Kilicho Nyuma ya Kura ya Maoni Juu ya Kulitenga Eneo la Kurdistan

بسم الله الرحمن الرحيم

Jibu la Maswali
(Imetafsiriwa)

Swali:

Ni kwa nini Barzani anasisitiza kufanyika kwa kura ya maoni ya kuutenga mkoa wa Kurdistan, licha ya kuwa hakuna uidhinishwaji wa kimataifa au wa kieneo wa kura hii ya maoni? Kulingana na dhurufu zilizoko kwa sasa si kura hii ya maoni iko dhidi ya matakwa ya Wakurdi wenyewe? Je kura hii ya maoni inatarajiwa kufanyika? Ikiwa kura hii ya maoni itafanyika na wengi wakaipitisha, inawezekana kubuniwa kwa serikali ya Kikurdi katika eneo hili? Jazakum Allah Khairan.

Jibu:

Kuna msemo usemao ikiwa mtawala atachukua uamuzi kinyume na maslahi ya nchi yake, humaanisha kuwa mtawala huyo ni kibaraka, na kwamba uamuzi huo huwa umeshurutishwa na dola nyengine kwa ajili ya maslahi yake… maneno haya yanashabihiana kwa karibu na hali ya Wakurdi katika eneo la Kurdistan, ufafanuzi wake ni kama ifuatavyo:

1 – Mwanasiasa yeyote aliye makinika anaelewa ni vigumu kiasi gani kwa Wakurdi kuwa na dola yao. Ukweli ni kuwa, kampeni ya kubuni dola ya Wakurdi katika dhurufu za kimataifa zilizoko kwa sasa ni haribifu kwa mkoa wa Kurdistan, sio tu kisiasa na kimaadili, bali pia uharibifu wa kimada. Kwani kadhia iliyoko sio juu ya kubuniwa kwa dola ya Wakurdi nchini Iraq, na kama hiyo ndiyo ingekuwa kadhia, basi ingewezekana…

Serikali iliyoundwa na Waamerika baada ya uvamizi wa Iraq, iliyokuja kutambulika kama katiba ya Bremer, serikali hii imeifanya Iraq kuwa mkusanyiko wa majimbo ya mkoa yaliyo na mahusiano tete na serikali kuu, mpaka ikaifanya idara ya jimbo la Kurdistan kuwa na nguvu zaidi kushinda serikali kuu jijini Baghdad katika upande wa utawala na usimamizi wa eneo hilo! Dhamira ya dola za kikafiri za kikoloni akilini mwao ni kupanda mbegu za kugawanya na kuvunja vunja biladi yoyote ya Waislamu wanayo ivamia, lakini husubiri tu kutokea kwa fursa muwafaka, yote haya yakitokana na chuki yao dhidi ya Uislamu na Waislamu… tumeeleza katika jibu la swali lilio tangulia la tarehe 12/8/2017:

 “-Amerika tangu uvamizi wake wa Iraq mnamo 2003 inaendelea kufanya kazi kuivunja vunja Iraq; katiba ambayo Bremer ameiweka kwa msingi wa ki-madhehebu imeweka eneo kwa kila dhehebu… Aligawanya kwa ushirikiano, na raisi, na kiongozi wa bunge, na waziri mkuu, na kwa kuwa waziri mkuu ndiye aliye na mamlaka ya utekelezaji, na kwa kuwa Bremer ameiunda kwa msimamo wa ki-madhehebu iligeuka kuwa nukta ya utesi na uchochezi kwa wadau wengine… kielelezo cha katiba yenyewe kinaieleza serikali kuwa ya majimbo juu ya maeneo, na kwamba mamlaka ya majimbo hayo ndiyo yenye nguvu. Kwa hivyo, Amerika imefaulu kuunda dhurufu za kuivunja vunja Iraq kimaeneo…” Mwisho. 

