Kuomba Mkopo kutoka Nchi za Kigeni na Taasisi za Fedha za Kimataifa

Ufupisho wa Suali na Jawabu – 8

Suali:

Imenukuliwa katika kitabu cha Mali katika Serikali ya Khilafah kwamba imekatazwa na Shari’ah kukopa kutoka nchi za kigeni na taasisi za fedha za kimataifa kwa sababu haiwezikani mpaka kupitia riba na masharti.

Je ni wakati gani kukopa kutaruhusiwa, na ni masharti gani ambayo yanafanya ikatazwe? Je kuna tofauti ikiwa nchi hizi tuko na mkataba nao au vita?

Jibu:

Ina onekana umeghafilika maanake kilichonukuliwa katika kitabu Mali katika Serikali ya Khilafah. “Kukopa katika nchi za kigeni na taasisi za fedha za kimataifa, hairuhusiwi na Shari’ah kwa sababu mikopo hayo hayapeanwi isipokuwa ikiwa na riba na masharti”.

Wewe umechukuliwa nukuu hiyo kumaanisha kuwa inawezekana kukopa ikiwa kutakuweko na masharti ya kuruhusu kukopa kutoka nchi za kigeni na taasisi za fedha za kimataifa, ndiyo ukauliza kuhusu masharti hayo. Hivyo sivyo ilivyo maanisha bali ilimaanisha kuwa kukopa kutoka nchi za kigeni na taasisi za fedha za kimataifa hakuruhusiwi kwa sababu mbili: ina riba na ina masharti. Na ikiwa kukopa kutachukua mwenendo huo basi hairuhusiwi. Na kitabu kimefafanua katika muendelezo wa paragrafu kama ifuatavyo: “Riba inayotozwa na benki imekatazwa na Shari’ah, ima iwe kutoka kwa mtu binafsi au nchi, kwa kuwa kuwekwa kwa masharti kunazipa nguvu nchi na taasisi zinazokopesha juu ya Waislamu na kuwafanya Waislamu kuwa wanyonge mbele ya nchi na taasisi zinazokopesha, jambo ambalo Shari’ah imelikataza.

Ama kuhusu sehemu ya pili ya suali kuhusiana na kukopa kutoka nchi ambazo tuko katika mkataba nao au vita, jibu lake ni kama ifuatavyo: Kulingana na taratibu za mikopo ya kimataifa za zama hizi, kukopesha hakusalamiki na ukiukaji wa Shari’ah, kwa maana nyingine “ina riba na masharti kinyume na Shari’ah”. Kwa sababu hiyo hairuhusiwi kukopa kutoka katika nchi za kigeni sawa tuwe katika vita au mkataba nao kwa mujibu wa mikataba ya sasa ya kimataifa.

Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye Hekima.

Link ya Kiengereza: http://hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/qestions/ideological-questions/6427.html

Chanzo: Hizb ut Tahrir Kenya

22 Shaaban 1439 Hijria

08 Mei 2018 Miladi