بسم الله الرحمن الرحيم
Halaqa 6: Propaganda ‘Uvumi’ Dhidi ya Mtume (saw) na Da’wah yake
Katika halaqa hii tutazungumzia mbinu ya pili ambayo wameitumia Maqureysh dhidi ya da’wah ya Mtume (s.a.w) nayo ni Propaganda ‘Uvumi’ dhidi ya Mtume (s.a.w) na da’wah ya Qur’an.
Walipoona Maqureysh kuwa Mtume (saw) hakuna kinachomzuia na da’wah yake walianza kumchezashere kumfanyia mizaha na kumkadhibisha,na hayo ni kwa madai yao kuwa ati ni mchawi, kuhani, mshairi, na kumzushia mengine mengi. Qur’an ilisajili propaganda/uvumi huo; kama ifuatavyo: Asema Allah (swt):
بَلْ قَالُوا أَضْغَاثُ أَحْلَامٍ بَلِ افْتَرَاهُ بَلْ هُوَ شَاعِرٌ فَلْيَأْتِنَا بِآيَةٍ كَمَا أُرْسِلَ الْأَوَّلُونَ
Lakini wao walisema: Hizo ni ndoto za ovyo ovyo, bali amezizua tu, bali huyo ni mtunga mashairi. Basi atuletee miujiza kama walivyo tumwa wale wa mwanzo
[Al-Anbya 21:5]
أمْ يَقُولُونَ شَاعِرٌ نَتَرَبَّصُ بِهِ رَيْبَ الْمَنُونِ
Au wanasema: Huyu ni mtunga mashairi, tunamtarajia kupatilizwa na dahari.
[At-Tur: 30]
وَقَالُوا يَا أَيُّهَا الَّذِي نُزِّلَ عَلَيْهِ الذِّكْرُ إِنَّكَ لَمَجْنُونٌ
Na walisema: Ewe uliyeteremshiwa Ukumbusho! Hakika wewe ni mwendawazimu
[Al-Hijr: 6]
Baada ya kusajiliwa propaganda ‘uvumi’ zao kisha zilijibiwa na Qur’an kama ifuatavyo; Asema Allah (swt)
فَلَا أُقْسِمُ بِمَا تُبْصِرُونَ
Basi naapa kwa mnavyo viona,
وَمَا لَا تُبْصِرُونََ
Na msivyo viona,
إنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ
Kwa hakika hii ni kauli iliyoletwa na Mjumbe mwenye hishima.
وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَاعِرٍ ۚ قَلِيلًا مَا تُؤْمِنُونَ
Wala si kauli ya mtunga mashairi. Ni machache sana mnayo yaamini.
وَلَا بِقَوْلِ كَاهِنٍ ۚ قَلِيلًا مَا تَذَكَّرُونَ
Wala si kauli ya kuhani. Ni machache mnayo yakumbuka.
تَنْزِيلٌ مِنْ رَبِّ الْعَالَمِينَ
Ni uteremsho utokao kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
وَلَوْ تَقَوَّلَ عَلَيْنَا بَعْضَ الْأَقَاوِيلِ
Na lau kama angelituzulia na baadhi ya maneno tu,
لَأَخَذْنَا مِنْهُ بِالْيَمِينِ
Bila ya shaka tungelimshika kwa mkono wa kulia,
ثُمَّ لَقَطَعْنَا مِنْهُ الْوَتِينَ
Kisha kwa hakika tungeli mkata mshipa mkubwa wa moyo!
فَمَا مِنْكُمْ مِنْ أَحَدٍ عَنْهُ حَاجِزِينَ
Na hapana yeyote katika nyinyi ambaye angeliweza kutuzuia.
وَإِنَّهُ لَتَذْكِرَةٌ لِلْمُتَّقِينَ
Kwa hakika huu ni ukumbusho kwa wachamungu.
وَإِنَّا لَنَعْلَمُ أَنَّ مِنْكُمْ مُكَذِّبِينَ
Na hakika Sisi bila ya shaka tunajua kwamba miongoni mwenu wapo wanao kadhibisha.
وَإِنَّهُ لَحَسْرَةٌ عَلَى الْكَافِرِينَ
Na hakika bila ya shaka itakuwa ni majuto kwa wanao kataa.
وَإِنَّهُ لَحَقُّ الْيَقِينِ
Na hakika hii bila ya shaka ni haki ya yakini.
فَسَبِّحْ بِاسْمِ رَبِّكَ الْعَظِيمِ
Basi litakase jina la mola wako Mlezi Mtukufu.
[Al-Haaqqa: 38-52]
Qur’an imeelezea kwa picha ya wazi kabisa kuhusu msimamo wa Waleed bin Mughira. Akijaribu kufikia maneno ya upambanuzi ambayo yanaonyesha msimamo wa wenye inadi kama yeye ambao walikuja kwake wakimtaka awape kauli kuhusu Qur’an kauli ambayo wataafikiana kwayo Maqureysh kuwakabili wageni wanaokuja hija watakapowauliza khabari za Mtume (s.a.w) na Qur’an ambayo inamteremkia:
Akasema Ta’ala:
كَلَّا ۖ إِنَّهُ كَانَ لِآيَاتِنَا عَنِيدًا
Hasha! Kwani hakika yeye alikuwa akizifanyia inadi Aya zetu!
سَأُرْهِقُهُ صَعُودًا
Nitamtesa kwa mateso yasio wezekana.
إِنَّهُ فَكَّرَ وَقَدَّرَ
Kwani hakika yeye alifikiri na akapima.
فَقُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ
Basi ameangamia! Vipi alivyo pima!
ثُمَّ قُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ
Tena ameangamia! Vipi alivyo pima!
ثُمَّ نَظَرَ
Kisha akatazama,
ثُمَّ عَبَسَ وَبَسَرَ
Kisha akakunja kipaji, na akanuna.
ثُمَّ أَدْبَرَ وَاسْتَكْبَرَ
Kisha akaipa kisogo haki, na akatakabari.
فَقَالَ إِنْ هَٰذَا إِلَّا سِحْرٌ يُؤْثَرُ
Na akasema: Haya si chochote ila ni uchawi ulio nukuliwa.
إِنْ هَٰذَا إِلَّا قَوْلُ الْبَشَرِ
Haya si chochote ila kauli ya binaadamu.
سَأُصْلِيهِ سَقَرَ
Nitakuja mtia kwenye Moto wa Saqar.
وَمَا أَدْرَاكَ مَا سَقَرُ
Na nini kitakujulisha ni nini huo Moto wa Saqar
لَا تُبْقِي وَلَا تَذَرُ
Haubakishi wala hausazi
لَوّاحَةٌ لِلْبَشَرِ
Unababua ngozi iwe nyeusi.
[Al-Muddaththir: 16 – 29]
Na mwisho baada ya taabu zote hizi, na bidii zote, na mashaka asema Waleed bin Mughira maneno yake ya mwisho kuhusu Qur’an. Na lau maneno haya yatatambulisha chochote basi yatakuwa yanatambulisha muujiza wa Qur’an na daraja yake ya juu. Akasema waleed:
“Wallahi nimesikia maneno kwa Muhammad si maneno ya mwanadamu, wala maneno ya jini, Wallahi maneno yake yana utamu, na yana mvuto, ni sawa na mti wenye matunda mingi juu yake na mizizi chini imekita. Na hakika yako juu wala hakuna kinachokuwa juu zaidi yake”.
Itaendelea katika UQAB Toleo 11…In Shaa Allah.