Mkoa huu kivitendo ni dola lakini isiyokuwa na afisi za ubalozi wala uanachama katika Umoja wa Mataifa na taasisi nyengine mfano wake… Ama kwa hali halisi, eneo la Kurdistan ni dola ndani ya dola iliyotenganishwa barabara na serikali kuu, kutokana na kuwekwa mbali Iraq kuwa kama dola moja! Hivyo basi, eneo la Kurdistan halihitaji dola ndani ya Iraq kwa kuwa kivitendo tayari ni dola… Na kama tulivyosema, kadhia sio kubuniwa kwa dola ya Kikurdi ndani ya mipaka ya eneo la Kikurdi nchini Iraq na wala haihusiani lolote na maeneo mengine ya Kikurdi nje ya Iraq, hii sio kadhia. Badala yake, ikiwa itaundwa dola yoyote ya Wakurdi, bila shaka nyuma yake itavutia harakati nzito za Wakurdi kati eneo hilo, ili dola hiyo ya Kikurdi isisimame katika eneo la Kurdistan… Hivyo basi, hili likitokea litakuwa ni pigo uchungu, hususan kwa Amerika na vibaraka wake nchini Uturuki, Iran na Syria. Kwa hivyo, mwanasiasa yeyote anajua kwamba kuundwa kwa dola ya Wakurdi, ima nchini Uturuki, Iraq au Syria, kwa sasa hakutavumiliwa kutokana na masharti ya kimataifa au ya kieneo, na kamwe hakumaanishi kuwa wanasiasa wa Kikurdi, wakiwemo Al-Barzani, hawatambui hili. Bali, kama ilivyo tangulia kutajwa, wazo la kuunda dola ya Kikurdi katika dhurufu zilizoko sasa huenda ikapelekea kutokea kwa mabadiliko ya mipango na harakati zisizo dhibitika katika eneo hilo, hususan eneo la Wakurdi. Ambalo, kama tulivyo sema, itawaathiri sio tu kimaadili na kisiasa bali pia kimada, na hivyo basi uamuzi wa Barzani uko dhidi ya maslahi ya nchi yake katika dhurufu zilizoko kwa sasa… Hii ndio sehemu ya kwanza ya maneno.

2- Kuhusiana na ni dola ipi iliyoko nyuma ya uamuzi wa Barzani, kwamba uamuzi huu ni kwa ajili ya maslahi ya dola hiyo, dalili ziko wazi katika hili, na si vigumu kulekeza kidole kutambua ni dola ipi hii. Tangazo la kura ya maamuzi kuunda dola kando kutoka Iraq, haliwezi kutolewa na Barzani huku kukiwa na upinzani dhidi ya Amerika na upinzani kutoka kwa dola za eneo zinazolizunguka eneo la Kurdistan ambalo ni tiifu kwa Amerika. Hawezi kupata nguvu ya kukabiliana na nguvu hizi pinzani, isipokuwa kuwe na dola nyengine kuu inayomsaidia Barzani na kumshajiisha kuchukua uamuzi huu. Kwani eneo lote la Kurdistan, ni dhaifu sana kusimama dhidi ya dola hizo, hususana Amerika, inayo idhibiti Iraq yote. Si vigumu, kama tulivyo tangulia kusema mwanzoni, kutambua kwamba dola hii kubwa inayo simama nyuma yake na kumpa maagizo kufanya maamuzi hayo ni Uingereza. Familia ya Barzani imenasibishwa na Uingereza tangu dola ya Kiuthmani. Barzani alirithi mahusiano haya kutoka kwa babake, Mustafa Mulla Barzani, na kabla yake ami yake Ahmed Barzani na kabla yao Abdul Salam Barzani, iliye ongoza uasi wa kisilaha dhidi ya dola ya Kiuthmani kuanzia mnamo 1909 mpaka 1914 akiwa na usaidizi wazi kutoka kwa Uingereza. Kwa hivyo, familia hii ina mahusiano ya muda mrefu na Uingereza… ikiwa tutafuata misimamo katika kura hii ya maamuzi, tutaona kuwa msimamo wa Uingereza ulikuwa ukipendelea uamuzi wa kura ya maamuzi, ingawa Uingereza inatambulika kwa mbinu yake ovu na uhadaifu:

Kwa mfano, Barzani alikutana na Frank Baker, Balozi wa Uingereza nchini Iraq mnamo 24/8/2017 kuelezea usaidizi wa Uingereza kwake. Tovuti ya kikurdi “Rudaw” iliripoti mnamo 24/8/2017, habari za mikutano hii, “Wakati wa mkutano wa Barzani na balozi wa Uingereza nchini Iraq, mgeni huyu (balozi) alielezea kuelewa kwa nchi yake juu ya haki za watu wa eneo la Kurdistan, na kumdokezea raisi wa eneo la Kurdistan kuhusu msimamo wa Uingereza wa kufanywa kwa kura ya maamuzi.” Maana ya kuelewa kwa lugha ya kidiplomasia ni kusaidia, na maana ya kumuelezea kuhusu msimamo wa Uingereza pasi na kutaja chochote pia ni kusaidia. Yaani, msimamo wa Uingereza una unga mkono uamuzi wa Barzani, bali unatoa usaidizi kwake na kumwambia aendelee nao licha ya upinzani wa Amerika na nchi zinazo egemea upande wa Amerika katika eneo hilo.

