Je Ramadhani itaingiza Taqwa mioyoni mwenu ili muweze kuikomboa Filastin?

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari

Hizb ut Tahrir / Kenya kwa furaha, inawapongeza Waislamu wa humu nchini na kote duniani kwa ujumla kwa kuingia kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan. Tunapoingia katika mwezi huu wa rehema, msamaha na kukombolewa na Moto wa Jahannam, tunamuomba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) atujaalie nguvu na afya ya kushika amali adhimu ya saumu ambayo sio kuwa ni wajibu tu bali ni mojawapo ya nguzo tano za Uislamu.

Ramadhani hii inakuja huku ulimwengu ukishuhudia mgongano kati ya matakwa ya Umma wa Kiislamu ya kushikamana na Ardhi iliyobarikiwa ya Filastin na matakwa  ya makafiri wa Magharibi. Umma umeonyesha imani yake kwa Uislamu na kwa dhati unatamani ushindi wa Mwenyezi Mungu. Ulimwengu unashuhudia kufilisika kwa maadili ya Magharibi wanavyounga mkono mashambulizi ya kikatili ya ‘Israel’ huko Gaza. Mataifa ya Magharibi na vyombo vya habari vinaonyesha uhalisia wa unafiki na ubaguzi wao.

Chakusikitisha ni kwamba, unyama wa waziwazi unaofanywa na majeshi ya Kiyahudi dhidi ya ndugu zetu wa Gaza bado haujachemsha mioyo wala mishipa ya viongozi wa Kiislamu na majeshi yao! Enyi viongozi! Je, Swaumu zenu zitaingiza  taqwa katika nyoyo zenu na kuwasukuma muweze kukata mahusiano na umbo la Kiyahudi? Enyi majeshi, je Ramadhani itawapeni taqwa ya kuwapuuza watawala wenu waliomfanyia khiyana Mwenyezi Mungu, Mtume wake na waumini ili muanze kwenda Palestina na kupambana jeshi la Mayahudi?

Katika historia yake yote, Ramadhani imekuwa ni mwezi wa ukombozi na ushindi. Kwa hakika historia hii inayong’ara  itahuisha ushindi katika Vita vya Badr, Qadisiyyah na Ein Jalut. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) atukubalie vitendo vyetu na aujaalie Ummah huu mlinzi na kinga ya Khilafah katika njia ya Utume. Khilafah ambayo itakusanya majeshi ya Waislamu ili kung’oa utawala wa kimauaji wa umbo la kizayuni lna kukomboa sio tu Filastin inayokaliwa kwa mabavu bali ardhi zote za Waislamu.

 

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari  Hizb ut Tahrir

Kenya