Ramadhani Inaingia huku Umma ukiendelea kukumbwa na maafa zaidi

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

Harakati ya Hizb ut-Tahrir Kenya inafuraha kupongeza Waislamu humu nchini na kote duniani kwa ujumla kwa kufikiwa na Mwezi mtukufu wa Ramadhan. Tunapoingia kwenye mwezi huu wa rehema, msamaha na kuachwa huru na Moto, tungependa kuwakumbusha Waislamu waweze kuisoma Quran kwa wingi wakitafakari maana yake kwa lengo la kujifunga na mafundisho yake.

Ramadhani inaingia huku baadhi ya maeneo yakiwemo  mji mkuu wa Nairobi yapo kwenye marufuku ya kutembea usiku na kuingia au kutoka katika  kile kiitwacho kupambana na msambao wa Corona, hali inayohujumu uchumi wa wakenya wengi. Isitoshe, kwa hatua hiyo kaka na dada zetu wa Kiislamu wa maeneo hayo hawatoweza kutekeleza swala za Jamaa katika kipindi kizima cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Tunabaini kwamba hatua ya kuweka idadi maalumu ya waumini ni kinyume na Uislamu na Waislamu. Na hapa twapenda kusisitiza kuwa kwenye kipindi cha maradhi ya maambukizi, sheria tukufu ya Kiislamu inabaini kuwa kinachohitajika sio kufunga misikiti au kuweka idadi maalum waumini bali ni kuzuia walioambukizwa na kutengwa kutoingia Msikitini. Sambamba na haya lazima kuchukuliwe mikakati yote ya kiafya kama vile udumishaji wa usafi,uvaaji wa vitamvua, watu kupimwa na kuosha mikono.

Katika hali ya kusuasua kwa uchumi, Ramadhani inakuja huku hamu ya serikali ya ukopaji fedha kwa mataifa ya kigeni bado ingali kuwa juu. Nairobi tayari imekwisha saini mkataba na shirika la Fedha Duniani IMF kupokea kiwango cha fedha kwa muda wa miaka mitatu kama hatua ya ‘kuisaidia kupambana na janga la Corona’ na mpango wake wa kupunguza kiwango cha malimbikizi yake ya madeni!  Ukopeshaji wa IMF na masharti yake magumu kamwe hayotoweza kuimarisha uchumi bali ni kuhujumu zaidi uchumi wa mamilioni ya wakenya. Tokea mwanzoni mwa mwaka bei za bidhaa muhimu kama unga wa ngano, maziwa, mafuta ya kupikia, mafuta taa na sukari imeongezeka juu zaidi. Sera mbaya za kiuchumi ndani ya mfumo wa Kibepari, zinazosema kwamba bei ndio kiwango cha kuamua na kutambua kasi ya uzalishaji na matumizi wa bidhaa,hali inayowafanya warasilimali kumiliki uzalishaji na usambazaji wa bidhaa. Kwa hakika hali yapaswa kuwa ukumbusho mkubwa kwamba serikali za Kibepari hazijali kabisa hali za raia wake.

Kwa yakini Ramadhani huletea Waislamu kheri lakini cha kutamausha ni kwamba hali ya Umma wa Kiislamu leo inatisha. Waislamu huko Mynmar, Syria, Filastin na Yemen bado wanakumbana na dhulma na madhila ya kila siku. Maafa haya bila shaka ni kukosekanwa kwa utekelezwaji wa Quran kwenye nyanja zote za maisha. Umma wa Kiislamu wapaswa kuelewa kwamba majanga haya yatamalizika punde tu watakapotekeleza moja wapo wa wajibu mkubwa wa Kuisimamisha tena Khilafah kwa mfumo wa Utume katika moja wapo ya mataifa makubwa ya Kiislamu.

Kwa kuwa leo twaishi katika jamii ya Kisekular ya Kilibirali inayoitambua Dini kama suala la wakati na sehemu tu ya maisha,Waislamu tunalazimika kufahamu kwamba Uislamu ni mfumo kamili wa kimaisha tunapaswa kuutekeleza  kikamilifu katika masuala ya kisiasa,kiuchumi na kijamii.

Mwisho twamuomba Mwenyezi Mungu SWT atupe nguvu kufikia kwenye lengo husika la ibada ya swaum lililotajwa kwenye Quran nalo ni uchajiMungu, nishati ya hali ya juu ya Muislamu inayomfanya aweze kujifunga na maamrisho ya MwenyeziMungu.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari

 Hizb ut -Tahrir in Kenya