 

Mfano mwengine, afisa wa mahusiano ya kigeni katika eneo la Kurdistan Falah Mustafa alisema katika shirika la habari la Kurdistan 24 kuwa “Uingereza haiko dhidi ya kura ya maamuzi, na wala haipingi matarajio ya Wakurdi.” Hotuba ya Mustafa ilikuja baada ya mkutano wa Waziri wa Kigeni wa eneo la Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika, Alistair Burt pamoja na maafisa wa Kikurdi mjini Erbil. Waziri huyu wa Kigeni wa Uingereza wa eneo la Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika aliwasili mjini Erbil mnamo Jumapili kwa mazungumzo na maafisa wa Kikurdi juu ya kadhia kadha wa kadha. Mpango wa Wakurdi kufanya kura ya maamuzi juu ya kulitenga eneo la Kurdistan kutoka kwa Iraq mnamo 25 Septemba ni hatua ya kwanza ya kubuni serikali huru. (Kurdistan 24 Arbil, 5/9/2017).

Hivyo basi, Uingereza ndio nchi iliyo nyuma ya uamuzi wa kura ya maamuzi uliotolewa na Barzani.

3 – Ama kuhusu maslahi ya Uingereza katika uamuzi huu, ni yenye kuendelea tangu Trump kushinda katika uchaguzi na Waziri Mkuu wa Uingereza May kuharakisha kumzuru Trump mnamo 26/1/2017 na kumpomgeza jijini Washington… Wakati huo, Trump alimsifu May na vile vile May alimsifu Trump, lakini kila mmoja alikuwa na lengo tofauti na mwengine! Ama Trump, alitaka Uingereza kufanya bidii iwezavyo kuuvunja Muungano wa Ulaya, ili iweze kuvunja mahusiano yake na Ulaya kimasomaso. Wakati huo huo, kutoa juhudi kuunda mazingira muwafaka ya kuvunja Muungano wa Ulaya, hususan nchi ya Ufaransa na Uholanzi, ambazo zilikuwa ukingoni mwa kura hizo. Ama May, alitaka makubaliano ya kibiashara kutoka kwa Trump kupatiliza katika shinikizo mpya juu ya nchi za Muungano wa Ulaya ili ijishindie biashara wakati itakapo jiondoa katika Muungano huo. Wakati wa ziara hii, Trump na May waliangazia dhamira ya malengo yao. May, kama ilivyo ada ya Uingereza, alijaribu kuficha lengo lake la kibiashara kwa njia za kinafiki, lakini kwa ukosefu wa diplomasia wa Trump na matamshi yake ya wazi hayaku muwezesha May kuficha nia zake…

Hivyo basi, pindi nchi zinazounga mkono Muungano wa Ulaya ziliposhinda kura chini ya Uholanzi na Ufaransa, na kwa kuongezea kuwa Ujerumani inaunga mkono kwa dhati Muungano wa Ulaya na kuupatia umakinifu wa hali ya juu, ilimfanya Trump kutambua kuwa hamu ya Uingereza ilikuwa tu kukamilisha makubaliano ya kibishara na Amerika na wala haikulitia maanani suala la kuvunja Muungano wa Ulaya kama alivyo taka Trump na yote haya yalipelekea majibu makali kutoka kwa Trump, natija yake ikiwa ni kuchapwa kwa Uingereza nchini “Qatar” kupitia kuzingirwa kivikwazo na kutengwa! Tayari tumeshafafanua hili katika jibu la swali tulilotoa mnamo 23/7/2017, ambapo tulisema:

“Kuhusiana na Uingereza: ziara ya mwanzoni ya Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May jijini Washington mnamo Januari 26, 2017 na hamu yake ya kutaka kutia saini makubaliano ya kibiashara na Washington itakuwa kama kielelezo kwa nchi nyenginezo za Muungano wa Ulaya kuzishajiisha kuondoka katika Muungano wa Ulaya. Hivyo basi, Uingereza ilidumisha kushikana kwake na Amerika na iliipendelea zaidi idara ya Trump, lakini baada ya matarajio ya Amerika ya kuuvunja Muungano wa Ulaya kuchanika, kama ilivyo shuhudiwa katika ushindi wa upande unaounga mkono Muungano wa Ulaya katika kura nchini Uholanzi na Ufaransa, mtazamo mzuri wa Trump kwa Uingereza ulibadilika kwa kuwa aliitaka iongoze mchakato wa kuivunja Ulaya, na pindi hali ya kujiondoa kwa Uingereza ilipokosa kujirudia jijini Paris na Amsterdam, Amerika imerudi tena kuchafua maslahi ya kimataifa ya Uingereza katika namna iliyoishtua London. Amerika inamsukuma kibaraka wake, Sisi, kuongeza usaidizi wake kwa Hafter bila ya kuzingatia maslahi ya Uingereza nchini Libya, na Amerika ikawasukuma vibaraka wake katika njia ya mshtuko kiasi kuishinikiza Qatar, ambayo ni kibaraka wa Uingereza eneo la waarabu na Uislamu…”  Mwisho   

Yote haya yalimfanya Trump kuhamaki na kufanya ziara ya haraka nchini Saudi Arabia na kufanya kongamano lile na kisha kuigonga Uingereza kupitia kuizingira kivikwazo na kuikata Qatar.

