BBI na Siasa za Mwaka 2022

Kujiapisha Raila Odinga kama rais wa watu March, 2018 ilikuwa ni hatua ya kutuma ujumbe kwa utawala wa rais Kenyatta wa kuwepo na nafasi ya mazungumzo. Natija yake kupatikana kwa Handshake iliyozaa jopo kazi la mradi wa ujenzi wa madaraja BBI uliochapishwa  kwenye gazeti rasmi la serikali tarehe 24 Mei 2018. Siku ya Jumanne tarehe 26, 2019, viongozi hao wawili wakapokea rasmi ripoti ya BBI. Siku ya Jumatano 27, 2019 ripoti hiyo ikazinduliwa rasmi kwa umma hii ni baada ya jopo kazi  kuchukua maoni ya baadhi ya wakenya kuhusu ajenda tisa ambazo zote kwa ujumla zinazungumzia kuboresha mfumo wa uongozi, mabadiliko ya kiuchumi upendeleo, ufisadi na utangamano.
Wengi wasiojua uhalisia wa siasa waliamini kwamba muundo wa tume ya  BBI ni wa kuleta marekebisho au ni ripoti ya kiufundi technical report bali. Kiuekweli ukiangalia wanajopo wengi wa BBI utakuta wengi wao ni washauri wa kisiasa wa zamani na wasasa wa vigogo hawa wawili. Hii ni kumaanisha wawili hao ndio walielekeza BBI ni kuiamulia mchakato wake. Kusajiliwa kwake katika gazeti rasmi kulimaanisha kwamba ni mradi wa serikali ambapo itatumia rasilimali zake katika kuchakata michakato yote.
Hivi ndivyo ilivyokuwa, shilingi takriban Bilioni 10 zilitumika katika kuandaa ripoti ya BBI. Ni dhahiri shahiri kwamba BBI ni mradi wa kisiasa unaohusiana na suala kurithiwa kwa Uhuru Kenyatta. Hakuna shaka William Ruto na Raila Odinga wana nia ya kutaka kurithi Uhuru Kenyatta. Japo Raila Odinga hajasema yeye mwenyewe binafsi lakini kauli za wandani wake zinaashiria kuwa yeye huenda akiangia tena kwenye kinyang’anyiro cha urais. Kama vile vile Ruto anaimani kwamba yeye ataibuka kidedea katika kupeperusha bendera ya kuwania urais.
•    Handshake na BBI
Raila amekua kifua mbele katika kuuza BBI kwa raia na amekua akitumia mbinu inayojulikana kama “Populist Aproach” Mbinu hii amekua akiitumia sana katika kampeni zake na kufaulu kuteka watu. Suala la BBI limekua ni mmoja wapo ya mkakati mpya wa Raila Odinga na hii ni kama alivyosema yeye mwenyewe kwenye mazishi ya mama wa aliekuwa mbunge wa GEM  Joe Donde: “You have seen me change tack, this is strategy. There are several ways than can lead us to where our ambition is.” Kupitia kwa BBI anaonekana kupanga timu inayowahusisha watu kama vile Ann Waiguru, Wyclife Oparanya, Fred Matiang’I na Eugen Wamalwa.
Mbali na haya kuna kwa kuruhusu maazimio ya watu wa pwani kama yalivyosomwa na Amazon Kingi ni kuuitia sura zaidi ya kitaifa na wala isionekana ni mradi wa watu wawili. Hatua hii ya Raila imetia kiwewe wana Tangatanga wanaolalia upande wa naibu rais William Ruto walioana kwamba ajenda ya BBI itakwaza maslahi yao ikiwemo uwaniaji wa urais.
•    Siasa za MT Kenya
Mwaka 2016, William Kabogo alipasua mbarika kwa kusema kwa  Ruto atahitajika kufanya kazi ya ziada kutafuta kura za wakikuyu. Baada ya kaimu mwenyekiti  wa Jubilee David Murathe kujiuzulu, aliwahutubia  wanahabari  January 2019 kwa kusema: “I now find that it is no longer tenable to stay on as the party vice-chairman, given that I will have to sit in the same National Executive Council with a man I am taking to court to block from running for president,”  Aidha,ashawai kusema kwamba  eneo la Mt Kenya halina deni na Ruto.
