Mbebaji Da’awa: Kati Ya Ubunifu Na Utendaji:

بسم الله الرحمن الرحيم

وَقُلِ اعْمَلُواْ فَسَيَرَى اللّهُ عَمَلَكُمْ وَرَسُولُهُ وَالْمُؤْمِنُونَ

(Na sema: Tendeni vitendo. Na Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Waumini wataviona vitendo vyenu.)

 

Hakika kuhuisha kadhia ya kuifanyia kazi Dini hii ambayo hukumu zake zimeondolewa katika ardhi, ni miongoni mwa matendo makubwa,bora, na yanayopendekeza zaidi kwa Allah na Mtume wake. Kwani, kujinasibisha na hii dini ni Sharaf kubwa, inayokabiliwa na  majukumu makubwa, na amana kubwa katika kubeba ujumbe wake, na kuutekeleza kwa njia ya ukamilifu zaidi, na kuuweka kwenye daraja yake inayotakiwa, ambayo ni serikali ya Khilafah itakayohukumu kwa Sheria za Allah, na kujaza ardhi nuru na uadilifu, baada ya kua imejaa dhulma na unyanyasaji.

Hakika kulingania kwa Allah ni kazi ya manabii, na ni njia ya wakubwa, na pia ndio mikakati ya watengezaji (Muslihina) ambao hujishughlisha na kutengeza hali za viumbe, na kuwarudisha katika maumbile ya sawa yaliyochimbuka kutokana na itikadi ya (Rabbaniyah) Mungu, (Itikadi) ambayo imewadhaminia furaha, usalama, na amani, chini ya kivuli cha utabikishaji wa sharia za Ar-rahmaan (Mwingi wa huruma).

Na kufikia hapa, hasa katika mazingira ya serikali kandamizi za kiraslimali ambazo zimetukalia kimabavu, imekua hakuna budi ila kulingania kurudisha hukmu ya Allah katika ardhi, na kuondoa hukmu ya kitwaghuti na dhulma zao, Pia imekua hakuna budi kwa kila Muislamu mwanamume na Mwanamke -bila kubagua- wajifunge na ulinganizi huu, kwa kuzingatia kwamba ni Faradhi, na Faradhi kubwa ilioje! Bali ndio taji la faradhi zote.

Mbebaji daawa yampasa yeye kufanya kazi akiwa katika safu za kundi linalolenga kuujenga ummah na kusimamisha serikali itakayokua ya kwanza duniani, Serikali itakayomridhisha Allah na Mtume wake, itakayotekeleza sheria za Allah na Sunnah za Mtume wake, na kuurudisha ummah kama ulivyokua, ummah bora ulioletwa kwa ajili ya watu. Na jambo hilo sio upuzi wala pumbao, Bali ni ukweli na majukumu makubwa, yasio na budi ila kujipinda, Na kuyatekeleza kwa naamna bora zaidi.

Mbebaji daawa huamini fikra ambazo anaziendea mbio ili zipatikane maishani. Naye pia hufanya kazi kwa bidii ili azifikishe kwa watu ili nao wamuunge mkono katika malengo yake hayo. Kwahiyo, jukumu lake sio tu kuidhihirisha haki, bali pia kufanya kazi hiyo haki ionekane wazi katika uhalisia.

Kwahiyo, yamlazimu mbebaji daawa kua mbunifu katika mbinu zake, na kupangilia vipaumbele vyake na kuviainisha kwa namna ambayo vitatumikia malengo yake na kufikia kufaulu kwa daawa yake. Na haya anayoyapa kipaumbele huenda yakatafautiana kwa kutafautiana nyanja za daawa. Hivyo basi, ni vizuri kua makini, na kubuni visaidia kazi na mbinu mbalimbali wakati wa kubeba daawa, hayo hua na athari kubwa katika kufaulu kwa daawa baada ya Tawfiq ya Allah Mtukufu. Na hayo hayaezekani ila kwa kuvifanyia utafiti wa kina na kamili, ili mbeba daawa awe na ujuzi na yakini ya uhakika wa anachokibeba. Na awe na utambuzi na uelewa pale anapotekeleza daawa yake. Ili awe na picha ya wazi, kuhusu lengo maalum analolenga, na atakua mwenye vigezo vya juu kabisa wakati anapofikisha kupitia mjadala na ulinganizi.

