Njia ya Mtume (saw) Kuleta Mageuzi

سم الله الرحمن الرحيم

Halaqa 12: Mapambano ya Kisiasa Katika Da’wah ya Mtume (saw)

Katika halaqah hii tunaendelea na hatua ya tatu katika njia ya Mtume (saw) kuleta mageuzi. Leo tutazungumzia kuhusu mapambani ya kisiasa katika da’wah ya Mtume (saw).

Mapambano ya kisiasa ni kuwabishia milango mabwenyenye na viongozi. Na walio katika wanasiasa na wanaotawala watu, nayo ni kupambana nao kwa fikra pekee bila kutumia mabavu, wala mgongano wa kuendelea wa Kisilaha.

Mapambano ya kisiasa yanakuwa kwa kufichua mipango ya watawala, na kufichua njama zao na khiyana zao. Kwani walijaribu maswahaba wa Mtume (saw) wakiongozwa na Umar ibnul Khatwwab (ra) kabla kusimama kwa dola walitaka kupambana na mabwenyenye na viongozi kwa mgongano wa kudumu wa kisilaha, Na walikuwa wana kiu ya kuwapiga vita, walikuja kwa Rasulullah (saw) na wakamwambia: “Ewe mjumbe wa Allah! Je, hatuko katika haki?” Akasema Rasulullah (saw): “Kwa nini? Ndio tuko katika haki” Na wakamwambia: “Je, wao hawako katika batil?” Rasulullah (saw) akasema: “Kwa nini? Wao wako katika batil” Wakasema: “Ewe mjumbe wa Allah kwa nini tuidunishe dini yetu…? Ewe Mtume wa Allah! Tupe amri kesho tuwashambulie hawa jamaa kwa panga zetu…!” Mtume (saw) akawaambia: “Hapana bado hatujaamrishwa hivyo”. Kwa mfano wa jambo kama hili lahitaji ruhusa kutoka kwa mtungaji sheria Allah, Taa’la.

Na hakika iliweza kupatikana baada ya kusimama dola ruhusa ya kupigana; Akasema Taa’la:

أُذِنَ لِلَّذينَ يُقاتَلونَ بِأَنَّهُم ظُلِموا ۚ وَإِنَّ اللَّهَ عَلىٰ نَصرِهِم لَقَديرٌ

Wameruhusiwa kupigana wale wanao pigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa – na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia

[Al-Hajj: 39]

Mapambano ya Kisiasa Yalivyokuja Katika Qur’an na Mtume (saw) Kuyafanya Kabla ya Kusimama Dola:

Ama kabla ya kusimama dola, alikuwa Rasulullah (saw) akiwasafihi waerevu wao majahili akiwasifu kuwa ni waongo, wapakaji mafuta. Na mara nyingi akiwatisha bila ya kupigana, na hakutaka kwa yoyote miongoni mwa maswahaba wake kuwapiga vita mushrikina pamoja na kuwa wanaudhia sana.

Mtume (saw) alipambana mapambano ya kisiasa kivitendo yeye mwenyewe, ikawa anawasomea:

وَدّوا لَو تُدهِنُ فَيُدهِنونَ

Wanatamani lau unge lainisha ili nao wakulainishie.

[Al-Qalam: 9]

Na akimsomea ami yake Abu Lahab:

تَبَّت يَدا أَبي لَهَبٍ وَتَبَّ

Imeangamia mikono ya Abu Lahab, na yeye pia ameangamia.

ما أَغنىٰ عَنهُ مالُهُ وَما كَسَبَ

Hayatamfaa mali yake, wala alivyo vichuma.

سَيَصلىٰ نارًا ذاتَ لَهَبٍ

Atauingia Moto wenye mwako.

[Al-Masad: 1-3]

Na akimsomea Walid bin Mughira aliyebeba bendera ya vita ya Maquresh:

ذَرني وَمَن خَلَقتُ وَحيدًا

Niache peke yangu na niliye muumba;

وَجَعَلتُ لَهُ مالًا مَمدودًا

Na nikamjaalia awe na mali mengi,

وَبَنينَ شُهودًا

Na wana wanao onekana,

وَمَهَّدتُ لَهُ تَمهيدًا

Na nikamtengezea mambo vizuri

ثُمَّ يَطمَعُ أَن أَزيدَ

Kisha anatumai nimzidishie!

كَلّا ۖ إِنَّهُ كانَ لِآياتِنا عَنيدًا

Hasha! Kwani hakika yeye alikuwa akizifanyia inadi Aya zetu!

سَأُرهِقُهُ صَعودًا

Nitamtesa kwa mateso yasio wezekana.

