Tangazo la Matokea ya Kuutafuta Mwandamo wa Mwezi wa Baraka wa Ramadhan wa Mwaka wa 1439 H

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

(Imetafsiriwa)

Najilinda na Allah kutokana na Shetani aliye laaniwa,

 (شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِيَ أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ يُرِيدُ اللّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلاَ يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُواْ الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُواْ اللّهَ عَلَى مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ)

“Mwezi wa Ramadhan ambao imeteremshwa humo Qur’an kuwa ni uongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongofu na upambanuzi. Basi atakaye kuwa mjini katika mwezi huu naafunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu siku nyengine. Allah anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Allah kwa yale aliyowaongozeni kwayo ili mupate kushukuru.” [Al-Baqara: 185]

Sifa njema zote zamstahiki Allah na rehma na amani zimshukie Mtume wa Allah, jamaa zake, maswahaba zake, washirika wake, na wale wanaofuata njia yake kwa kuifanya itikadi ya Kiislamu kuwa ndio msingi wa fikra zao na hukmu za kisheria kuwa kipimo cha vitendo vyao na chimbuko la maamuzi yao.

Al-Bukhari amepokea katika Sahih yake kutoka kwa Muhammad Bin Ziyad kwamba amesema: Nilimsikia Abu Hurairah (ra) akisema, “Mtume, rehma na Amani zimshukie yeye na jamaa zake, amesema, au alisema, Abu Al Qasim (saw) amesema:

«صوموا لِرُؤيتِهِ وأَفْطِرُوا لرؤيتِهِ فإنْ غُـبِّيَ عليكم فأَكْمِلُوا عِدَّةَ شعبانَ ثلاثين»

“Fungeni kwa kuonekana mwezi na fungueni kwa kuonekana mwezi, na ikiwa kutakuwa na mawingu juu yenu (na kuwaziba kuuona mwezi), basi kamilisheni siku thalathini za Shaaban.”

Baada kuutafuta mwandamo wa mwezi mpya wa Ramadhan iliyo barikiwa usiku huu, usiku wa kuamkia Jumatano, mwezi haujathibitishwa kuonekana kwa mujibu wa matakwa ya shari’ah, hivyo basi kesho, Jumatano, ni kukamilisha mwezi wa Shaaban InshaAllah, na Alhamisi, kesho kutwa, itakuwa ndio siku ya kwanza ya mwezi wa baraka wa Ramadhan…

Enyi Waislamu Wapendwa:

Mwezi huu wa baraka unawashukia juu yenu hali ya kuwa munashuhudia mataifa ya kikafiri yakiungana (na kutoa wito) kwa kila mmoja wao kutushambulia, pamoja na watawala waovu miongoni mwa watu wenyewe, wanaokimbilia kuwasaidia katika njama zao dhidi ya Uislamu na watu wake. Hili latukumbusha Hadith Sahih: Mtume (saw) amesema:

«يُوشِكُ الْأُمَمُ أَنْ تَدَاعَى عَلَيْكُمْ كَمَا تَدَاعَى الْأَكَلَةُ إِلَى قَصْعَتِهَا» فَقَالَ قَائِلٌ: وَمِنْ قِلَّةٍ نَحْنُ يَوْمَئِذٍ؟ قَالَ: «بَلْ أَنْتُمْ يَوْمَئِذٍ كَثِيرٌ وَلَكِنَّكُمْ غُثَاءٌ كَغُثَاءِ السَّيْلِ وَلَيَنْزَعَنَّ اللَّهُ مِنْ صُدُورِ عَدُوِّكُمْ الْمَهَابَةَ مِنْكُمْ وَلَيَقْذِفَنَّ اللَّهُ فِي قُلُوبِكُمْ الْوَهْنَ» فَقَالَ قَائِلٌ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، وَمَا الْوَهْنُ؟ قَالَ: «حُبُّ الدُّنْيَا وَكَرَاهِيَةُ الْمَوْتِ»

“Watu wataalikana kukushambulieni kama wanavyoalikana walaji kuishambulia sahani ya chakula. Mmoja akauliza: Je, hiyo itatokana na uchache wetu siku hiyo? Akajibu: La, bali siku hiyo mutakuwa wengi: lakini mutakuwa kama taka mithili ya taka zinazo sombwa na mvua, na Allah ataondoa hofu yenu katika vifua vya maadui zenu na atazigonga nyoyo zenu kwa al-Wahn. Mmoja akauliza: Ni nini al-Wahn? Mtume wa Allah (saw) akajibu: Kupenda dunia na kuchukia kifo.”