Mbebaji daawa huziamsha hisia za watu pale anapozihutubja akili zao, Na kuzungumza na fikra zao pale anapoziamsha hisia zao, ili aweze kuvuna hamasa zao za utendaji. Hivyo, yeye hutafuta Kufikia haki wakati wa kujadili kwa njia nzuri zaidi, na hujua ni vipi atazivunja hoja batili, na kuzibadili kwa hoja za kweli.

Na mbebaji daawa huzungumza na akili za watu kwa mbinu zinazo nasibiana na kiwango cha fikra za walio mbele yake, Hivyo basi yeye huchagua matamshi mepesi mbele ya watu wa kawaida ili kuwafikishia fikra na kuwahimiza na kuwaamsha kwa ajili ya kufanya kazi. Pia hunyanyua kiwango cha matamshi yake na mbinu za juu pale anapokua mbele Ya wasomi na wajanja, Ili wavutiwe na jinsi anavyojenga hoja, Hapo hua mbunifu katika ufikishaji wa fikra kwa ufanisi. Na atavuta hima zao na kuwasukuma kuelekea kwenye njia iliyo nyooka ambayo ndani yake hupatikana radhi zake Allah.

Na mbebaji daawa hufuatilia matukio ya kiulimwengu na ya kieneo na msururu wa habari. Wala hapuuzi habari yoyote au maalumati, huunganisha matukio kwa fikra ya kina na angavu, na hushikanisha hukmu na uhalisia kulingana na utafiti wake ulio kamili na kufuatilia kwake matukio. Hivyo, hubainisha njama chafu za wamagharibi, na mapambano yao duni ya kuukamata vizuri ummah na kuubakiisha katika hali ya udhaifu, udhalili, na unyonge!.

Na ni mara nyingi sana daawa za kikweli zinayolenga mageuzi ya kimsingi na ya kimfumo  kukutana na mashambulizi ya kuzichafua, na kutoangaziwa katika vyombo vya habari, Kutoka kwa serikali na wapambe wao. (kwa hali hiyo basi) hizo daawa zahitaji watakaojitokeza mbele na kusambaratisha (hayo mashambulizi). Kwa hiyo, hapana budi kwa wabebaji daawa kujitokeza kama viongozi wenye ushawishi (mkubwa) kwa watu katika maeneo yao, Ili waongoze kazi za kisiasa kwenye uwanja wa mapambano. Isipokuwa kujitokeza huku yatakiwa kuwe ni kimaumbile tu, bila ya kujifanyisha. Vigezo vyao na uwezo wao ndio viwaeke mbele kimaumbile. La si hivyo, watakua mzigo kwa daawa. Hivyo basi, hili jambo (la daawa) ni lazima lifanywe na mwenye kufaa kiukamilifu, wala sio kufanywa tu yeyote.

Na kuwajenga wenye sifa hizo, ima iwe ni kwa njia ya kuwalenga wale ambao wanaonekana kua na ujanja, usiriasi, wanaoweza kufuatilia (mambo), na kuathiri katika maeneo yao. Au ima iwe ni  kwa njia ya kulenga kuwavuna wenye utambulisho maalumu na wenye ushawishi katika jamii, kwa ajili ya maslahi ya daawa. Kwa namna ambayo watakubali hii daawa na kuinusuru au kuikumbatia na kuwa sehemu ya daawa, (na hatimae) wafaulu kuifikisha kwa watu.

Na tuna kiigizo chema kwa Mtume s.a.w kwani Mjumbe wa Allah alikua akimuomba Allah aunusuru uislamu kwa mmoja kati ya Umar wawili. Kama ambavyo pia, kumchagua kwake Jaafar Ibn Abi Twalib kua kiongozi na msemaji wa msafara wa kwenda habasha, kulikua ndio sababu ya kufaulu kwa majukumu yake baada ya Tawfiq ya Allah. Vile vile, uzuri wa Mtume s.a.w kumchagua Mus-ab Ibn Umair kua balozi wa Madina.