3 – Hapa, ilikuwa ni muhimu kwa Uingereza kukatiza baadhi ya maslahi ya Amerika katika eneo hili, kwa hivyo iliamua kutumia uamuzi wa Barzani kuitisha kura ya maamuzi kuiudhi Amerika na vibaraka wake. Na bila shaka, Uingereza inaweza tu kuikatizia Amerika, kwani haina uwezo wa kukabiliana na Amerika paruwanja, lakini inaweza kuikatizia na kuiudhi, hususan ikiwa itachagua hali muwafaka na kazi barabara kama ilivyo pata ndani ya kura ya maamuzi ya Kurdistan. Uingereza ilikuwa makini kwa Barzani kufuata njia iliyo muekea kwa sababu hali iliyoko kwa sasa ni moto kwa Amerika pamoja na vibaraka wake; Uturuki, Iran na Syria kwa sababu ya harakati za kisilaha zinazoendelea… kwa hivyo Barzani alidumu kusisitiza juu ya kura ya maamuzi na Uingereza ikaifanyia propaganda kura hii ya maamuzi kuwa ndiyo itakayo faulu kupatikana kwa dola huru ya Wakurdi katika eneo la Kurdistan. Na kama ilivyo kawaida ya ujanja na unafiki wake, Uingereza haitilii maanani kupatikana au kutopatikana maslahi ya Wakurdi maadamu tu itafaulu kufikia maslahi yake binafsi, na historia ya Uingereza na Wakurdi imesheheni mambo haya!

Tulisema katika jibu la swali la tarehe 1/4/2009:

 “… Uingereza ilimuahidi Mahmood Al-Hafeed dola ya Kikurdi mnamo 1919 Miladi baada ya kupigana na majeshi ya dola ya Kiuthmani eneo la Sulaimaiyyah. Majeshi ya Al-Hafeed yakapigana, yakawaua ndugu zao wa Kiuthmani na kuwafurusha, lakini bila shaka Uingereza haiku khini tu ahadi yake, bali pia ilimfukuza Al-Hafeed na kumpeleka katika koloni yake ya India. Vile vile katika mkataba wa Sèvres mnamo 1920, Uingereza iliisisitiza dola ya Kiuthmani kujumuisha kifungu kinachohusu dola ya Kurdistan kwa lengo la kumtia dhiki Khalifa Muhammad Waheeduddin. Katika mkataba huu, ujumbe wa Khalifa ndio uliokuwa ukijadiliana. Uingereza ilipo faulu kuivunja Khilafah na kumuweka kibaraka wake Mustafa Kamal kama raisi wa Jamhuri ya Uturuki, na baada ya kutia saini mkataba wa Lausanne pamoja nayo mnamo 1924, Uingereza ilikataa kujumuisha kifungu cha dola ya Kikurdi na sababu yake nyepesi ikiwa: tayari ishafaulu kufikia lengo lake, ambalo bila shaka ni kuivunja dola ya Khilafah, kwa hivyo ahadi hii sasa imepitwa na wakati! Uingereza ndiyo iliyo chochea hamasa na miito ya kikabila ya Kikurdi pamoja na ‘matarajio’ yote mengine ya kikabila katika eneo zima (la ulimwengu wa Kiislamu), na ni Uingereza vile vile iliyo patiliza hamasa hizi na kuwashinikiza kupigana na kuasi dhidi ya dola ya Kiislamu ili Uingereza iweze kufikia malengo yake. Hatimaye ikazitumia hamasa zote hizi kwa kushirikiana nao na kuwatumia kama vibaraka wake na kuwaweka mamlakani kama watawala na viongozi katika biladi hizo…” Mwisho. Huu ndio ujanja na khiyana ya Uingereza…

5- Hivyo basi, Barzani amesisitiza kufanyika kwa kura ya maamuzi mnamo 25/9/2017, ili awe na dola! Kamwe hakutilia maanani upinzani wa kimataifa au wa kieneo uliopinga kura hiyo, hata kutoka kwa miongoni mwa Wakurdi wenyewe, badala yake akasema: (Eneo la Kurdistan limekariri tena mnamo Jumatano kupinga kwake kuakhirishwa au kufutiliwa mbali kwa kura hii ya maamuzi ya uhuru kutokana na Iraq iliyo pangwa kufanyika mnamo Septemba 25, licha ya juhudi za kimataifa na kieneo za kuisihi Erbil kuachana na hatua hii, na kukataa kwa serikali kuu jijini Baghdad kura hii na matokeo yake.