•    Vita dhidi ya Ufisadi.
Kuna lalama nyingi sana za wandani wa Ruto kwamba vita dhidi ya ufisadi vinalenga Ruto. Oscar Sudi na senata Murkomen wamekua wakimtaja mkurugenzi mkuu wa uchunguzi wa makosa ya jinai George Kinoti kuwa anatumiwa kumpiga vita Ruto. Akihutubia kongamano la LSK Mombasa, Ruto alisema:“A war on corruption that lacks integrity ceases to be a war on corruption and becomes corruption itself. A war that lacks integrity is impunity. An integrity war waged selectively, using convenient half-truths, with political outcomes in mind, is impunity,”. Yaliyofanywa Sonko na hivi punde Ferdinad Waititu yamechochea upande wa Ruto kuona ni jaribio la kukwaza kampeni za Ruto. La muhimu kufahamu ni kwamba rasilimali ni muhimu sana katika siasa na uchaguzi. Hivyo vita hivi ni kumdhoofisha Ruto uwezo wake wakifedha asiweze kuzitumia katika kununua watu na kujifanyia kampeni kisiasa mbinu hii huitwa containtment policy
Kimantiki ukiangalia mapendekezo yote ya BBI utafahamu hakuna ajenda mpya ndani yake ila ni karata nyengine ya kisiasa inayochezwa na wababe wa kisiasa dhidi ya raia. Ukitafakari kwa kina utatambua kuwa mapendekezo yote hayo kiasili ni majukumu ya serikali kuyatekeleza. Hii ina maanisha kazi ya serikali ni kusimamia raia wake waweze kufikia mustawa wa juu ya kiuchumi na kijamii masuala yasohitaji tume wala ripoti.
Kwenye hotuba yake katika mkutano uliofanywa Mama Ngina Water Front Jijini Mombasa Raila alisema:”No one cannot stop Reggea” kumaanisha ngoma inayopigwa na vigogo wa kisiasa hakuna budi ila raia wataicheza tu! Mwandishi wa Makala Dkt Wandia Njoya amaitaja BBI kama Tangazo la vita la wabababe wa kisiasa dhidi ya raia  wababe wa kisiasa”declaration of war by the political elite on the people”.
Kwa kuwa raia wengi wana ukosefu wa kile kiitwacho ufahamu halisi wa kisiasa ‘political awareness’ basi wanasiasa hupatiliza hali hii na mara kwa mara huwahadaa wa kuwawekea raia mbeleni suluhisho walitakalo wao wanasiasa. Fauka ya haya matatizo yanayokumba jamii nzima leo licha ya kuwa yamesabishwa na mfumo muovu wa kibepari unaofaidi tu tabaka la kisiasa, raia kwa upande wao siku zote huwa na kiu cha mabadiliko na hapo ndipo wanasiasa hupatiliza kuwazushia ajenda zinazoteka hisia zao.
Tofauti za wanasiasa zinazoibuka kila wakati na hasa kwenye ajenda za kisiasa ni tofauti za kimaslahi baina yao wala sio kwa msingi wa kujali maslahi ya raia. William Clay alisema; ‘ This is quite a game,Politics. There are no permanent enemies and no permanent friends,only permanent interests.’(Huu ni mchezo tu  katika siasa hakuna maadui wa kudumu wala marafiki wa kudumu bali yaliyoko ni maslahi ya kudumu).
Mantiki ya maneno haya ni kwamba wanasiasa hutofautiana na kukubaliana kwa maslahi hivyo tofauti zao haziko katika kujali wala kulinda maslahi ya umma. Kambi moja ni ile inayotaka kudhibiti hali ilioko inayowafaa status-quo na upande mwingine ni kutaka kuibadili hali hiyo iweze kwenda watakavyo wao ili ioane na maslahi yao. Cha msingi kwenye kung’angania madaraka wao hutumia mbinu za kufarikisha raia kwa kuwapandikiza chuki za kieneo na kikabila hivyo hawa katu lengo la kuunganisha umma.
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut-Tahrir Kenya.