Kwahiyo, Mtume s.a.w  katika kuwachagua wenye sifa za kiuongozi, walio wepesi wa kufkiria, na wenye mbinu za hali ya juu katika kuongea na kuamiliana na watu, pia wenye ufahamu na uelewa wa kina na mpana katika kufahamu hukmu za Allah kwenye Quran na Sunnah za Mtume wake… (kuwachagua wenye sifa hizi) ndio ilikua sababu muhimu ya kufanikiwa kwake katika majukumu yake ya ulinganizi na kuenea kwa Uislamu.

Kama ambavyo, pia hapana budi kwa mbebaji daawa kutathmini matendo yake kila wakati. (akijiuliza) Je, kile kitendo kilikua mnasaba ili kufikia lengo? Na kweli lengo lilifikiwa kwa hicho kitendo? Je, muda, juhudi, na raslimali zilizotengwa zilitosha kufanikisha kitendo? Je, kulikua na mikakati, mpangilio, na ufuatiliaji wa Amali kwa hali nzuri?. Kwa sababu, kutumia nguvu zote, na mbinu mbalimbali zenye matunda, pamoja na kumsafia niya Allah katika kila kipengee cha kitendo, hii ndio njia ya ufanisi kwa idhni ya Allah. Hivyo basi, hapana budi kutambua kwamba, kupuuza au kuzembea katika jambo lolote kati ya hayo, au kua na niya tofauti bila kumsafia Allah, au kuingiwa na majivuno na kujiskia moyoni, au mfano wa hayo, yote hupelekea kutoa suluhu dhaifu, pia husababisha kuyumbayumba katika safari, na kutoweza kuuelekeza ummah na kushindwa kuchukua uongozi kutoka kwao kwa njia sahihi.

Na pia mbebaji daawa hawi laini, wala hajipendekezi kwa hisabu ya  dini yake, hata kama ni kitu kidogo katika vipengee vya aqidah yake. Kwa sababu, mbebaji daawa yuko tayari wakati wowote kuwa katika msimamo wa bwana wa mashahidi, akiwa wazi katika kuchalenji. Hivyo basi, huifikisha fikra waziwazi peupe, bila ya kumuogopa mtawala au kifungo, au kupoteza kazi au cheo.

Mbebaji daawa hujua kwamba, lengo lake ni la juu zaidi kuliko majukumu binafsi yote ya kimaisha. Kwa hiyo, lengo lake sio tu kudhihrisha haq, bali zaidi ni kufanya kazi ili haq ipatikane katika uhalisia.

Hivyo basi, kuamrisha mema na kukataza maovu ni mtindo wake. Na kulingania uislamu ili uwe hai maishani ndio lengo lake kuu. Na kurudisha upya maisha ya kiislamu ndio hamu yake yote, huungulika kwa hamu ya kuona uislamu ukirudi kuhukumu kwenye ardhi, uislamu ambao ndani yake ndio kuna ushindi,ulinzi, usalama, uadilifu, na amani, na kuvunja nguvu za ukafiri na dhulma.

Nataraji huenda haya maneno yakawasha moto wa kuungulika kwa ajili ya uislamu katika nyoyo zetu. Na nataraji kinga cha moto cha kuhisi majukumu ya kuwajali waislamu kitawaka katika viungo vyetu. Pia uvivu, usingizi, na kuitegemea dunia yote yatayeyuka katika maisha yetu, Ili tuamke kwa ajili ya dini na kuufanyia kazi uislamu na kuunusuru, na tusimamishe Khilafah. natarajia tutapatiliza siku za huu mwezi mtukufu uliobarikiwa, kwa kujikaribisha kwa Allah kupitia kitendo kikubwa cha ibada bora, aipendayo zaidi kwake, nacho ni kitendo cha kubeba daawa yake na kuinusuru dini yake!.

قُلْ هَذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّهِ عَلَى بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِين

“Sema: Hii ndio njia yangu ninailingania kwa Mwenyezi Mungu kwa kujua, mimi na wanaonifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! wala mimi si katika washirikina”.

 

Manal Hussein-Ardhi tukufu ya Palestina

Imeandikwa kwa ajili ya Idhaa ya Afisi kuu ya Habari  ya Hizb-Ut-Tahrir