Baraza Kuu la kura hii ya maamuzi katika eneo la Kurdistan, wakati wa mkutano ulioongozwa na raisi Masoud Barzani, jana, lilijadili matokeo ya ziara ya ujumbe wa Kurdistan jijini Baghdad, kuhusiana na suala la kura ya maamuzi, pamoja na matokeo ya mazungumzo kati ya Barzani na Mattis mjini Erbil, juzi. Mshauri wa Barzani alisema: raisi Masoud Barzani amesema kuwa kura ya maamuzi kamwe haita akhirishwa na itafanyika mnamo Alhamisi 25 Septemba sawia na 2 Dhu al-Hijja 1438 Hijri – 24 Agosti 2017 Miladi – Dubai – al-arabiya.net). Hii ni pamoja na ufahamu wa upinzani wa kimataifa na kieneo kuwa wazi kabisa:

A – Amerika ilipinga kura hii ya maamuzi kuanzia siku ya kwanza Barzani alipotangaza kufanyika kwake, ambapo mnamo 7/6/2017 alitangaza kuwa kura ya maamuzi ya kuasisi dola huru ya Kikurdi itafanyika katika maeneo ya Wakurdi nchini Iraq mnamo 25 Septemba. Amerika ilijibu kupitia mjumbe wa raisi wa Amerika katika muungano wa kimataifa, Bert Mc Gurk: “Hatuoni haja ya kufanyika kwa kura ya maamuzi mnamo Septemba kwa sababu itazua hali ya wasiwasi. Kufanywa kura ya maamuzi kwa njia hiyo ya haraka, haswa katika maeneo yenye mizozano, kwa madhanio yetu, itazua wazi hali ya wasiwasi.” (AFP, 8/6/2017)

Hivi majuzi, Waziri wa Kigeni wa Amerika Rex Tillerson mnamo 11/8/2017 katika maongezi ya simu na raisi wa eneo la Kurdistan Masoud Barzani, alieleza “hamu ya Washington kuakhirisha kura ya maamuzi ya uhuru wa eneo hilo na kuunga kwake mkono kuendelea kwa mazungumzo na majadiliano baina ya eneo hilo na Baghdad.” Amerika ilituma waziri wake wa ulinzi James Mattis jijini Baghdad mnamo 22/8/2017 kukutana na Waziri Mkuu wa Iraq Abbadi na kisha kwenda Erbil na Ankara mnamo 23/8/2017 kuisukuma Uturuki, mkono wake imara katika eneo…

B – Serikali za eneo zilizotiifu kwa Amerika pia zimepinga… Msemaji wa Waziri Mkuu Saad          al-Hadithi alisema “Uamuzi wowote unaohusu mustakbali wa Iraq ni lazima uzingatie vipengee vya katiba kwa kuwa ni uamuzi wa Iraq, kikatiba Iraq imefafanuliwa kama taifa la kidemokrasia, la kimajimbo na lenye ubwana kamili… Wairaqi wote ni lazima wawe na kauli juu ya mustakbali wa nchi yao. Hakuna yeyote atakaye waamulia hatma yake bila ya wao kuhusishwa.”                        (Free American 9//6/2017).

Uturuki imetangaza upinzani wake kwa kura hii ya maamuzi ya kutangaza uhuru wa Kurdistan kuanzia siku ya kwanza, kwa hayo Waziri wa Kigeni wa Uturuki akatoa taarifa kuelezea uamuzi wa raisi wa mkoa (wa Kurdistan) kama “kosa baya mno na wenye kuhatarisha umoja na hadhi ya eneo la Iraq” (Free American 9/6/2017) … Erdogan alitangaza baada ya mkutano na Waziri wa Ulinzi wa Amerika Mattis na kusema: “Uamuzi huu wa kura ya maamuzi ni wa kimakosa”              (Al-Jazeera 24/8/2017)… Vile vile Iran ikatangaza, mnamo Jumamosi, 11 Juni 2017, muda mfupi baada ya tangazo la kura ya maamuzi, kuwa inapinga vikali kufanyika kwa kura hii ya maamuzi katika maeneo ya Wakurdi nchini Iraq Septemba ijayo. Ikisisitiza kuwa Tehran ina msimamo wazi juu ya umoja wa maeneo ya Iraq. Msemaji wa Waziri wa Kigeni wa Iran, Bahram Qasimi, alisema: “Maamuzi mapana ya upande mmoja ambayo ni sehemu ya vipimo halali vya kitaifa, yatapelekea matatizo zaidi na kudorora zaidi kwa hali ya usalama nchini Iraq.” (15/6/2017 http://afkarhura.com). Tovuti ya fikra huru ya http://afkarhura.com/?p=6839  ilichapisha mnamo 7 Septemba 2017, taarifa ya raisi wa baraza la shura la Iran, ambayo ilisema: “Raisi wa Baraza la Kiislamu la Shura katika masuala ya kimataifa, Hussein Amir Abdullahian, amethibitisha kuwa kura ya maoni katika eneo la Kurdistan nchini Iraq itasababisha kuzuka kwa mgogoro mpya.”

