Zaka na Madeni ya Baba na Mtoto

Ufupisho wa Suali na Jawabu – 14

Suali

Babangu ana madeni mengi. Sasa imekuwa kawaida kutotofautisha kati ya pesa au madeni ya baba na mtoto. Nikimaanisha kuwa madeni pia ni yangu moja kwa moja na sote tunafanya kazi kuyalipa. Lakini suala hili kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu inasemaje hususan kwa mtizamo wa Zaka? Je deni ni la babangu pekee na yuko huru na Zaka au sote tunatakiwa kulipa deni?

Jibu

Pesa za baba kwa mujibu wa Shari’ah sio pesa za mtoto na madeni ya baba sio madeni ya mwanawe, kwa hivyo Shari’ah iweka kuwa kila mmoja wao anasimamia pesa zake. Shari’ah imeweka haki na majukumu juu ya pesa za baba bila kujali pesa za mwanawe. Napia ikaweka haki na majukumu juu ya pesa za mwanawe bila kujali pesa za baba. Kwa sababu kila mmoja yuko huru kijukumu. Mfano Shari’ah imemwajibisha baba kulipa Zaka juu ya pesa zake ambazo zimetimiza Nisab (kiwango cha kutolewa Zaka) na zimepita mwaka mmoja bila kujali pesa alizonazo mwanawe. Mfano Shari’ah imemruhusu mwanawe kupata pesa kwa kutumia juhudi yake bila kujali pesa alizonazo babake. Ushahidi wa hilo ni

“Mwenyezi Mungu anakuusieni juu ya watoto wenu: Fungu la mwanamume ni kama fungu la wanawake wawili” [An-Nisaa: 11]

“Na wazazi wake wawili, kila mmoja wao apate sudusi ya alicho kiacha, ikiwa anaye mtoto” [An-Nisaa: 11]

“Haya ni baada ya kutolewa alicho usia na kulipa deni” [An-Nisaa]

Ad-Darqatny alisimulia kutoka kwa Mtume (saw) kuwa alisema:

“La, lakini kata kucha zako, kata ndevu zako na kata nywele zako za siri, hayo yatakamilisha kafara yako kwa Mwenyezi Mungu.” Hayo yalikuwa majibu yake (saw) kwa mtu aliyesema kuwa lau hatopata chochote cha kuchinja basi atachinja ngamia wa babake au kondoo wa babake Siku ya Adha.

Kwa mujibu wa kauli ya Allah (swt) na ya Mtume (saw) zinaashiria kuwa kila mmoja ana miliki chake na ana jukumu juu yake ima iwe baba au mwanawe. Napia anapokufa jukumu hilo huzingatiwa yeye kama yeye ikiwemo mali yake juu ya wasia wake, deni lake na urathi na wanaorithi.

Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye Hekima.

Link ya Kiengereza: http://hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/qestions/jurisprudence-questions/13564.html

Chanzo: Hizb ut Tahrir Kenya

28 Shaaban 1439 Hijria

14 Mei 2018 Miladi