Hazina ya ‘Hustler’: Tungo nyengine mpya ya Mfumo wa Kibepari Ulioshindwa Kusimamia watu Kiuchumi.

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

Katika hatua ya kuwapa mikopo wafanya biashara wadogowadogo ambao wamekua wakitaabika kuchukua mikopo katika benki kubwa, serikali imezindua mfuko wa fedha unaojulikana maarufu Hustler Fund ambapo baada tu ya uzinduzi huo takriban wakenya milioni 17 tayari wamechukua mkopo huo kwa muda tu wa saa moja kwenye siku ya kwanza ya uzinduzi huo.Kipindi cha urejeshaji wa mikopo kitapunguzwa hadi siku 14 katika mpango unaonekana kufungua dirisha kwa wafanyabiashara wadogo kupata mkopo wa bei nafuu. Mfuko huo uliozinduliwa, utaona wakopaji wa kiwango cha chini wakipata Sh500 huku kiasi kikubwa zaidi cha nyongeza kitakuwa Sh50, 000 kwa riba ya asilimia nane

Harakati ya Hizb ut Tahrir Kenya ingependa kubaini yafuatayo:-

Ukweli kwamba kumekuwa na benki zinazotoa mikopo hiyohiyo ya riba na ambayo imezidisha ugumu zaidi kwa raia kawaida na hatimaye kuwanufaisha wale wakopeshaji (wadai), inathibitisha kufilisika kisera kwa siasa na uchumi wa wa mfumo wa Kibepari. Kwa hivyo hazina hii mikopo inayotelewa na serikali ya sasa si lolote ila ubadilishwaji majina mapya ya mikakati ileile ya zamani hivyo katu haitotatua kimsingi matatizo ya kiuchumi ambayo yamekita mizizi ndani ya taasisi za kifedha za kibepari.

Chini ya mfumo unaotegemea pesa za makaratasi (Fiat-Monetary), ambazo kiasili hazina thamani ya kidhati ili tu kupitia kanuni za kiserikali, pesa imefanywa ni bidhaa inayouzwa kwa bei ya riba ambayo inatumiwa na mabepari kunyonya na kuzuia raia wakawaida kujikomboa kiuchumi. Mienendo ya mfumo wa kiuchumi wa kibepari, Riba (riba) hubadilisha sura yake mbaya mara kwa mara  kwa kubadilisha kauli mbiu kama hii ya sasa  ‘Hustler Fund’.

Matatizo ya kiuchumi ya raia hayototatuliwa kwa kutegemea mfumo wa mikopo ya Riba bali ni kwa kupita utekelezwaji wa mfumo wa kiuchumii wa Kiislamu na hapo ndio matatizo hayo yatatatuka kwani umeharamisha vikali riba kwenye miamala yote ya kifedha. Fauka ya haya, kwa kuwa Uislamu unaangalia tatizo la kiuchumi ambalo linapaswa kushughulikiwa ni ugawaji/usambazaji wa rasilimali. Kwa maana haya Khilafah kama serikali huwajibishwa kuchukua sera za kiuchumi zinazolenga kudhaminia kila raia waweze kukimu mahitaji yao msingi  sambamba na kuwawezesha kufikia kukimu mahitaji ya ziada.

Tamati tungependa, kunasihi kidhati  jamii yote kujiweka mbali na miamala yote ya kifedha ya riba kwani MwenyeziMungu amelikemea kwa ukali uovu pale aliposema:

: ﴿الَّذِينَ يَأْكُلُونَ الرِّبَا لاَ يَقُومُونَ إِلاَّ كَمَا يَقُومُ الَّذِي يَتَخَبَّطُهُ الشَّيْطَانُ مِنَ الْمَسِّ ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُواْ إِنَّمَا الْبَيْعُ مِثْلُ الرِّبَا وَأَحَلَّ اللّهُ الْبَيْعَ وَحَرَّمَ الرِّبَا فَمَن جَاءهُ مَوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّهِ فَانتَهَىَ فَلَهُ مَا سَلَفَ وَأَمْرُهُ إِلَى اللّهِ وَمَنْ عَادَ فَأُوْلَـئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ

  1. Wale wanaokula riba, hawasimami (kuendesha yao) ila kama anavyosimama yule ambaye Shetani kamzuga kwa kumsawaa; (wako mbioni tu, hawana kituo). (Na) haya ni kwa sababu wamesema, “Biashara ni kama riba”, bali Mwenyezi Mungu · ameihalalisha biashara na kaiharimisha riba. Na aliyefikiwa na mauidha kutoka kwa Mola wake (ya huku kukatazwa riba), kisha – akajizuia, basi yamekwisha mthibitikia yale (mali) yaliyopita (aliyokwisha yapata); na hukumu yake iko kwa Mwenyezi Mungu. Lakini wanaorejea (kula riba) basi hao ndio watu wa Motoni, humo watakaa milele.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habaroi

 Hizb ut Tahrir in Kenya