Zaidi ya hayo, Amerika ina wafuasi ndani ya Kurdistan, ikiwemo harakati ya Kikurdi ya Goran (chama cha mabadiliko) na chama cha umoja wa kitaifa cha Talabani. Harakati ya Goran imepinga tangazo la Barzani la kura ya maamuzi, haya yamesemwa na Hoshyar Abdullah mwanachama wa harakati hiyo katika bunge la Kurdistan: “Harakati ya mabadiliko bado inashikilia rai ile ile kwamba huu sio wakati muwafaka kwa kura ya maamuzi na ajenda hii ni ya kibinafsi na ya chama cha Masoud Barzani” akisisitiza kuwa “Chama cha Kidemokrasia cha Kurdistan (KDP) ni kibaraka na wala si mshika dau.” (Elaph, 5/8/2017)

Vile vile, raisi wa Jamhuri ya Iraq Fuad Masum, anayetoka katika Chama cha Kitaifa cha Kidemokrasia cha Talabani alipinga kura hii ya maamuzi, akisema: “Afisi ya raisi imekuja kuwasaidia Wakurdi, kura za Wakurdi kamwe hazilingani na tone la damu yao na kujitolea muhanga kwao na hivyo haitaruhusu ndoto ya “Masum” ya kuasisi dola yao na itakabiliana nayo siku ya kura ya maamuzi.” Chama cha Kidemokrasia cha Kurdistan (KDP) kilisema katika taarifa kufafanua taarifa ya Masum kuwa “taarifa hatari na ujumbe mbaya kwa nchi za kiulimwengu zuieni matokeo ya kura hii ya maamuzi na muidunishe.” (Kutoka katika chanzo kilichotangulia).

Licha ya upinzani huu wa kieneo na kimataifa, Barzani anasisitiza kufanyika kwa kura ya maamuzi na kutangaza kuwa hataichelewesha hata kwa dakika moja, kama tulivyo tangulia kutaja juu. Yote haya ni kwa sababu ya msukumo wa Uingereza katika suala hili la kura ya maamuzi kama tulivyo onyesha kwa kuirudia upya hali hii.

6 – Sasa baada ya kurudia upya matukio ya kura hii ya maamuzi inayo athiriwa na mambo kadha wa kadha… Sasa twaweza kujibu matarajio ya kura hii… Linalo tarajiwa zaidi katika hili, na kutoka katika yale tuliyo yaangazia ni kama ifuatavyo:

  1. Katika hali zote, haitarajiwi kuwa dola ya Kikurdi itabuniwa kwa sura halali kama dola, kwa sababu mradi wa Kiamerika wa Iraq ni kuifanya Iraq kuwa serikali ya kimajimbo ya mikoa yenye mahusiano tata baina ya majimbo na serikali kuu. Hili lamaanisha, kivitendo kuna kutenganishwa kati ya utawala na usimamizi wa Iraq, huku rasmi ikibaki kuwa serikali ya kimajimbo ya mikoa kwa jina Iraq… Huu ndio mradi wa Kiamerika kwa Iraq tangu uvamizi wake mnamo 2003, ambao imekuwa ikibeba mbegu za kuigawanya na kuivunja vunja Iraq, pasi na kuzitangaza rasmi kuwa dola huru, bali itafanya hivyo wakati muwafaka utakapowadia. Bremer, gavana wa Amerika nchini Iraq, hatimaye akaweka katiba ya kimajimbo ya mikoa ya Iraq, ikaiangamiza hadhi ya Iraq kuwa kama dola moja yenye nguvu na mamlaka moja makuu, na kuibadilisha kuwa dola hafifu ya kimajimbo, ambayo mamlaka ya mikoa yana nguvu zaidi kuliko mamlaka katika serikali kuu! Ili Iraq itayarishwe, katika wakati ambao Amerika itauona kuwa muwafaka kwa maslahi yake binafsi, na ili itayarishwe kufanywa rasmi kuwa vijidola kadhaa kutokana nayo… Ama kwa sasa, mradi huu wa Kiamerika ni kubaki kuwa serikali ya kimajimbo ya mikoa ya Iraq katika hali ya mahusiano tata na serikali kuu… Tumetoa katika jibu la swali lililotangulia la tarehe 12/8/2017 linalosema:

