Hizb ut Tahrir Kenya yafaulu kuandaa semina kuhusu Janga la kiulimwengu la Mfumuko wa Bei

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

 Katika juhudi na hima yake ya kusimamisha tena Khilafah, Hizb ut-Tahrir Kenya ilifaulu kuandaa semina kuangazia jinsi  ya janga la mfumuko wa bei linavyoathiri maisha ya kila siku  ya raia, hususan walalahoi. Tatizo hili linatokamana na mfumo wa kiuchumi wa kibepari ambalo kwa sasa limekuwa ni janga la dunia nzima na kuathiri mambo kama vile:-

-Pesa kukosa thamani#

-Kutokua na usawa wa kiuchumi#

-Kiwango kikubwa cha ubadilishaji wa sarafu#

-Gharama kubwa kwenye kukopa mikopo#

-Ongozeko la gharama ya maisha

-Kutatizwa pakubwa kwa wafanyakazi kwa mfano wanaotaka kulipwa malipo yao ya uzeeni, waajiriwa na kuweka pesa benki#

Semina hii iliandaliwa Mtwapa katika gatuzi la Kilifi tarehe Jumapili tarehe 26 Juni 2022,ambako suala la mfumuko wa bei liliweza kuchambuliwa kwa kina, hasa kiini na sababu zake, pia kuweka suluhisho la tatizo hili kwa kulingana na mfumo wa Uislamu. Semina hii ilihudhuriwa na  wahudhuriaji zaidi ya mia moja.

Wazungumzaji katika semina hii walikuwa wanachama waandamizi wawili wa ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir Kenya; Ali Omar mwanachama wa Ofisi na Ustadh Shabani Mwalimu mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut-Tahrir Kenya

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari Hizb  ut Tahrir Kenya