Hizb ut-Tahrir Kenya yafaulu kuhitimisha kampeni yake  chini ya  kauli mbiu- Kila Mmoja wetu ni mchungaji

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kwa rehma za MwenyeziMungu Swt, Harakati ya Hizb ut-Tahrir Kenya iliweza kuhitimisha kampeni yake ilioanza tarehe 25 Agosti, 2020 na kutia nanga tarehe 31 Disemba 2020. Kampeni hii ilijikita katika kuonesha kiini hasa cha matendo ya kingono na mimba za wanafunzi wa shule nchini Kenya zilizoripotiwa kufuatia kufungwa kwa shule kwa sababu ya maambukizi ya janga la Covid-19.

Kwenye kipindi chote cha kampeni, Hizb ikaweza kufanya darasa mbalimbali misikitini, matembezi ya mitaani na midahalo mubashara kwenye mitandao miongoni mwa amali nyengine. Amali zote zililenga  kufichua jinsi gani zaidi Mfumo wa kirasilimali na itikadi yake mbovu ya kiilmaaniya ilivyochangia sio maovu ya kijamii bali maovu katika nyanja zote za maisha. Kwa ujumla, Ummah wa Kiislamu ukakumbushwa aidha majukumu yake katika kuwakinga watoto dhidi ya uchafu na muozo wa tamaduni za kimagharibi kwa kuhakikisha kwamba wanajukumika katika kuunda utambulisho halisi wa Kiislamu kwa watoto.

Kampeni hiyo ilitumia hashategi:-

# Covid-19_inafichua_Urasilimali

 #Covid -19 _Usekula _ unatenganisha Dini  

 #Covid-19   Majanga ya umma _Hupatilizwa Na warasilimali kujipatia faida.

Tunamuomba MwenyeziMungu SWT atakabali amali zetu na kuturuzuku Khilafah kwa mfumo wa unabii itakayolinda kizazi chetu na umma kwa ujumla dhidi ya makucha ya mfumo fisidifu wa kibepari.

 

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari

 Hizb ut Tahrir in Kenya