Lakini tunajua kuwa Ramadhan ni mwezi wa subira; na subira ndio ufunguo wa afueni (kutokana na mateso). Tunakumbuka yale yaliyosimuliwa na al-Bukhari (rh): kutoka kwa Abu Abd Allah Khabbab ibn al-Arat (ra):

«شَكَوْنَا إِلَى رسولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَهُو مُتَوسِّدٌ بُردةً لَهُ في ظلِّ الْكَعْبةِ، فَقُلْنَا: أَلا تَسْتَنْصرُ لَنَا أَلا تَدْعُو لَنَا؟ فَقَالَ: قَد كَانَ مَنْ قَبْلكُمْ يؤْخَذُ الرَّجُلُ فيُحْفَرُ لَهُ في الأَرْضِ فيجْعلُ فِيهَا، ثمَّ يُؤْتِى بالْمِنْشارِ فَيُوضَعُ علَى رَأْسِهِ فيُجعلُ نصْفَيْن، ويُمْشطُ بِأَمْشاطِ الْحديدِ مَا دُونَ لَحْمِهِ وَعظْمِهِ، مَا يَصُدُّهُ ذلكَ عَنْ دِينِهِ، واللَّه ليتِمنَّ اللَّهُ هَذا الأَمْر حتَّى يسِير الرَّاكِبُ مِنْ صنْعاءَ إِلَى حَضْرمْوتَ لاَ يخافُ إِلاَّ اللهَ والذِّئْبَ عَلَى غنَمِهِ، ولكِنَّكُمْ تَسْتَعْجِلُونَ»

“Tulimlalamikia Mtume wa Allah (saw) huku amejipumzisha katika kivuli cha nguo ya Ka’aba, na kumuuliza: kwa nini usituombee nusra kwa Allah? Kwa nini usituombee kwa Allah? Yeye (saw) akajibu: Hakika miongoni mwa wale waliokuwa kabla yenu alikuwa akichukuliwa mtu (muumini) akichimbiwa shimo akitiwa ndani yake. Kisha ukiletwa msumeno na kuekwa juu ya kichwa chake na kukatwa vipande viwili. Na kuchanwa kwa kichana cha chuma na nyama yake kunyofolewa kutoka katika mifupa yake, lakini, yote hayo hayakumfanya yeye kuachana na dini yake. Wallahi! Dini hii (Uislamu) itakamilika (na kupata ushindi) mpaka aliye juu ya kipando (msafiri) atatoka Sanaa (mji mkuu wa Yemen) kwenda Hadhramout haogopi chochote isipokuwa Allah na mbwa mwitu kwa mbuzi wake, lakini nyinyi muna pupa”.

Hii ni ahadi ya Allah ya izza na ushindi kwa Dini yake hata kama ni baada ya muda, na tunachotakiwa pekee ni tuwe na ikhlasi kwa Allah na kuwa na subira na ukakamavu katika kumtii Yeye (swt), na kuwa na dhana nzuri na matarajio ya kupata ahadi hiyo ya Allah pasi na shaka wala tashwishi. Na Allah havunji ahadi yake, Yeye ni Mkweli na ahadi yake ni ya kweli.

Sisi katika Hizb ut Tahrir tunaulingania Ummah wa Kiislamu kuchukua msimamo mkubwa, unaomridhisha Mola wake, na kuusafisha na kuukomboa kutokana na dhambi hili kubwa na khiyana kuu, msimamo utakaoondoa fedheha mabegani mwake, na kuregesha utukufu katika ardhi zake zote…

Tunawasihi Waislamu kuunganisha mikono yao (iliyo twahirishwa kwa udhu) pamoja na mikono yetu katika Hizb ut Tahrir, iliyomo ndani ya mvutano wa kifikra na mvutano mkali wa kisiasa. Inayofichua njama za kijanja za Wamagharibi, na kuwaonesha mstari ulionyoka wa Uislamu. Huenda Allah akapitisha kuwa kwa mikono yenu na yetu ushindi na izza zitakuja; kwa kusimama dola ya Khilafah Rashida katika njia ya Utume. Allah ajaaliye ushindi huu katika mikono ya Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu Rashtah, na kwamba mumpe ahadi ya utiifu (Ba’yah) awe Khalifah na kutawala kwa Kitabu cha Allah na Sunnah za Mtume wake mwenye daraja (saw), na muishi ndani ya dola ya Khilafah inayotekeleza Shariah ya Allah, na mubebe ulinganizi wa Uislamu, mwenge wa uongofu kwa wanadamu wote…

Enyi maafisa wa majeshi ya Waislamu, jueni kuwa Allah ataipa ushindi Dini yake, ikiwa si kwa kupitia mikono yenu basi itakuwa kwa kupitia mikono ya wanaume wengine wenye ikhlasi ambao Yeye (swt) atawakirimu kwa izza, kwa hivyo musiikose hadhi hii kubwa na kusimama na Ummah ili kupata radhi za Allah kwa utukufu wa hapa duniani na kesho akhera.

Pia ni furaha yangu kuwafikishia salamu zangu na zile za Mkuu wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na wote wale wanaofanya kazi ndani yake kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni maarufu Ata Bin Khalil Abu Rashtah, na kwa Waislamu wote kwa ajili ya mwezi huu wa baraka, nikimuomba Allah atuokoe na Moto wa Jahannam ndani ya mwezi wa rehma na toba, na tunamuomba Allah (swt) aturuhusu kuushuhudia Usiku wa Cheo (Laylatul Qadr) na kutubariki kwa malipo yake…

Ewe Allah, Mola wa Mbingu na Ardhi, tukirimu kwa kumpa Ba’yah Khalifah wa Waislamu katika Khilafah Rashida ya pili katika njia ya Utume, sasa au sasa hivi… Allahumma ameen ameen ameen.

Wassalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh

Kuamkia Jumatano ni tarehe 30Sha’ban mwaka wa 1439 H.

Dkt. Osman Bakhach
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

H.  29 Sha’aban 1439 Na: 1439 H /023
M.  Jumanne, 15 Mei 2018