Janga la virusi vya Corona: Serikali isikwepe kidole cha lawama

Police in Kenya use tear gas to enforce coronavirus curfew | South ...

Huku idadi ya maambukizi na vifo vinavyotokamana na maradhi ya COVID 19 ikiendelea kukua kwa kasi kote duniani, serikali ya Kenya inaonekana ikikwepa kidole cha lawama badali yake inakielekezea raia wake kwa kile ilichokitaja ukosefu wa nidhamu miongoni mwa wakenya.Kufikia tarehe 26 March,2020 kisa cha kwanza cha kufariki dunia kwa sababu ya Corona kiliripotiwa huku siku ya kabla yake kukaripotiwa kupona kwa mtu mmoja. Kufikia sasa, jumla ya visa 31 vya walioambukizwa maradhi haya hatari vimethibitishwa.

Hatua ya hivi karibuni iliochukuliwa na serikali kama jaribio la kudhibiti usambaaji wa virusi vya Corona, ni amri ya kutotoka nje kwa raia kuanzia saa moja jioni hadi kumi na moja alfajiri. Mbali na hatua hiyo, siku kadhaa zilizopita, nyumba za ibada zikafungwa pamoja na shule. Kumehimizwa pia hatua ya kuepuka misongamano ya watu. Haya yote yakiwa ni mikakati inayodhaniwa kuwa hatua za kukabiliana na janga la Corona.

Tukichunguza uhalisia wa maisha ya raia wengi ambao kwa ujumla wao ni hohehae na hali mbovu ya sekta muhimu kama vile za usafiri utafahamu kuwa kuna changamoto kubwa zinazoikabili serikali ambayo kuja na mikakati hiyo ni kujisahaulisha kusudi. Matokeo yake ni kuja na mikakati ambayo ndio imezusha zaidi balaa. Usafiri wa umma nao ni hatari kabla hata ya kutokea majanga huku ikijulikana wazi jinsi sekta ilivyokosa nidhamu. Abiria husongamana sio tu kwenye vituo bali hata ndani ya matatu hurundikana kama magunia ya makaa! Msongamano wa magari ni sokomoko la kawaida mijini. Barabara ambazo hugeuka kuwa mito maji kwa mvua tu chache huku mvua ikizidi ndio balaa.  Kwa mfano, kinachofanyika sasa kwenye kivuko cha feri pwani ya Kenya ni hali hatarishi zaidi kwani hata uwepo wa vikosi vya usalama ndio hasa vimeleta tafrani zaidi kwa abiria hadi wengi wao wakililia na kusema tunamalizwa na askari kabla hata ya Corona inayotukodolea macho!

Kenya Taking Drastic Measures to Curb Coronavirus Spread | Voice ...

Kwa kuwa raia wengi hutegemea uchumi kijungu mwiko ambao hulazimika kuhangaika kutafuta vibarua tayari kuweka ilani ya watu kuepuka maeneo ya watu wengi hili ni jambo linalotatiza zaidi maisha yao. Ikiwa masoko ambayo hutegemewa na mama mboga kuendeleza vibanda vyao vya mboga yanafungwa huku hakuna njia mbadala, ina maana ni kumbana mama huyu kupitia biashara yake hiyo ambayo ndio njia pekee ya kina mama wengi  hukimu mahitaji yao na ya familia zao. Suala la kujitenga hilo nalo lina changamoto yake hasa ikizingatiwa kwa raia waishio kwenye mitaa ya mabanda katika miji mikubwa. Nani asiejua familia kubwa kubwa hujazana tu kwenye chumba kimoja tena kidogo. Kwa mfano Jiji la Nairobi lenye idadi ya wakaazi milioni nne takwimu zinaonyesha kwamba thuluthi mbili ya wakazi wake huishi kwa kusongamana kwenye mitaa duni ya mabanda.  Isitoshe hali ya uchafu na maji taka imekuwa ni jambo lililozoeleka kwenye mitaa hiyo. Je watu hao wataweza kweli kujikinga na mkurupoko wa Corona ilhali hatua ya kuosha mikono ni changamoto?

Ukiachilia mbali matatizo haya kuna tatizo jengine nalo ni ukosefu wa vitendea kazi kwa wahudumu wa Afya ambao ndio haswa wanaotarajiwa kuwa na msaada mkubwa katika kukabiliana na virusi vya Corona.

Hali hii ya sasa inayoshuhudiwa isengifika kiwango hiki lau serikali ingelichukua hatua za mapema kama kuweka vidhibiti katika viwanja vya ndege baada tu kupata habari za mkurupuko wa virusi vya Corona. Ikumbukwe mwanzoni mwa Mwezi March,kabla hata hakuja ripotiwa kisa cha kwanza virusi vya Corona nchini kamati ya masuala ya afya ya bunge ililalamikia utepetevu wa wakuu wa wizara tatu husika; ya usalama wa ndani, ya uchukuzi na ile ya afya. Visa vyote vya maambukizi vilitokamana na abiria waliokuwa wanatoka mataifa ambayo tayari yalikuwa yameripotiwa maradhi.

Kwa mazingara haya hatarishi hapa ni Mungu asaidie! Mungu saidia hapa ni kumaanisha kunahitajika uangalizi wa uhakika wa kiserikali wenye mipango imara na nia ya kikweli ya kusimamia maisha ya watu. Janga hili la Corona linaendelea kufichua sifa ya kutojali maisha ya watu ndani ya mfumo wa kirasilimali na dola zake. Dola ya Khilafah pekee ndio inayohitajika leo kwani asili inatekeleza mfumo ulio na sera za kujali maisha ya watu pasina na kujali rangi wala dini. Mkurupuko wa maradhi ndani ya Khilafah yatachukuliwa kama kadhia ya kibinadamu wala sio ya kiuchumi inayogeuzwa kama kitega uchumi kwa warasilimali.

Kuna umuhimu wa jamii kuchukua tahadhari kwani kinga ni bora kuliko tiba. Kuosha mikono mara kwa mara na vitakasa na kutulia nyumbani baada ya shughuli za kuhangaika na maisha ni hatua nzuri za kujikinga na maradhi haya.

Dunia leo inahitaji uongozi mpya wa kiulimwengu ili kuwatoa watu kwenye kiza na kuwapeleka kwenye nuru na kutoka katika jeuri ya usekula na urasilimali wake na kuwapeleka kwenye uadilifu wa Uislamu na Dola yake (Khilafah ya Uongofu ya pili kwa njia ya Utume). Na hakika muda wake umefika kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu zisizoshindwa na Mwenye kuhimidiwa, na hasa baada ya kupita miaka 99 tangu kuanguka kwake huko Istambul.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut-Tahrir Kenya