Katiba za kutungwa na Wanadamu ni rahisi kukengeukwa na kubadilishwa

Habari na Maoni

Habari:

Mahakama ya upeo imetoa uamuzi wa kuisambaratisha mradi wa ujenzi wa madaraja lakini ikafungua dirisha kwa vinara wa makubaliano ya ‘handshake’ kuanzisha marekebisho  mpya ya kikatiba. Kweny uamuzi wake wa kihistoria, siku ya Alhamisi 31st March,2022 jopo la majaji saba  ilibatilisha hoja tano za mahakama ya rufaa ilizotumia kupinga mabadiliko ya kikatiba kama yalivyopendekezwa na mradi wa BBI. Miongoni mwa masuala muhimu yaliyotajwa na mahakama ya juu ni kwamba Katiba ya Kenya haina msingi wa kikanuni ‘basic structure’ kumaanisha kwamba hakuna kipengele cha kikatiba kinachowezwa kurekebishwa maadam sheria ni yenye kufuatwa.

Maoni:

Ni bayana kwamba uamuzi wa mahkama kuu kuhusu BBI umeonesha udhaifu mkubwa Demokrasia inayodai kwamba ubwana ni watu yaani kuwa mwanadamu ana mamlaka ya kutunga kulinda na kuhifadhi kanuni.Kanuni za kutungwa na wanadamu hukabiliwa na ukiukwaji na mabadiliko,kwani kwa uhakika kiasili mwanadamu ni dhaifu, mwenye mapungufu na mwenye upeo maalum. Kwa hivyo hata hiyo nadharia ya  mfumo wa kimsingi hausalimiki na kutovunjwa kwani mwanadamu ni mwenye kupelekwa na maslahi.

Mabadiliko ya kikatiba ya Kidemokrasia ambayo mara kwa mara hufanyika kwenye mataifa mbalimbali kwa hoja kuwa jamii hukabiliwa na durufu hivyo kuweka mazingira ya kuhitajika mabadiliko ya katiba ni dalili nyengine ya ajizi ya mwanadamu na mapungu yake ya kutoweza kuweka sheria zinazodhamini mahusiano mazuri katika jamii. Uhalisia wa katiba za kutungwa ni kuwa haziwezi kuachwa kufanyiwa marekebisho kwani haziwezi kukabiliana na kipengele cha wakati na hii ni kama inavyoshuhudiwa kwenye katiba zote za kutungwa zilizoko duniani.

Kwa kuwa huwa ndio ukweli usiopingika, mwito wa marekebisho ya kikatiba na mabadiliko ndani ya jamii ya Kidemokrasia kamwe haitokoma. Mchakato huu utaendelea kusababisha mivutano ya kisiasa na vutevute huku jamii siku zote ikiachwa kwenye ombwe. Kosa kubwa la Demokrasia lipo katika katika kumpa mwanadamu mamlaka ya ubwana wa kutunga kanuni huku ikikana  mamlaka hayo kwa MwenyeziMungu muumba wa mwanadamu, uhai na ulimwengu alien a haki pekee ya kuongoza wanadamu na kuweletea sheria.  Kwa hakika mwanadamu anahitaji muongozo ambao bila shaka lazima uwe ni wenye kutoka kwa MwenyeziMungu (swt) Uongozi huu ni sheria (Quran na Sunna) hivyo kufaulu au kufeli kunategemea katika kushikamana au kutoshikamana na sheria hizi.

Kwa kufikia kwenye ukombozi halisi kutokana na kasoro na dosari za siasa ya Kidemokrasia inayotokamana na itikadii ya kiilmaania (kutenganisha Dini na Maisha) ambayo ndio msingi ambao juu yake umejengwa mfumo wa kibepari, Jamii nzima wakiwemo wasomi , mufakirina na wanasiasa lazima wafanye kazi ya kufikia kwenye mfumo wa maisha unaotegemea maongozi ya   MwenyeziMungu ambayo bila shaka hayafanyiwi marekebisho wala kuwa na uongozi wenye sifa ya uchu na tamaa za kibinafsi.

Binadamu anahitaji katiba ifaayo kwani huo ni waraka muhimu unaoainisha sura ya mfumo wa utawala na kuunda mkataba kati ya watawala na wananchi na vile vile kuwa kielelezo cha itikadi na maadili ya watu wanaowaongoza katika nyanja zote za maisha. Uislamu ukiwa ni itikadi toshelezi umethibitisha hitajio kubwa la katiba lakini ukafafanua kwa uwazi kwamba sheria ya Mwenyezi Mungu iliyoteremshwa na Muumba (Allah Ta’ala) lazima iwe ndio msingi wa katiba inayoongoza wanadamu  chake ubinadamu. Katiba hii inaweza tu kutekelezwa kwa njia ya Khilafah hali ambayo kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu itakuja haraka..

Imeandikwa kwa niaba ya Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir na

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyomba Vya Habari

 Hizb ut-Tahrir Kenya