“Umma Uko Tayari kwa Khilafah”

بسم الله الرحمن الرحيم

Hotuba ya Dkt. Osman Bakhash Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Kwa Ajili ya Kongamano la Khilafah Nchini Malaysia Mnamo 21 Rabii’ I 1439 H – 9 Disemba 2017 M

Ni wazi kwa kila muangalizi asiye na mapendeleo kuwa mvutano pekee wa kimfumo unao endelea kwa sasa katika ngazi ya kiulimwengu ni baina ya Uislamu na Urasilimali na itikadi yake ya kisekula. Mgongano baina ya Urasilimali na dola ya Ujamaa wa Kimarxi uliokuwa muungano wa Umoja wa Nchi Huru za Kisovieti (USSR) ulikuwa ni usanii na purukushani tu, kwani Ujamaa ulikuwa ni mshawasha wa haraka kwa urasilimali uliounyima muda wa kutafakari mambo kwa umakinifu, lakini pia sawia na hili ni thibitisho la kufilisika kwa akili ya mwanadamu kwa kujaribu kuchukua jukumu la Muumba katika kusimamia mambo ya waja; mikasa, maafa, majanga ya karne ya 20 ni shutma za wazi kwa akili ya kisekula katika upande wa urasilimali pamoja na upande wa ukomunisti.

Ni dhahiri kuwa mgongano huu wa hadhara hauna usawa: kwa upande mmoja majeshi ya kimagharibi yana nguvu za kijeshi za kisawa sawa, uchumi imara, na nidhamu ya kirasilimali yenye kuhisika inayotabikishwa katika mambo ya kimaisha ya kila siku katika viwango vyote, na kujihami na mtandao mkuu wa vyombo vya habari vyenye kufikia eneo kubwa na kila aina ya ushawishi katika sekta ya umma na ya kibinafsi kwa watu binafsi na jamii kwa jumla, kieneo na kilimwengu. Kwa upande mwengine, hadhara ya Kiislamu imetoweka kabisa katika hali halisi, kwa kule kujiweka mbali kwa watawala wa biladi za Kiislamu na utabikishaji wa Sharia kama mfumo kamili wa kimaisha, na badala yake kuridhia urasilimali ulio lazimishwa na Wamagharibi. Hivyo basi, swali linalojitokeza ni je, tutaelezaje kuhusu msururu wa taarifa zinazotolewa na viongozi wakuu duniani: George W Bush, Tony Blair, Nicolas Sarkozy, Vladimir Putin, Dmitry Medvedev, Charles Clarke na wengineo, ambapo wote katika hali tofauti tofauti wameapa kuzuia kuibuka kwa serikali ya Kiislamu na hivyo basi kuchukua kila hatua ya tahadhari kwa jaribio lolote la kutabikisha Sharia?? Nitamnukuu George W Bush pekee alipotangaza wazi mnamo 16 Septemba 2001 (siku 5 baada ya tukio la 9/11 ambalo kuna uwezekano mkubwa lilipangwa na vyombo vya usalama vya Amerika) “hivi ni vita vya msalaba, vita hivi dhidi ya ugaidi vitachukua muda”. Pia alionya kuwa “wanamgambo wanaitakidi kuwa kudhibiti nchi moja kutawajumuisha pamoja Waislamu nyuma yake, kuwawezesha kupindua serikali zote ‘poa’ za eneo hilo na kuasisi utawala wenye msimamo mkali utakao anza Uhispania mpaka Indonesia.”

Lau kama maono ya utabikishaji Sharia ingekuwa ndoto ya mbali, basi hakuna hata mmoja kati yao angejisumbua kuipinga, na kutoa vitisho wazi wazi vya kupigana na kurudi kwake! Ahmad Tumeh, aliyekuwa kiongozi wa serikali pinzani ya Syria aliyeko mafichoni, mnamo Novemba 11, 2015 alisema, amri ya kimataifa (yaani, dola za kimagharibi) kamwe haiwezi kukubali utabikishaji wa Sharia. Kuitisha utabikishaji wa Sharia ni jambo lisilo wezekana kulingana na uamuzi wa dola za kimagharibi; akasonga mbele na kutahadharisha kuwa “matakwa haya yatamaanisha umwagikaji mkubwa wa damu kwa ajili ya kuizuia”, yaani, dola za kikoloni za kimagharibi zimejitolea kidete katika kupiga vita kurudi kwa Uislamu kama mfumo kamili wa maisha.