“-Amerika tangu uvamizi wake wa Iraq mnamo 2003 inaendelea kufanya kazi ya kusababisha kuvunjika vunjika kwake; katiba ambayo Bremer ameiweka katika msingi wa madhebevu imegawanya sehemu kimadhehebu… Amezigawanya baina ya Raisi, kiongozi wa bunge na Waziri Mkuu, na kwa sababu Waziri Mkuu ndiye mtu aliye na mamlaka ya utendaji, na kwa kuwa msimamo alio uweka Bremer ni wa kimadhehebu ili geuka kuwa chuki na uchochezi kwa wadau wengine… kielelezo cha katiba chenyewe chaeleza kuwa serikali ni ya majimbo juu ya maeneo, na nguvu za majimbo haya ziko imara. Hivyo basi, Amerika imefaulu kuunda dhurufu za kuivunja vunja Iraq kuwa majimbo matatu…” Mwisho

Hivyo basi, sera ya sasa ya Kiamerika haitaki kuwepo kwa dola ndani ya Iraq, bali inachotaka ni kuwepo kwa serikali dhaifu ya majimbo, iliyogawanyika katika upande wa utendakazi huku kimuundo ikibakia kama dola moja. Kwa haya, haitarajiwi katika dhurufu zilizoko kwa sasa kuigawanya Iraq rasmi, bali Iraq inabaki kuwa kwa mujibu wa Bremer mradi ambao kivitendo imegawanyika na mikoa yake ina nguvu kuliko serikali kuu! Angalau kwa mustakbali wa karibu.

B – Kwa kuwa tangazo la kura ya maamuzi ni agizo la Uingereza kukwepa tatizo la Uingereza kutokana na yale yaliyotokea kwa Qatar, basi, kura hii ya maamuzi itafutiliwa mbali ikiwa Amerika itasaidia katika kusitisha kutengwa kwa Qatar au hata kuipa afueni kwa njia muwafaka kuuokoa uso wake…

C – Amerika yaweza kufutilia mbali kura hii ya maamuzi ikitaka, kwa sababu ni nchi pekee inayo idhibiti Iraq. Ima ufutiliaji mbali huu wa kura ya maamuzi ufanywe moja kwa moja na Amerika, au kwa kuzisukuma harakati za Kikurdi zilizo tiifu kwake katika eneo la Kurdistan, au kwa kuisukuma Uturuki na Iran dhidi ya eneo hilo na, dhidi ya Barzani hata ikibidi utumiaji nguvu katika ushinikizaji. Mkuu wa jeshi la Iran, Mohammad Baqri, alizuru Uturuki kwa mara ya kwanza tangu kuasisiwa kwa Jamhuri ya Iran mnamo 1979. Ziara hii ilifanyika mnamo 15/8/2017, na ilichukua siku tatu. Alipokewa na Raisi wa Uturuki Erdogan katika makao ya Raisi jijini Ankara na mkutano ukachukua dakika 50, kama ilivyo ripotiwa na shirika rasmi la habari la Uturuki la Anatolia agency, ukionyesha umuhimu wa jambo hili. Mkuu wa jeshi la Iran aliandamana na mkuu wa kikosi cha wanajeshi wa nchi kavu na kamanda wa kikosi cha walinzi wa mipaka wakiwemo pia makamanda kadhaa wa kijeshi wa ngazi za juu wa Iran, shirika rasmi la habari la IRNA liliripoti. Msemaji wa wizara ya kigeni ya Iran Bahram Qasimi aliitaja ziara hii ya kiongozi wa jeshi la Iran Mohammad Baqri nchini Uturuki na mkutano wake na mwenzake wa Uturuki kuwa ni “muinuko” na “hatua muhimu katika uhusiano baina ya nchi mbili hizi…” (Mehr Iranian Agency 12/8/2017). Kwa hivyo, inatarajiwa sana kuwa ziara hii ilikuwa ni kupanga juu ya kazi yoyote ya kisilaha katika eneo hili, endapo itahitajika ili kufutilia mbali kura ya maamuzi au kuondoa matokeo yoyote yenye kuleta athari… kinachoipatia uzito rai hii ni kule kuzuru kwa Waziri wa Ulinzi wa Amerika Ankara mnamo 23/8/2017 baada ya ziara ya mkuu wa majeshi ya Iran…

D- Ikiwa Amerika itahofia kwamba kwaweza kutokea kwa vurugu kutokana na natija ya nukta (c), Amerika haitazuia kufanyika kwa kura ya maamuzi, lakini bila ya kuwa na matokeo ya maana na yenye athari. Na kwamba kura hii ya maamuzi haitahusisha uchukuaji hatua zozote kwa njia huru.

  1. Mwisho, kihakika inaumiza kuona kwamba fungamano la Kiislamu, lililo thaminiwa na Waislamu; Waarabu na Waajemi, makafiri wakoloni wamefaulu kuliweka mbali katika maisha ya Waislamu na kuwabadilishia mafungamano yaliyooza; ya uvunjifu yaliyo wafanya Waislamu kusambaratika: vita baina yao vikikithiri, udugu wao ukitoweka!

