KAMPENI YA KUTETEA HAKI ZA MAHABUSU NA DHIDI YA UTEKAJI

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
Kutokana na kuwekwa mahabusu kwa wanaharakati wetu watatu wa Hizb ut Tahrir Tanzania (Ust. Ramadhan Moshi Kakoso, Wazir Suleiman Mkaliaganda na Omar Salum Bumbo kwa zaidi ya miaka miwili sasa bila ya kesi zao kusikilizwa wala kupewa dhamana, pamoja na  kuwa mahabusu mashekhe wa Uamsho ambao wapo mahabusu zaidi ya miaka saba sasa, na wote walioshikiliwa kwa kukosa dhamana wala kesi zao kusikilizwa, Hizb ut Tahrir Tanzania inatangaza kampeni rasmi ya kutetea haki za mahabusu hao.
Kampeni itaanza rasmi kuanzia mnamo tarehe 12 Juni 2020 mpaka 24 Julai 2020, na itakuwa na  sura ifuatayo:
1. Malengo ya kampeni:
a. Lengo la Jumla (general):
Kupaza sauti zetu dhidi ya mambo yafuatayo:
• Uwekwaji mahabusu kwa tuhuma bila ya kushtakiwa
• Hali ya watuhumiwa kunyimwa dhamana
• Upelelezi usio na kikomo
• Watu kutekwa
• Sheria ya Ugaidi
b. Lengo makhsus (specific)
Kupaza sauti ili wanaharakati wetu waweze kutekelezewa utaratibu sahihi wa kisheria ili kesi zao zisikilizwe, wapate dhamana au waachiliwe huru.
2. Maeneo ya Kampeni :
• Mihadhara ya Kiislamu sehemu mbalimbali
• Kutumia mitandao ya kijamii-twitter,facebook,whatsapp,tovuti nk. kwa kuandika makala na kutawanya, vipindi mubashara, video fupi  nk.
• Kuvitaka vyombo vya habari, Tv, redio, magazeti  kuipaza na kuitangaza kampeni hii
• Kuitangaza kampeni hii na kuwashawishi wengine washiriki wakiwemo: wanasheria, wasomi, wanaharakati wa haki za kibinadamu, masheikh, maimamu, wanaharakati wa Kiislamu, makhatibu, maustadh, wanahabari, wanasiasa, wanafikra na watu jumla.
 • Pia kuzihamasisha asasi za kiraia katika kampeni hii hususan za haki za kibinaadamu na asasi/taasisi nyengine mbalimbali nk.
3. Kauli mbiu ya kampeni:
        “Ni dhulma kisheria kuwekwa mahabusu bila ya mashtaka, kunyimwa dhamana, upelelezi usiokwisha na utekaji”
         Ni matumaini yetu kuwa kila mmoja katika jamii atashiriki kikamilifu katika kampeni hii adhimu, kwa  kuwa ajenda yake inamgusa kila mmoja katika upande wa kiimani au wa kibinadamu.
Masoud Msellem
Mwakilishi kwa vyombo vya Habari
 Hizb ut Tahrir Tanzania
#KomeshaUkandamizajiWaKisheriaNaUtekaji

 

REF: 1441 / 02 
Jumatano, 26th Shawwal 1441 AH/
17/06/2020 CE