Afisi Kuu ya Habari: Angazo Maalum “Naveed Butt… Je, Haijatosha Miaka Kumi ya Utekaji Nyara?!”

بسم الله الرحمن الرحيم

 

Mnamo tarehe 11 Mei 2021 M, utaanza mwaka wa kumi tangu Naveed Butt, msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Pakistan, alipotekwa nyara mnamo 11 Mei 2012 M na kufungwa katika seli za vyombo vya siri vya ukandamizaji. Mpaka sasa serikali hii ingali inaendelea kumnyima Naveed Butt mawasiliano ya aina yoyote na familia yake. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

 ﴿مُحَمَّدٌ رَسُولُ اللَّهِ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ

Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao.” [Fathi: 29] Je! Hali ya watawala hao ambao ni vibaraka wa Amerika ikoje? Wao ni wapole kwa maadui makafiri na hubadilishana nao hisia za upendo, huruma na upole, huku wanaamiliana na Waislamu kwa mkono wa chuma, mpaka wanatumia lugha ya moto na mabomu pamoja nao. Hii ni licha ya maneno yake (swt) katika Hadith Al-Qudsi ambayo ameizungumza Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

 «إِنَّ اللَّهَ قَالَ: مَنْ عَادَى لِي وَلِياً فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالْحَرْبِ»

“Anaye fanya uadui na kipenzi changu (walii) basi nimekwisha tangaza vita na yeye,” Imepokewa na Al-Bukhari. Naveed Butt, mwenye umri wa miaka hamsini na mbili, baba wa watoto wanne, ni mtoto wa Umma wa Kiislamu, na anasifiwa, kwani ni mwanasiasa wa kimfumo na miongoni mwa wenye uwezo kudura ya kutimiza jukumu la kutawala katika nafasi yoyote, baada ya kurudi kwa Khilafah kwa njia ya Utume, na yeye anatoka katika familia mashuhuri ya Kashmir anayeishi jijini Islamabad. Alikubaliwa katika Chuo Kikuu mashuhuri cha Uhandisi na Teknolojia (UET) jijini Lahore. Kwa ubora wake, alipelekwa Chuo Kikuu cha Illinois nchini Amerika, ambapo alimaliza kuhitimu kwake. Alifanya kazi katika sekta ya kibinafsi nchini Amerika, kabla ya kuamua kurudi Pakistan kuwa sehemu ya mapambano ya kiulimwengu ya kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume katika nchi za Kiislamu, akiacha nyuma maisha ya kifahari kukabiliana na ghadhabu za madhalimu. Ameendelea bila kuchoka kufichua khiyana ya watawala wanaofanya kazi dhidi ya Uislamu na Waislamu na kufichua ubaraka wao kwa Amerika, kwa kuandika mamia ya taarifa za vyombo vya habari, kuandika safu kadhaa za magazeti, akihutubia mikutano kadhaa ya waandishi wa habari, akizungumza kwenye semina na makongamano, na kufanya mahojiano na maelfu ya watu wenye ushawishi wakati wa mapambano yake. Amesafiri kote nchini Pakistan ili kueneza ufahamu kati ya watu juu ya wajibu wa kusimamisha Khilafah na kufafanua vyombo vyake, na wakati wa mapambano yake ya kisiasa na mvutano wa kifikra, alikamatwa mara kwa mara na kufungwa na alikuwa maarufu katika kupambana kwake na ujasiri wake. Ni wazi kwamba licha ya ukandamizaji mkali wa serikali ya Pakistan, Hizb ut Tahrir haijaachana na mapambano yake na hajapunguza kasi. Badala yake, ushawishi wa Hizb ut Tahrir kwa ujumla umeongezeka baina ya Waislamu na haswa katika jeshi. Kwa hivyo, Waislamu wanaovumilia shida katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw), wana ikhlasi na wanastahili uongozi. Na katika mwezi huu uliobarikiwa wa Ramadhan, tunamwomba Mwenyezi Mungu (swt), kwamba kama vile Nabii Yusuf (as), alivyo achiliwa kutoka gerezani kwake, kwamba Naveed Butt pia atoke kwenye korokoro za watawala wa kiimla, na amkirimu kwa kuhukumu kwa yale yote yaliyoteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt), na wakati huo

﴿وَسَيَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَيَّ مُنْقَلَبٍ يَنْقَلِبُونَ﴾.

“Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka.” [Ash-Shu’ara: 227]

Ijumaa, 18 Ramadhan Al-Mubarak 1442 H sawia na 30 Aprili 2021 M

– Ili Kufuatilia Angazo Hili kwa Lugha Nyenginezo –

Ar

En

Tr

Ur

Gr

Kalima ya Video ya Mhandisi Salah Eddine Adada (Abu Muhammad)

Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Kuhusu Kuendelea Kutekwa Nyara kwa Ndugu Naveed Butt Mwenyezi Mungu Amfariji Shida Yake

00:00
01:46

Kalima ya Video ya Dkt Nazreen Nawaz

Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Kuhusu Kuendelea Kutekwa Nyara kwa Ndugu Naveed Butt Mwenyezi Mungu Amfariji Shida Yake

(Hivi Punde InshaAllah)

– Alama Ishara ya Angazo –

#FreeNaveedButt Face Insta Twitter

Tufani ya Twitter

Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt) tutaandaa Tufani ya Twitter kwa kutumia alama ishara

#FreeNaveedButt

Mnamo Siku ya Jumamosi 8 Mei 2021 M

Saa 8pm kwa saa za mji wa Madina Al-Munawwara / 10pm kwa saa za Pakistan.

Tunawaomba Waislamu wote wenye Ikhlasi kupaaza sauti zao kwa ajili ya kuachiliwa huru ndugu yetu Naveed Butt Mwenyezi Mungu amwachishe kutoka kutekwa kwake na mateka wote wa Waislamu.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu kwamba juhudi zenu ziwe katika mizani ya mema yenu

2021 05 08 Naveed Butt Twitter Storm EN

Naveed logo FaceBook

Old Camp en Copy