Kutupilia mbali kesi ya Hijab ni dalili kwamba haki za Waislamu ndani ya katiba za Kisekula haziwezi kudhaminiwa.

 

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kutupilia mbali kesi ya Hijab ni dalili kwamba haki za Waislamu ndani ya katiba za Kisekula haziwezi kudhaminiwa.

Mahakama kuu imetupilia mbali kesi iliowasilishwa mbele yake kuhusu ombi la kutaka uamuzi wa kesi ya iliowasilishwa kupinga uamuzi wa shule ya St Paul Kiwanjani kuwazuia wanafunzi wa Kiislamu kuvaa hijab. Uamuzi huo wa mahakama umeshikilia ule wa awali uliotolewa mwezi Januari mwaka jana ambapo ulianisha uamuzi wa mahakama ya rufaa uliozuia uvaaji wa Hijab shuleni.Miongoni mwa masuala yaliyowasilishwa katika ombi la kesi hiyo ni kutaka mahakama ipitie tena upya uamuzi uliotolewa mwaka jana kwani hakuzingatia masuala nyeti ya kikatiba bali uliamuliwa tu kwa msingi wa makosa ya utaratibu wa kikanuni.

Kufuatia uamuzi huu tunasema yafuatayo:-

Huku katiba ya mwaka 2010 iliotajwa kama katiba endelevu inayodhaminia raia wote uhuru wa kuabudu na wa maoni, kwa upande mwengine bado inabania raia wengine uhuru wao huo.Kwa kuegemea masuala ya “makosa ya kiutaratibu wa kikanuni”, Mahakama inakataa kuwapa wanafunzi wa Kiislamu haki zao na kuunga mkono hatua ya kiubaguzi ya usimamizi wa shule kuwanyima haki hizo. Uamuzi huu unatolewa huku ikiwa Wanafunzi wa Kiislamu katika maeneo mbalimbali nchini wanakumbana na changamoto nyingi katika masuala yanayoambatana na Dini yao. Baadhi ya shule zikiacha kuwapa  wanafanunzi wa Dini ya Kiislamu sehemu za kuabudu na huku nyengine hasa zikilazimisha wanafunzi hao kuhudhuria ibada za dini nyenginezo.

Uamuzi huu ni shambulizi kubwa dhidi ya Uislamu hasa tukizangatia kuwa Hijab ni amri ya MwenyeziMungu kwa wanawake wa Kiislamu. Tunaona hatua hii ni sehemu ya kampeni kubwa duniani dhidi ya Waislamu. Ulimwengu unajua wazi jinsi ya utawala wa Kichina unavyonyanyasa Waislamu wa Kiughuri ukitumia mbinu za kijabari kama vile kuwazuia kutekeleza ibada zao, kufunga misikiti na kuwazuia ibada ya swaum katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Matendo haya ya kihuni ni ukiukwaji wa haki msingi za binadamu.

Katiba za kisekula hazitoweza kabisa kudhaminia haki za Waislamu ambao wamekalifishwa kufuata sheria za Muumba (Swt). Uamuzi umeonesha wazi urongo wa miito ya uhuru na haki za binadamu inayotajwa kuwa ni yenye kulindwa ndani ya siasa ya Demokrasia kama wanavyoipigia debe maliberali wa kisecular. Ni bayana kuwa miito ya uhuru na ile iitwayo haki za binadamu ni urongo na hadaa kwa Waislamu. Kwa haya, tunatoa mwito kwa Waislamu na hasa wanavyuoni kutopoteza juhudu zao kwa kutafuta marekebisho ya kikatiba kama suluhu ya matatizo ya umma, badali yake wanawajibika kufanya kazi kwa ajili ya kuutawalisha Uislamu ambapo haki zote za Waislamu bali za wanadamu wote zitalindwa. Tuna Imani kubwa kuwa Uislamu kupitia Al-Khilafah  Raashidah kwa mfumo wa bwana Mtume (SAAW) itadhamini haki zote za raia wake.

 

Shabani Mwalimu,

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari,

Hizb ut Tahrir in Kenya.

Simu: +254707458907

Pepe: mediarep@hizb.or.ke