa shahada ya kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah peke yake hana mshirika, na hakika Muhammad ni Mjumbe wa Allah, Na mnipe makaazi na mninusuru na kunihifadhi mpaka niweze kutekeleza aliyoniamrisha Allah (swt).” Hakika Maqureysh walikataa amri ya Allah, na wakamkadhibisha Mtume wake, wakajitosheleza na batiIi kuliko haki, na Allah ndiye aliyetoshelezeka zaidi na Mwenye sifa. Wakasema: “Sisi tuko katika mkataba tuliofunga na Kisra, ya kwamba tusizungumze na mgeni wala kumkaribisha mgeni, na huenda jambo hili likawa ni katika mambo yanayowaudhi wafalme…! Ukitaka tukunusuru upande wa Waarbu tutalifanya hilo.”

Akasema Rasulullah (saw): “Hamkujibu vibaya mlipoweza kusema ukweli…! Wallahi hakuna anayeweza kusimamisha Dini ya Allah ila aliyezunguka pande zote”

Haijuzu kuusoma Mustaqbali (mambo yatakavyokuwa mbeleni) kwa kupitia waqia (uhalisia) wanaoishi nao wabebaji Da’wah. Kisha akasema Rasul (saw) kuwaambia Bani Shaiban: “Je, mwaonaje hamtokaa ila muda mchache Allah atawatunuku miji yao na mali yao, na kuwachukua mabinti zao, je mtamsabihi Allah na kumtakasa?!”

Nu’man bin Sharik akamwambia Mtume: Hakika hilo ni lako wewe ewe ndugu wa kiquraysh…!”

Kisha Mtume (saw) akasoma:

وَدَاعِياً إِلىَ اللهِ بِإِذْنِهِ وَسِرَاجاً مُّنِيْراً

“Na mwitaji kumwendea Mwenyezi Mungu kwa idhini yake, na taa yenye kutoa nuru.”

[Al-Ahzaab: 46].

Kisha akasimama Rasul (saw) akiwa amemshika mkono Abubakar (ra)…!

Katika Hadithi hii tukufu anatufundisha Mtume (saw) na anawafundisha wabebaji Da’wah darasa lilio na umuhimu mkubwa, nayo ni kuwa haifai kusoma mustaqbali kupitia waqia (uhalisia) wanaoishi nao wabebaji da’wah. Kwani nguvu za batili kiasi chochote zitakavyokuwa kubwa haziwezi kuwarudisha nyuma na ufanyaji kazi ya kuing’oa kutoka mizizi yake na kuiondosha kabisa…! Na nguvu za batili kiasi zitakavyokuwa kubwa mwisho wake ni kupenduka…! Na haikuwa kwa wabebaji ulinganizi ila wazidi thiqa kwa Nusra ya Allah, Na wasubiri mpaka itakapofika ahadi ya Allah…!

Itaendelea katika UQAB Toleo 19…In Shaa Allah.