Tangazo la Mwandamo wa Mwezi wa Shawwal wa Mwaka 1439 H na Tahnia za Sikukuu Yenye Baraka ya Idd ul-Fitr

Allah Akbar, Allah Akbar, Allah Akbar, La Ilaha Ila Allah, Allah Akbar, Allah Akbar, Wa lilah Alhamd

(Imetafsiriwa)

Sifa njema zote ni za Allah na rehma na amani zimshukie Mtume wa Allah na jamaa zake na maswahaba zake na kila anayefuata njia yake, na kuifanya itikadi ya Kiislamu kuwa ndio msingi wa imani yake, na hukmu za Kiislamu kuwa ndio kipimo cha amali zake na chimbuko la hukmu zake…

Amepokea Ahmad kutoka kwa Muhammad Bin Ziyad, aliyesema: Nilimsikia Abu Huraira akisema, “Mtume (saw) amesema – au akisema Abul Qasim amesema:

«صُومُوا لِرُؤْيَتِهِ، وَأَفْطِرُوا لِرُؤْيَتِهِ، فَإِنْ غُبِيَ عَلَيْكُمْ فَعُدُّوا ثَلَاثِينَ»

“Fungeni kwa kuonekana kwake [mwandamo wa mwezi wa Ramadhani], na fungueni kwa kuonekana kwake [mwandamo wa mwezi wa Shawwal], na kukitanda mawingu juu yenu (kiasi cha kutouona mwezi), basi kamilisheni siku thalathini.”

Baada ya kuutafuta mwandamo wa mwezi wa Shawwal katika usiku huu wa kuamkia Ijumaa, kuonekana kwa mwezi kumethibitishwa kwa mujibu wa matakwa ya kisheria katika baadhi ya nchi za Waislamu, hivyo basi kesho, Ijumaa ndio siku ya kwanza ya mwezi wa Shawwal na ndio siku ya kwanza ya Idd ul-Fitr yenye Baraka.

Katika Sikukuu hii ya Idd ul-Fitr yenye baraka, Amiri wa Hizb ut-Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu Rashtah, Allah amuhifadhi, anawapa tahnia watu wote katika Ummah mtukufu wa Kiislamu, na kumuomba Allah Subhanahu kuturuzuku fadhla yake ya kusimamisha dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume itakayotekeleza sharia za Allah duniani na kubeba ujumbe wa uongofu na nuru, dola adilifu itakayokomboa ardhi na kuleta uadilifu kwa watu; dola ya Jihad itakayoendeleza ufunguzi wa miji, na watu watapiga takbira katika Idd zao, na futuhaat: Allah Akbar, Allah Akbar, la ilaha ila Allah, Allah Akbar, Allah Akbar, Wa lilah Alhamd.

Pia ni furaha yangu kutoa tahnia zangu na zile za Mkuu wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir na wale wote wanaofanya kazi ndani yake kwa Amiri wa Hizb ut-Tahrir, na kwa Waislamu wote kwa ajili ya Idd hii yenye Baraka; sikukuu hii Allah ameileta ili iwe ni furaha kwa wenye kufunga na alama ya umoja wa Waislamu, na ukumbusho kwao kuwa wao ni Ummah mmoja tofauti na watu wengine wote.

Enyi Waislamu mulioko kila mahali:

Namuomba Allah (swt) kukubali kutoka kwenu na kwetu saumu, kisimamo, rukuu na sujud zetu na amali zote njema. Kama ninavyo muomba Yeye (swt) kuijaalia irudi tena kwa Ummah wa Kiislamu katika hali ya uwepo wa Khalifah mwema na muadilifu, ambaye watu huhifadhika na kupigana nyuma yake, na anayetawala kwa Kitabu cha Allah na Sunnah za Mtume wake (saw), na hilo ni jepesi kwa Allah.

Idd ul-Fitr ni fadhla kutoka kwa Allah Azza Wa Jal juu ya Waislamu, na siku itakayokuwa Idd ya Idd zote pale ahadi ya Allah (swt) na bishara njema za Mtume wa Allah (saw) zitakapotimia kwa ushindi na mamlaka, na kuunda dola inayotawala kwa sharia za Allah, dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Ili furaha hii ikamilike, ni lazima tuzing’oe serikali za kibinadamu, vibaraka wa makafiri na wakoloni makhaini wa Allah, Mtume Wake na waumini Wake.

Ili furaha hii ikamilike, ni lazima tuunganishe nguvu zote za Umma wa Kiislamu.

Ili furaha hii ikamilike, majeshi ni lazima yatoe Nusra kwa wale wanaofanya kazi kwa ikhlasi kuleta ushindi wa Uislamu.

Ili furaha hii ikamilike, ni sharti maisha kamili ya Kiislamu yarudi katika nyanja zote za maisha kisiasa, kiuchumi, kijamii na kielimu.

Ili furaha hii ikamilike, muundo adhimu wa Kiislamu ni lazima ujengwe, ule wa Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.

Nawaalikeni kufanya kazi ya kunali Idd ya Idd zote, jaaliyeni kushikamana kwenu na sharia za Allah (swt) kuwe ndio tamati ya Idd yenu, kwa kufanya kazi na wanaofanya kazi kwa ikhlasi kuleta ushindi na mamlaka kwa Dini hii na kupiga takbira kwa pamoja siku ya ushindi huo, takbira za ushindi, utiifu, kumsifu Allah na kumuomba msamaha wake.

Allah Akbar, Allah Akbar, Allah Akbar, La Ilaha Ila Allah, Allah Akbar, Allah Akbar, Wa lilah Alhamd

Allah Akbar Kabira, Walhamdulilah Katheera, Wa Subhan Allah Bukratan Wa Aseela

La ilaha ila Allah, Wahduhu, Sadaq Wa’du, Wa Nasr Abdu, Wa A’azza Junduh, Wa Hazzam AL Ahzab Wahdu

La Ilaha Ila Allah… Wa la Na’bud Ila Iyah…Mukhliseen Lahu Ad-Deen Wa Lau Kariha Al-Kafiroon

Idd Mubarak na Allah awakubali nyinyi na sisi amali njema.

Wassalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuhu

Usiku wa kuamkia Ijumaa ndio siku ya kwanza katika mwezi wa Shawwal, 1439 H ikiafikiana na 15/6/2018 M.

Dkt. Osman Bakhach

Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

H.  29 Ramadan 1439 Na: 1439 AH / 027
M.  Alhamisi, 14 Juni 2018