Miaka sitini ya Machungu na Kero

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

Kenya iliadhimisha miaka 60 ya ‘Uhuru’ siku ya Jumane tarehe 12 Disemba mwaka 2023. Kila mwaka, Disemba 12 huadhimishwa  kama  siku ambayo Kenya ilipata kile kiitwacho uhuru kutoka kwa utawala wa  mkoloni mwingereza mwaka 1963.

Sisi katika Hizb ut Tahrir Kenya tunapenda kueleza yafuatayo:-

Baada ya vita vya pili vya dunia, tamko la ‘Uhuru’ lilikuja kumaanisha ukombozi kutoka kwa ukoloni. Maana haya kihakika ni ya kijuu juu. Ukweli ni kuwa Marekani ndiye aliyeibua na kuanzisha mchakato huu ili  kubuni nafasi ya waliokoloniwa wajitoe kwa ukoloni wa mataifa ya kiulaya na kuingia kwenye ukoloni wake.Viongozi wa kisiasa waliotawala baada ya mkoloni Mwingereza, ndio waliofaidi zaidi kwani wao walinyakua maeneo makubwa ya ardhi huku wakiwaacha raia jumla kuwa maskwota.

Mbegu za kuanguka na kuporomoka zilipandikizwa na wakoloni waliokuza mifarakano kati ya jamii na makabila mbalimbali, na kuanzisha mapigano ambapo kila jamii ilikosa imani na jamii nyengine na kuanza kupigana. Viongozi wa kisiasa wakafanya juhudi kubwa ya kufikia kupata maslahi yao ya kisiasa, kiuchumi na kijamii wakitumia mbinu ya kugawanya raia kwa misingi ya kimaeneo na ukabila na kuwa ndio zana ya kufikia mafanikio yao ya kisiasa. Kurejeshwa kwa Demokrasia ya vyama vingi iliyochukuliwa kuwa ukombozi mpya kumeiweka nchi katika migawanyiko ya kikabila na chuki zaidi huku tabaka la kisiasa likitumiwa kuteka nyara misukumo ya umma katika kuweka ajenda zinazolenga kutoa matumaini hewa. Kuzinduliwa kwa katiba mpya ya mwaka 2010 ambayo ilikuja na mfumo mpya wa utawala wa ugatuzi hakujawaokoa raia kutoka kwa matatizo.

Kinachoifanya Kenya kushindwa kutatua matatizo ya kimsingi ya umma ni kwa sababu ya kuegemea kwake mfumo wa kibepari wa kikoloni ambao msingi wake ni akili ya mwanadamu na sio Wahyi kutoka kwa Allah (swt).Utekelezwaji wa Sera mbovu za kibeberu na Serikali zilizotangulia na hata hii ya sasa, kunaaendelea kudhuru Kenya. Ni kupitia mikataba ya kibiashara na mataifa makubwa ya Magharibi kama vile Uingereza na Marekani ambayo yameiacha Kenya na Afrika kwa ujumla zikiwa zimegubikwa na viwango vya juu vya umaskini, njaa na magonjwa.

Ili kupata uhuru wa kweli, tunahitaji mfumo utakaobadilisha kimsingi jamii nao si mwengine ila ni Uislamu. Kwa hakika miaka 60 ni muda wa kutosha kufikia mafanikio makubwa kuegemea mfumo bora wa Uislamu.Mafanikio makubwa yalipatikana ndani ya muda mfupi na viongozi wa kweli walioutekeleza Uislamu kupitia dola huru ya Khilafah. Kwa mfano, Khalifa Umar bin Abdul Aziz (ra) aliweza kuunda jamii isiyo na umasikini kwa muda wa miaka miwili na miezi mitano tu. Hivyo basi, uhuru wa kweli utapatikana tu kupitia utekelezaji kamili wa Uislamu katika nyanja zote za maisha chini ya mwamvuli wa Dola ya Khilafah itakayosimamishwa tena katika mojawapo ya nchi za Kiislamu.

 

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari Hizb ut Tahrir

Kenya