Ufupisho wa Suali na Jawabu – 1
- Unayopewa na Taasisi ya Fedha (mfano Benki) kwa sharti ya kuwa utaitumia kwa mujibu wa pesa ulizokuwa nazo katika Taasisi hiyo bila ya kuzidisha (Debit Card). Mfano unakwenda kununua huduma/bidhaa katika duka/soko linalo ruhusu matumizi ya kadi hii alafu Muuzaji analipwa na Taasisi hiyo kupitia kadi hiyo lakini iwe kiwango kinachohitajika kulipwa kimo katika Akaunti yako ndani ya Taasisi hiyo. Kadi hii inaruhusiwa kwa mujibu wa Uislamu kwasababu uhakika wake ni kuwa umeiwakilisha taasisi ile ikununulie bidhaa/huduma kwa niaba yako. Ama ada itakayokutoza taasisi hiyo kwa ajili ya kukuwakilisha hii huingia katika mlango wa mshahara wa wakala na inaruhusiwa.
Mfano: Mimi nimesajiliwa na Taasisi ya Fedha na kupewa kadi. Kisha nikaweka pesa katika Taasisi hiyo mfano Ksh.2,000. Nikaenda katika duka linaloruhusu mteja kununua huduma/bidhaa kwa Kadi. Nikanunua bidhaa fulani mfano kwa Ksh.1,500. Basi Muuzaji huyo atachukua Habari/Taarifa za Kadi yangu kisha atalipwa na Taasisi hiyo.
- Unayopewa na Taasisi ya Fedha (mfano Benki) pasi na wewe kuwa na pesa za kutosha katika taasisi hiyo za kukuwezesha kununua huduma/bidhaa (Credit Card)unayoihitaji kwa makubaliano ya kuwa Taasisi hiyo itakulipia lakini kwa kukutoza pesa ziada. Mfano unakwenda kununua huduma/bidhaa katika duka/soko linalo ruhusu matumizi ya kadi hii hata kama huna pesa katika Taasisi hiyo alafu Muuzaji analipwa na Taasisi hiyo kupitia kadi hiyo lakini baadaye utatozwa ada na Taasisi hiyo kwa kukulipia. Kadi hii hairuhusiwi kwa sababu;
- Taasisi inachukuwa sura ya mdhamini kwa kukudhamini wewe kwa muuzaji (kwasababu huna pesa) alafu kukulipia baada ya kukutoza ada ya kukudhamini. Kwa mujibu wa uislamu, mdhamini hafai kupokea/kulipwa ada kwa kukudhamini
- Taasisi inakukopesha pesa zile alafu unapolipa, utalipa na ziada. Hii nayo ni Riba
Mfano: Mfano: Mimi nimesajiliwa na Taasisi ya Fedha na kupewa kadi. Kisha nikaweka pesa katika Taasisi hiyo mfano Ksh.2,000. Nikaenda katika duka linaloruhusu mteja kununua huduma/bidhaa kwa Kadi. Nikanunua bidhaa fulani mfano kwa Ksh.3,500. Basi Muuzaji huyo atachukua Habari/Taarifa za Kadi yangu kisha atalipwa na Taasisi hiyo.Lakini Mimi itanibidi kulipa Ksh.1,500 na (ZIADA) kwa Taasisi hiyo kwa sababu ya kunidhamini na kunipa mkopo wa Ksh.1,500 ambao niliongeza kulipia gharama zangu.
Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye Hekima.
Link ya Kiengereza: hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/qestions/ideological-questions/15103.html
Chanzo: Hizb ut Tahrir Kenya
15 Shaaban 1439 Hijria
01 Mei, 2018 Miladi