Chini ya Makucha ya mfumo muovu wa Kibepari Maisha yanaendelea kuwa magumu na dhiki zaidi

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

  Gharama za maisha nchini zinaendelea kuwa juu zaidi kwa kupanda maradufu bei za vyakula na bidhaa nyengine hali inayowafanya raia wa kawaida wakaukiwe mifukoni  na kuwaacha kutapatapa wasijue nini cha kufanya! Wakenya wanaitaka na kuiomba serikali ilioko mamlakani kwa sasa itatue tatizo hili ambalo ndani ya mfumo wa kibepari limekua ni dimbwi la kudumu.

Sisi katika Hizb ut Tahrir tungependa kusisitiza yafuatayo:

Utawala ulioko sasa kattu hautotatua tatizo hili kimsingi ambalo limekua ni kero ya mara kwa mara kwenye tawala za kibepari. Ukweli ukibakia kuwa sera za kiuchumi zinazotokamana na mfumo wa kiuchumi wa kibepari zilizoainisha bei kuwa ndio kigezo kikubwa cha uzalishaji wa rasilimali,usambazaji wake na matumizi ya bidhaa na huduma hivyo kupelekea kuweko kwa mashirika ya watu binafsi wanaomiliki soko peke yao kwa lengo la kujiongezea faida maradufu kwa gharama za mwananchi wa kawaida. Fauka ya haya, kihakika tawala za kibepari kimsingi ndio zinazostahiki kubebeshwa lawama kwa  hali hii ngumu ya kiuchumi kwani zimeegemea mfumo uliofeli wa kiuchumi, kwa maana hii dhana ya kuwa utawala ulioko huu ni msafi wa kutofanya makosa yaleyale yaliyofanywa na tawala zilizopita ni jaribio lake la kuficha kufeli kwa mfumo wa kibepari.

Katika Uislamu ushibishwaji wa mahitaji msingi na uwewezashaji wa kuyafikia mahitaji ya ziada yote ni jukumu linaloangukia serikali. Na kwa kigezo hiki Khalifah huwajibishwa kuiacha  soko kuwa huru yaani kutoingiliwa na genge  maalumu la wafanyibiasha walafi na wanasiasa wachoyo. Hatua hii itafanya soko kimaumbile lijipileke kwa nishati ya mahitaji na usambazaji, hivyo kufanya bei za bidhaa zenye ushindani na nafuu. Isitoshe, Uislamu umetatua tatizo la kiuchumi kwa msingi wa usambazaji wa utajiri(rasilimali) wala sio kama Urasilimali unavyosema kuwa tatizo la kiuchumi ni kupitia uzalishaji.

Kama ilivyoshuhudiwa katika historia ya Ukhalifa wa Umar ibn Al-Khattab (Khalifah wa pili wa katika Dola ya Kiislamu), wakati watu wa jimbo la Hijaz walipokumbwa na njaa kali, alitekeleza sera ya kiuchumi iliohakikisha kwamba hakuna mtu au kikundi chochote kinachoweza kuhujumu soko kwa kutaka kujichukulia faida na mtaji kwa kudhuru watu wakati wa ukame huo.Alichofanya Bin Khattab(r.a) alitoa amri ya kiutendaji kwa Amr bin Al-assi wakati huo akiwa gavana wa Afrika Kaskazini kuongeza usambazaji wa chakula katika soko la Madinah ili kupunguza bei ya juu na njaa.

Tunathibitisha kwamba kwa kusimamishwa tena kwa Khilafah (Ukhalifa), migogoro na matatizo yote ya kiuchumi itatatatuliwa kwa ukamilifu.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari  Hizb ut-Tahrir Kenya