Ufahamu kuhusu Thamani

Ufupisho wa Suali na Jawabu – 15

Swali

Nina maswali kuhusiana na ufahamu juu ya thamani. Thamani ni kiwango cha manufaa ndani ya bidhaa tukizingatua sifa ya uchache.

  1. Ni zana zipi nitegemee kama mjuzi katika bidhaa fulani ili kujua manufaa ya bidhaa hiyo?
  2. Manufaa yanategemea kuelezwa kwa manufaa pekee au yana thamani ya dhahabu, fedha au juhudi? Ikiwa ndio, toa mfano.
  3. Manufaa ndani ya bidhaa yana thamani na inapatikana vipi?
  4. Nafanya vipi katika kuzingatia kigezo cha uchache katika kuamua thamani na ni yapi mahusiano yake?
  5. Thamani ni eleimu juu ya nidhamu ya uchumi au sayansi ya uchumi?
  6. Kuna umuhimu gani katika kujadili suala la thamani na manufaa katika masomo?

Jibu

Kuanzia Na.1, 2 na 3: Ukitaka kujua thamani na zana zinazotumika kujua, ni manufaa kwa mtu binafsi kama mwanadamu katka kushibisha mahitaji yake msingi napia katika vitu ambavyo vina thamani kivyenyewe mfano dhahabu na fedha. Thamani inajulikana kwa kulinganisha bidhaa na sio bei ya bidhaa. Mfano thamani ya mkate iko juu ukilinganisha ya kileo hata kama bei ya kileo iko juu n.k. Twaweza kueleza kuwa: Thamani ya kweli ya bidhaa ni kipimo cha manufaa yake ambacho hakibadiliki kwa kuwa manufaa yake yamo ndani ya bidhaa yenyewe. Hivyo, katika biashara tunapokadiria thamani inaitwa thamani halisi. Makadirio ya thamani yanafanywa kwa kulinganisha manufaa ya bidhaa iliyopo dhidi ya kitu kilichotumiwa wakati wa kukadiria. Hivyo thamani haikadiriwi na kitu ambacho hakina thamani ndani yake mfano pesa za makaratasi. Na wala thamani haibadiliki ndani ya bidhaa kutegemea wakati maanake thamani yake ipo ndani ya bidhaa sio kugemea wakati.

  1. Thamani ni kiwango cha manufaa katika bidhaa ima tukizingatia au tusipozingatia sifa ya uchache wake katika makadirio. Nukta muhimu ieleweke ni wakati gani unafanya makadirio. Mfano wakati una mkate mmoja na hujui ikiwa utaupata tena basi utaula kwa umakinifu kiasi kwamba hata chembe kikidondoka utakiwahi na kukila. Lakini tuchukulie una mikate kadhaa basi utakula bila umakinifu kwa kuwa hata chembe kikidondoka hautajali kukiokota kwa kuwa unaomkate mwingine utakula.
  2. Thamani elimu yake ni ya nidhamu ya uchumi au sayansi ya uchumi kutegemea muktadha wa elimu hiyo. Lau elimu hiyo ni kuhusiana na mada ya tofauti kati ya thamani na bei, basi itakuwa ni elimu ya sayansi ya uchumi. Hivyo, twasema thamani ni kiwango cha manufaa ndani ya bidhaa yenyewe illhali bei ni kiwango cha pesa zilizolipwa kununua bidhaa hiyo bila kujali ima ina manufaa au la. Maanake huo ni ulinganishaji tu wa maana. Lakini ingelikuwa mada ni biashara basi itakuwa ni nidhamu ya uchumi. Mfano: Mtu amekopa bidhaa fulani yenye thamani ya Dinar 100 za dhahabu na kuirekodi kama mkataba kuwa wakati wa kulipa, arudishe bidhaa hiyo hiyo au Dinar 100 za dhahabu lau itakuwa bidhaa imeharibiwa. Hii ni kwa sababu thamani haibadiliki kwa kutegemea wakati au mahali.
  3. Umuhimu wa elimu juu ya thamani unatokana na tofauti kati ya thamani ya kudumu yenye manufaa ndani ya bidhaa kwa mwanadamu kwa mujibu wa mahitaji msingi na vitu ambavyo vina thamani ndani yake na bei ambayo yategemea ukadiriaji kwa mujibu wa wingi au uchache wa manufaa unaopatikana ndani ya bidhaa. Kupitia nukta hii na nukta Na.4 utagundua kuwa utafiti wa kiuchumi umejifunga katika nyanja mbili:

– Kufanya utafiti wa kiuchumi juu ya thamani, kuwa thamani ina mahusiano na manufaa ambayo yanashibisha mahitaji msingi ya mwanadamu, na vitu ambavyo vina thamani ndani yake inapelekea kujali vitu vyenye manufaa. Kwa maana nyingine inamaanisha kuwa utafiti uwe juu ya yaliyo na manufaa kwa watu na hivyo kuwa ndio msingi wa utafiti ni thamani na utafiti kuhusu bei uje baada yake. Hivyo utafiti huo hautajali kuhusu bidhaa zenye kudhuru hata kama zitakuwa bei ghali kwa sababu hazina manufaa.

– Kufanya utafiti kuhusu bei ndio msingi, na utafiti kuhusu thamani uje baada yake, kutapelekea kujali bidhaa ghali na kuziona kuwa zenye thamani hata kama vitu vyenye madhara mfano vileo na madawa ya kulevya kwa sababu yana bei ya juu na yanaleta mapata makubwa.

Hivyo basi, msisitizo wa mtizamo wa kiuchumi uwe juu ya thamani na kisha ndio bei kama tanzu ya thamani; mtizamo huu hueneza khair na utulivu miongoni mwa watu. Kinyume, na mtizamo wa kicuhumi juu ya bei na kisha ndio thamani kama tanzu ya bei; mtizamo huu unafanya bidhaa zenye bei ya juu kuwa na thamani ya juu licha ya kuwa zinaweza kuwa na madhara kwa jamii, na hivyo mtizamo huu una eneza uhalifu na ukosefu war aha miongoni mwa watu.

Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye Hekima.

Link ya Kiengereza: http://hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/qestions/jurisprudence-questions/13166.html

Chanzo: Hizb ut Tahrir Kenya

29 Shaaban 1439 Hijria

15 Mei 2018 Miladi