Ukabila ni mwiko wa maangamivu kwa Ummah, kama ulivyokuwa jana mwiko wa kuivunja dola ya Kiislamu. Na huyu hapa tena kafir mkoloni anaendelea kuutumia kama silaha kuangamiza kilicho bakia katika nguvu ya Umma ikiwa ataweza… Na kisha kuzigeuza biladi za Waislamu kuwa uwanja wa vita kwa dola kuu na njia ya umwagaji damu za Waislamu, ndugu akikata shingo ya ndugu yake! Uislamu umeharamisha yote haya, na umesisitiza umoja wa Waislamu, na udugu wao, Allah (swt) asema:

وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنتُمْ أَعْدَاءً فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُم بِنِعْمَتِهِ إِخْوَانًا وَكُنتُمْ عَلَىٰ شَفَا حُفْرَةٍ مِّنَ النَّارِ فَأَنقَذَكُم مِّنْهَا كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ﴿

“Na shikamaneni kwa Kamba ya Allah nyote pamoja, wala musifarikiane. Na kumbukeni neema ya Allah iliyo juu yenu: pindi mulipokuwa maadui nyinyi kwa nyinyi basi akaziunganisha nyoyo zenu; mukapambaukiwa hali ya kuwa ni ndugu. Na mulikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi ndivyo Allah anavyo kubainishieni Ishara zake ili mupate kuongoka”.

[Aali Imran: 103].

Na Allah (swt) asema:

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ﴿

“Hakika ya Waumini ni ndugu”

[Al-Hujurat: 10].

Pia, Uislamu umeharamisha kila aina ya Asabiyah: utaifa, uzalendo na ukabila… nk. Amr ibn Dinar amesema: Nimemsikia Jaber bin Abdullah akisema: tulikuwa pamoja na Mtume (saw) katika vita na mmoja miongoni mwa Muhajirin akampiga mmoja miongoni mwa Maansari. Muansari akapiga ukelele wa kikabila, “Enyi Maansari!” na Muhajir naye akaita, “Enyi Muhajirin!” Mtume wa Allah akayasikia haya akasema, «مَا هَذَا؟» “Ni nini hii?” Wakasema, “Ewe Mtume wa Allah, mmoja miongoni mwa Muhajirin amempiga mmoja miongoni mwa Maansari. Muansari akanadi, “Enyi Maansari!” Na Muhajir akanadi, “Enyi Muhajirin!” Mtume (saw) akasema:  «دَعُوهَا، فَإِنَّهَا مُنْتِنَةٌ». “Uacheni, hakika huo ni uvundo”. (Imepokewa na Bukhari).

Na Abi Mijlaz, amepokea kutoka kwa Jundab ibn Abdillah albajali aliyesema: Mtume wa Allah (saw) amesema: مَنْ قُتِلَ تَحْتَ رَايَةٍ عُمِّيَّةٍ، يَدْعُو عَصَبِيَّةً، أَوْ يَنْصُرُ عَصَبِيَّةً، فَقِتْلَةٌ جَاهِلِيَّةٌ» “Yeyote anaye uliwa chini ya bendera ya ukabila, akilingania ukabila, au akiutetea ukabila, basi kifo chake ni cha kijahiliya.” (Imepokewa na Muslim).

Waislamu waliishi kwa karne nyingi, wakipata izza kutoka kwa dini yao, wakiwa na nguvu kutoka kwa Mola wao, na kuunganishwa na udugu wao wa Kiislamu. Hivyo basi, miongoni mwa Maswahaba wa Mtume wa Allah (saw) kulikuweko na Abubakar, Omar, Uthman, Ali, Salman       al-Farsi (Mfursi) na Bilal al-Habashi (Muhabeshi)… Walikuwa waja wa Allah, ndugu, waliojitolea kwa ajili ya Allah… Kwa hivyo, Omar ambaye ni Muarabu aliingia Al-Qudsi (Jerusalem) kama mkombozi, Salahuddin Mkurdi aliikomboa Al-Qudsi kutoka kwa Makruseda, na Abdulhamid Mturuki aliihifadhi kutokana na uharibifu wa Mayahudi… Kwa hivyo, Waislamu wametukuzwa, na hivyo hivyo kwa kila mwenye moyo, au mwenye kusikia na kutafakari.

إِنَّ فِي هَٰذَا لَبَلَاغًا لِّقَوْمٍ عَابِدِينَ﴿

“Hakika katika hii [Qur’an] yapo mawaidha kwa watu wafanyao ibada”

[Al-Anbiya: 106]

18th Dhul Hijjah 1438 H

9/9/2017 M