إِنَّهُ فَكَّرَ وَقَدَّرَ

Kwani hakika yeye alifikiri na akapima.

فَقُتِلَ كَيفَ قَدَّرَ

Basi ameangamia! Vipi alivyo pima!

ثُمَّ قُتِلَ كَيفَ قَدَّرَ

Tena ameangamia! Vipi alivyo pima!

[Al-Muddaththir: 11-20]

Na akimsomea (saw) kinara wa ukafiri, Abu Jahli:

كَلّا لَئِن لَم يَنتَهِ لَنَسفَعًا بِالنّاصِيَةِ

Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele!

ناصِيَةٍ كاذِبَةٍ خاطِئَةٍ

Shungi la uwongo, lenye makosa!

فَليَدعُ نادِيَهُ

Basi na awaite wenzake!

سَنَدعُ الزَّبانِيَةَ

Nasi tutawaita Mazabania!

[Al-Alaq: 15-18]

Na akimsomea Umayya Bin Khalaf :

وَضَرَبَ لَنا مَثَلًا وَنَسِيَ خَلقَهُ ۖ قالَ مَن يُحيِي العِظامَ وَهِيَ رَميمٌ

Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake, akasema: Ni nani huyo atakaye ihuisha mifupa nayo imekwisha mung’unyika?

قُل يُحييهَا الَّذي أَنشَأَها أَوَّلَ مَرَّةٍ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ خَلقٍ عَليمٌ

Sema: Ataihuisha huyo huyo aliye iumba hapo mara ya mwanzo. Na Yeye ni Mjuzi wa kila kuumba.

[Yasiin: 78-79]

Alikuja Umayya kwa Rasulullah (saw) amebeba mkononi mwake mifupa iliyo oza akawa anaitifua, na kuipulizia katika uso wa Mtume (saw) na kusema: “Ewe Muhammad, Je Mola wako ataifufua hii mifupa baada ya kuoza Na kuwa mchanga…?” Mtume (saw) akajibu: “Ndio, Allah atakufufua na akutie Jahannam”, ikawa hili ni jibu lenye kuathiri kutoka kwa Mtume (saw) akifuata amri ya Allah iliyokuja katika Kauli yake:

فَأَعرِض عَنهُم وَعِظهُم وَقُل لَهُم في أَنفُسِهِم قَولًا بَليغًا

Basi waachilie mbali, uwape mawaidha na uwaambie maneno ya kuathiri na kuingia katika nafsi zao.

[An-Nisaa: 63]

Na alikua akimsomea Walid bin Mughera’:

وَلا تُطِع كُلَّ حَلّافٍ مَهينٍ

Wala usimt’ii kila mwingi wa kuapa wa kudharauliwa,

هَمّازٍ مَشّاءٍ بِنَميمٍ

Mtapitapi, apitaye akifitini,

مَنّاعٍ لِلخَيرِ مُعتَدٍ أَثيمٍ

Mwenye kuzuia kheri, dhalimu, mwingi wa madhambi,

عُتُلٍّ بَعدَ ذٰلِكَ زَنيمٍ

Mkavu, na juu ya hayo, mshari, amejipachika tu.

[Al-Qalam: 10-13]

Na ZANIIM ni mtoto wa zina, wanasema mufassirun: ziliteremka aya hizi kwa Walid bin Mughera Kwani alikuwa anadai uqureshi na si miongoni mwao, zilipoteremka aya hizi Walid alimuendea mamake akamwambia: “Hakika Muhammad amenisifu kwa sifa tisa, zote ninazo nazitambua isipokua ya tisa, akimaanisha ZANIIM/mwanaharamu. Usipo niambia ukweli nitaipiga shingo yako kwa Upanga…!” Mamake akasema: “Hakika babako alikuwa hawezi kuwaundama wanawake, wewe ni mtoto wa yule mchunga mbuzi”, hakutambua kuwa yeye ni mtoto wa zinaa mpaka zilipoteremka Aya hizi…!

Asema ibnul Abbas: “na anaye kusudiwa kuwa babake ni Akhnas ibnu Shariq”.

Alikuwa Rasul (saw) anasimama kwa matendo ya kisiasa, Alikuwa akiwapa sifa watawala na wenye madaraka kwa sifa walizonazo chafu, anamsifu muongo kwa sifa ya uongo, na khaini kwa sifa za khiyana, na mnafiki kwa sifa ya unafiki, na akifichua mipango yao, na njia zao za upotoshaji.

Itaendelea katika UQAB Toleo 17…In Shaa Allah.