Licha ya hayo, Waislamu wanaitakidi imani msingi ya Itikadi ya Kiislamu: Hakuna Mola ila Allah, na Muhammad ni Mtume Wake. Hivyo basi, viongozi wa kimagharibi, licha ya nguvu zao zote zisizo na mithili katika historia ya hivi karibuni na zamani, bado wana mapungufu ya kibinadamu; na licha ya majivuno yao wao si miungu, na nguvu zao za kijeshi haziwapi idhini ya kuzifanya sera zao za kihalifu kuwa haki, kando na kutaja vyombo vyao viovu vya habari walivyo navyo, na teknolojia ya kisasa katika kulemaza rai jumla ya kiulimwengu.

Allah Ta’ala amewawajibisha Waislamu kuishi kuambatana na mfumo wa maisha wa Kiislamu, katika hali yoyote ile, na kufanya kazi kuurudisha ikiwa haupo; si kwa sababu ya kutaharaki dhidi ya unyanyasaji, lakini kwa sababu ni jambo la kimaumbile kwa Waumini kuishi kuambatana na muongozo wa Allah, na kuuonyesha ulimwengu mzima uzuri wa dini Yake.

Umma wa Kiislamu umekataa hatma ya mwanzoni iliyo amuliwa juu yake na miji mikuu ya mbali ya kimagharibi. Mustakbali uliobuniwa na Wamagharibi kwa karne kadhaa ili kuufanya Umma uachane na Uislamu, uvunje ngao yake ya Dola ya Khilafah na kufikiria na kufanya kama wafanyavyo wengine. Kilicho salia katika muundo wa wamagharibi juu ya Umma pia kinakwenda kikidhaifika kila uchao huku ulimwengu wa Kiislamu ukiendelea na mwamko wake kamili kutokana na majanga ya karne iliyopita.

Kuupima Umma kiwango ulichofikia kwa sasa si vigumu. Kura za maoni na tafiti kadhaa zimeonyesha hamu hiyo ya kutaka umoja, na hata ikiwa mtu atakuwa na shaka juu ya kura hizi za maoni, kuna ushahidi wa kutosha kutoka katika ulimwengu wa Kiislamu, kuwa raia wake wanawakataa Wamagharibi na vibaraka wao waziwazi  na kuitisha Sharia na serikali ya Kiislamu. Lengo la uwepo wa kigeni katika ardhi za Waislamu ni kupanda mbegu ya mizozo na kugandamiza ulinganizi wa Khilafah.

Muongo mmoja na nusu uliopita umethibitisha kuwa miito ya kuzigeuza biladi za Kiislamu kwa hadhara ya kimagharibi inaambulia patupu. Hakuna yeyote aliyeshindwa kushajiishwa na ujasiri wa Waislamu wa Mashariki ya Kati. Mwaka wa 2011 ulishuhudia kufurika kwa watu mabarabarani kama njia ya kuonyesha upinzani wao nchini Tunisia, Misri, Libya, Yemen na Syria. Ingawa vibaraka wapya wamewekwa na chaguzi kufanywa: mapambano bado yanaendelea. Upinzani wa watu hawa ulilenga watawala katili, ushawishi wa kimagharibi na kimsingi dhidi ya nidhamu mbovu katika biladi zetu za Kiislamu, ambazo zimedumu katika kufeli kupeana hata mahitaji msingi kwa watu wetu.

Matukio haya pia yanatoa ushuhuda kuwa mpangilio wa sasa wa siasa za eneo, ulio shinikizwa na wakoloni wa kimagharibi kwa lengo la kuugawanya Umma, umefeli vibaya mno: nyoyo na akili za Waislamu zimeungana na kuonyesha umoja wao na huruma kwa ndugu zao Waislamu kote ulimwenguni: kuanzia Waislamu wa jamii ya Uyghur katika nchi iliyo kaliwa ya Turkestan, mpaka Rohingya, eneo la Asia ya Kati, Kashmir na Afghanistan, mpaka eneo la Afrika ya Kati, na kitovu cha maeneo yote haya kikiwa ni: Msikiti wa Aqsa na ardhi tukufu inayo uzunguka, Ash Sham kama ilivyo katika Surah Al-Isra.

