Malipo ya Deni lililopita Muda

Ufupisho wa Suali na Jawabu – 9

Suali

Ni nani ambaye anabeba mzigo wa tofauti ya sarafu ikiwa mkopaji amechelewa kulipa deni kwa mkopeshaji bila sababu, kwa mfano, miaka kumi, ima deni liwe ni mshahara au mkopo.

Jibu

Mshahara unaofaa kulipwa ni kama deni, yeyote anaye daiwa na mtu mwengine, ni lazima kutimiza kulipa kwa mujibu wa makubaliano kati yao. Lau mkopaji/mdaiwa  atachelwa katika kulipa deni, huzingatiwa: ikiwa amekabiliwa na uzito, basi anaedai lazima ampe muda mpaka ajimudu hali yake ya kifedha na aweze kulipa deni kama alivyosema Mwenyezi Mungu (swt):

وَإِنْ كَانَ ذُو عُسْرَةٍ فَنَظِرَةٌ إِلَى مَيْسَرَةٍ

“Na akiwa mdaiwa ana shida, basi (mdai) angoje mpaka afarijike. [Al-Baqara: 280]

Ikiwa mdaiwa anaweza kulipa lakini asilipe deni lake analazimishwa kulilipa na akikataa ataadhibiwa kwa mujibu wa alivyosimulia Abu Dawud na Ibn Majah kutoka kwa ‘Amr bin Sharid kutoka kwa babake kwamba Mtume (saw) alisema:

لَيُّ الْوَاجِدِ يُحِلُّ عِرْضَهُ وَعُقُوبَتَهُ

“Yeyote ambaye anaweza kulipa deni lakini akachelewa kulipa, heshima na adhabu yake imeruhusiwa.”

Maana ya “Lai Alwajd” katika Hadith ni kuchelewa kwa tajiri, maana ya heshima yake imeruhusiwa ni kumlalamikia na kumkemea kwa maneno, na maana ya adhabu yake ni kufungwa na kuwekwa kizuizini.

Ama kuhusu tofauti katika sarafu yaani thamani yake kupungua au kuzidi ikilinganishwa na dhahabu au fedha wakati wa bisahara sokoni, anaye beba mzigo wa tofauti kwa mujibu wa rai yenye nguvu kwa mtazamo wangu ni kuwa ulipaji wa deni uwe kwa sarafu ile ile na kiwango kile kile ambacho kimethibitishwa katika deni ili kuepuka Riba wakati unapochukua kiwango cha zaidi. Hii ni ikiwa sarafu ipo katika mzunguko na inatambulika rasmi na taasisi iliyoiidhinisha.

Na ikiwa mkopeshaji anataka kuhifadhi pesa zake kutokana na kupungua thamani, basi ni akopeshe kwa dhahabu au sarafu yenye nguvu iliyo na uwezo wa kubakisha thamani yake

Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye Hekima.

Link ya Kiengereza: http://hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/qestions/ideological-questions/7145.html

Chanzo: Hizb ut Tahrir Kenya

23 Shaaban 1439 Hijria

09 Mei 2018 Miladi