Kuwapokonya Ummah Utawala wao, Kuwakandamiza na Kushambulia Matukufu yao ni Moja katika Uhalifu Mkubwa dhidi ya Uislamu na Waislamu
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
(Imetafsiriwa)
Tawala za ukandamizaji na udhalimu hususan utawala wa kihalifu na ukandamizaji wa Ash-Sham, umekuwa ukiwapokonya Ummah maamuzi yao, ukiyakosea heshima matukufu yao, na kuwafuatilia kinyama kupitia taasisi za ujasusi ili kuwatia hofu kiasi kwamba watu wameshindwa mpaka kuzungumza na ndugu zao kuhusu masuala ya ummah.
Baada ya mapinduzi ya baraka ya Ash-Sham, watu waliokiuka wa Ash-Sham walifaulu kuuvunja ukuta wa hofu na kujawa na ushujaa ambao ulipindua uhalali wa nidhamu ya mauaji na uhalifu na kuifedhehesha.
Kutokana na kuchipuza kwa makundi tofauti tofauti kutoka kila upande na majina na miungano ya viongozi wake wa nchi za kigeni kupitia pesa za kisiasa zilizo na sumu, basi mtizamo wa makundi haya ulibadilika kutoka kufanya kazi kuupindua utawala hadi kuanza kulazimisha udhibiti wa maeneo ambayo yamekombolewa na kupigana wenyewe kwa wenyewe ili kuongeza udhibiti huu.
Kwa kiu yao na kukosekana kwa akili iliyo makini na kuwepo kwa akili ya kidhalimu, makundi yalijikita katika matendo ya ukandamizaji na kufanya kazi ili kuwapokonya watu mamlaka yao tena, na wakadidimia zaidi na kuanza kushambulia mali binafsi na kuyakosea heshima matukufu na kumwaga damu kiholela. Hivyo basi, watu wamepoteza imani juu ya makundi hayo ambayo yametia hofu katika mioyo ya wengi katika Ummah waliowapa ushirikiano kutokana na matendo yao ya kiusalama.
Matendo ya kidhalimu na mashambulizi juu ya matukufu na mali za kibinafsi sio tu hatua walizochukua pekee, bali kulianza kusikika sauti za “uhalali” hapa na pale ili kuweza kupatiliza fursa za kuhalalisha matendo yao ya kiusalama wa ukandamizaji na uvamizi wa matukufu ya watu. Hayo ya kiashiriwa na nafasi zao kwa mujibu wa uamuzi na uhalalishaji uliodaiwa kutumika ili kupigana baina yao na kuipa pumzi nidhamu ya mauaji na uhalifu ndani ya Damascus.
Tunawakumbusha wale mukhlisina katika Mujahideen wetu ndugu zetu wasitiwe katika mtego na kuwakandamiza watu wao na uungwaji mkono wao. Tunawakumbusha uhalifu wa kwenda kinyume na matukufu ya mali binafsi na dhuluma juu ya watu. Hawakuja katika mapinduzi haya isipokuwa ni kwa ajili ya kuondosha ukandamizaji na dhuluma juu yao na watu wao ambao ndio msaada wao mkubwa, wakiwapoteza hawatokuwa na uungwaji mkono wala msaada. Ni msaada wa kirongo tu ambao utabakia, kisha nao utaondoka punde tu ukweli utakapo bainika. Kabla ya hapo, tunawakumbusha kuhusu Hadith ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw): «الظُّلْمُ ظُلُمَاتٌ يَوْمَ الْقِيَامَةِ» “Ukandamizaji utakuwa giza Siku ya Kiyama.” [Sahih].
Kwa hiyo chungeni msifanye dhuluma na kuweni makini na wale wanao waamrisha muitekeleze kwa kuwapa uamuzi wa kupotosha. Na rudini kama mlivyokuja katika mapinduzi, mnusuruni Mwenyezi Mungu na Dini Yake na unganeni na watu wenu na ndugu zenu wanaosubiri msaada wenu baada ya msaada wa Mwenyezi Mungu ili muwanusuru dhidi ya wakandamizaji na wala sio kuwasaidia wakandamizaji dhidi yao.
Tunawakumbusha watu wetu ambao wanabidii ndani ya mapinduzi ya Ash-Sham na ni wanaume ambao wamekwenda kinyume dhidi ya tawala ovu mno katika ukandamizaji na uhalifu pamoja na taasisi zao za usalama na majeshi. Wamejitoa muhanga kwa lengo hilo la mapinduzi kwamba lazima waisitishe mikono ya mkandamizaji na wakandamizaji wapya. Kunyamazia ukandamizaji wao, utazidisha udhalimu juu yetu. Mtume wetu (saw) anatuamrisha sisi kuisitisha mikono ya madhalimu na wakandamizaji. Yeye (saw) amesema:
«كَلَّا، وَاللَّه لَتَأْمُرُنَّ بِالْمَعْرُوفِ، وَلَتَنْهَوُنَّ عَنِ الْمُنْكَرِ، ولتَأْخُذُنَّ عَلَى يَدِ الظَّالِمِ، ولَتَأْطرُنَّهُ عَلَى الْحَقِّ أَطْراً، ولَتَقْصُرُنَّهُ عَلَى الْحَقِّ قَصْراً، أَوْ لَيَضْرِبَنَّ اللَّه بقُلُوبِ بَعْضِكُمْ عَلَى بَعْضٍ، ثُمَّ ليَلْعَنكُمْ كَمَا لَعَنَهُمْ»
“La, kwa Mwenyezi Mungu, ima uamrishe mema au ukataze maovu na uushike mkono wa mkandamizaji na umnasihi atende haki na ashikamane na ukweli, au Mwenyezi Mungu ataijumuisha mioyo ya baadhi yenu na mioyo ya wengine na atawalani nyinyi kama Alivyo walani wao.” [Abu Dawud na Tirmidhi]
Na munaweza kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na kwa kumuamini Yeye mkawashinda wakandamizaji na kuwabadilisha na kuwaweka mukhlisina katika ndugu zenu.
Mamlaka ya kweli ni yenu, msiyapoteze na wakabidhini tu wale wanaostahili, msipoteze juhudi zenu, na kuweni macho msiwategemee wakandamizaji. Hivyo basi, kwa mara nyingine kuweni na imani na Mwenyezi Mungu na mkataba wenu Naye Azza Wa Jal, kwa kumnusuru Yeye na Dini Yake na mufanye kazi na wale wanaoshikamana na Dini Yake na musimamishe Sheria Yake chini ya kivuli cha Khilafah kwa njia ya Utume. Khilafah itasimamia mambo ya watu kwa mujibu wa sheria za Mwenyezi Mungu (swt) na kutimiza haki za watu na kuondosha ukandamizaji na wakandamizaji kupitia uadilifu.
Mwenyezi Mungu (swt) Asema:
(وَاللَّهُ غَالِبٌ عَلَى أَمْرِهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ)
“Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui”. [Yusuf: 21]
Ahmad Abdul Wahhab
Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah ya Syria
H. 26Rabi’ I 1440 | Na: 1440 / 004 |
M. Jumanne, 04 Disemba 2018 |