Ndio dola za kimagharibi zimepanga njama zote, na kubuni kila aina ya urongo pamoja na unyama wa nchi za kiaskari zikiongozwa na vibaraka wake, walio jaribu kucheza karata za ukabila, ujamaa, demokrasia na urasilimali, ambazo zote zimefeli na hivyo basi kufungua njia kwa Waislamu kutambua kwa ukamilifu kwamba suluhisho pekee ni Uislamu.

Haishangazi kuwa Hizb ut Tahrir imeshiriki pamoja na Umma katika ya mvutano dhidi ya njama ya kimagharibi. Da’wah ya Hizb ut Tahrir imesambaa mbali na kwa mapana huku ikikumbatiwa na nyoyo na akili za waumini mukhlisina, wanaume kwa wanawake, wazee kwa vijana, eneo la Turkestan, Asia ya Kati, Indonesia, Malaysia – huku kongamano hili likiwa ni ushahidi tosha, Bangladesh, India, Pakistan, Afghanistan, katikati mwa eneo la Tatarstan, Caucasus, Crimea, vile vile Uturuki na biladi za kiarabu, huku ikifika mpaka Kenya na Nigeria.

Mbegu za mwanzo za da’wah hii iliyo barikiwa zilipandwa mjini Jerusalem, na mti mkuu wa da’wah hii ukaota mizizi kwa haraka nyoyoni na akilini mwa Waislamu eneo la Sham, Misri, Libya, na Tunisia. Mti huu mzuri kwa sasa unatoa kivuli kwa Umma wa Kiislamu karibu kila mahali.

Hizb ut Tahrir imefaulu kikweli kuunganisha Waislamu katika hamasa, itikadi, fikra na fahamu zao juu ya vizingiti vyote: haijali anakotoka Muislamu (mwanamume au mwanamke): anaweza kuwa anatoka Kenya au Bengal au Uzbekistan, anaweza kuwa ni wa dhehebu la kifiqhi la Hanafi, au Shafi, au Hanbali, anaweza kuwa mweupe au Malay au mweusi… lakini umbile lake la kindani la kibinadamu yeye ni muumini kwa Allah Subhanahu wa Ta’ala, na amejitolea kwa dhati kujisalimisha katika kumuabudu Bwana wa Ulimwengu… na huu ndio uzuri wa Uislamu, kuwa ni ujumbe wa rehma kwa wanadamu wote: sio kwa Waarabu, wala kwa Wafursi, wala kwa Wakurdi, wala kwa Waturuki pekee. Uislamu unawajibisha kuwa Muislamu awe ndugu ya Muislamu mwenzake, na Uislamu uko wazi kwa yeyote atakaye kuukumbatia pasi na mapendeleo yoyote au uzushi wa watu.

Hapa ndipo penye matunda ya Hizb ut Tahrir: kwa kufaulu kuunda jukwaa la kuunganisha Umma kikweli katika mvutano wa kurudisha Uislamu kama mfumo kamili wa maisha; chini ya Sharia ya Kiislamu haijalishi ikiwa Imam/Khalifah atatabanni ijtihadi hii au ile, kwani zote zachipuza kutoka katika Itikadi ya Kiislamu na uteremsho wa wahyi ndani ya Qur’an tukufu. Zaidi ya hayo, Hizb ut Tahrir imeonyesha wazi wazi njia ya kufikia utabikishaji kamili wa Sharia katika kukabiliana na kadhia zote za kimaisha. Hizb ut Tahrir imetoa vitabu vingi vikiwemo katiba kielezo, na vitabu vinavyo fafanua kwa kina nidhamu ya kiuchumi, ya kisiasa, ya kielimu, ya kifedha, siasa za kimataifa pamoja na ubebaji ulinganizi ulimwenguni kupitia Jihad. Na hasha katu hatutaogopa kulingania Jihad kama chombo cha kulingania ujumbe wa Uislamu ulimwenguni; hatuwezi kubadilisha wala kupinda amri ya Allah Subhannahu wa Taala, aliye amrisha katika Qur’an amri ya dhahabu ya kutolazimisha katika dini. Watu wako huru kufuata ukinaifu wao: ima kwa kukubali Uislamu au kuukataa.

Mafanikio ya Hizb ut Tahrir hayako tu katika kutoa muono safi katika kurudisha Uislamu kama mfumo kamili wa maisha kupitia kutabikisha Sharia chini ya dola ya Khilafah, bali pia yako katika kuzalisha kizazi cha wabebaji ulinganizi miongoni mwa sekta kadha wa kadha za Umma, katika kila biladi ya Kiislamu. Yeyote anayefuatilia mjadala huu wa hali zilizoko kwa sasa hawezi kukosa kutambua kuwa kutakikana kwa Uislamu kama mfumo kamili wa maisha chini ya Khilafah kumetawala anga.

Orodha ndefu ya vipindi vya runinga, makala ya magazeti, fatwa (au fatwa za kirongo) zilizotolewa na mashekhe “rasmi”, watumishi wa hawaa za madikteta nchini Misri, Jordan, Tunisia, Morocco, Uturuki, Tajikistan, Uzbekistan na nchi nyenginezo, orodha ni ndefu mno kiasi cha kukosekana nafasi ya kutosha hapa kuitaja yote. Ni ushahidi wazi kuwa dola za kikoloni za kimagharibi zinaogopa kuendelea kukua kwa ulinganizi wa Khilafah miongoni mwa Waislamu. Wakati Saudi Arabia ilipo amua kuasisi kituo cha kupambana na misimamo mikali kwa ushirikiano na ikulu ya White House, na kuwafuta kazi takriban maimamu 3000, na kufungua mlango kuruhusu ugeuzwaji wa jamii kwa hadhara ya kisekula ya kimagharibi chini ya kisingizio cha “burudani”, yote haya pamoja na kuimarisha uhusiano na wavamizi wa Kiyahudi wa Palestina, matukio yote haya yanathibitisha kuwa ulimwengu wa Kiislamu umeungana pamoja kukabiliana na vibaraka hawa wa dola za kimagharibi.

Baadhi ya watu wamekuwa wakiikashifu Hizb ut Tahrir kwa muda mrefu kwa kuwalingania viongozi wa majeshi ya Kiislamu kutoa nusrah kusimamisha Khilafah; matukio ya hivi majuzi eneo la Mashariki ya Kati yamethibitisha uhalali wa msimamo wake: kuanzia Algeria (1991) mpaka kwa mapinduzi ya kiarabu (2010 mpaka sasa). Ni wazi kuwa matakwa thabiti ya kurudisha Uislamu kama mfumo kamili wa maisha ni sharti ya ambatanishwe na usaidizi kutoka kwa miongoni mwa majeshi, ambao ni watoto halisi wa Umma, ili kuweza kujikomboa kutoka kwa udhibiti wa kikoloni na ili Umma uweze kufurahia matunda ya Sharia, ambayo si jengine isipokuwa ni rehma kwa wanadamu wote.

Dola za kimagharibi zimeamua kuanzisha kampeni ya kuichafulia jina Hizb ut Tahrir kwa kujaribu kwa fadhaiko kuinasibisha na ugaidi, ili kuhalalisha msako wao wa kinyama dhidi ya amali zetu. Alhamdulillah ulinganizi wetu hauhitaji kuhamiwa: tumeapa kuanzia siku ya kwanza kufuata nyayo za Mtume (saw) katika ubebaji ulinganizi, na vile vile tumefafanua wazi njia yetu kuwa tunafanya kazi na Umma ili pamoja tujenge rai jumla na uaminifu kwa Uislamu kama mfumo kamili wa maisha, na wakati huo huo kufichua ukweli juu ya serikali hizi fisadi zinazotumikia maslahi ya wamagharibi; katika kutekeleza mvutano wa kifikra pamoja na mvutano wa kisiasa, Hizb ut Tahrir kamwe haijawahi kuchukua msimamo kwa msingi wa kukubaliana na hali halisi au kujaribu kulegeza misimamo. Kilicho iwezesha Hizb ut Tahrir kufuata mkondo huu wa vitendo ni kule kuwa haitafuti isipokuwa radhi za Allah Subhannahu wa Taala pekee, na, huku ikijua kikamilifu maumbile ya serikali hizi fisadi, Hizb ut Tahrir imezipinga zote na imezichukulia zisokuwa za halali machoni mwa Sharia.

Katika wakati ambapo mfumo wa kiulimwengu wa kirasilimali unaugua kutokana na mgogoro mbaya katika ngazi zake zote: kisiasa, kijamii, na kiuchumi, wakati umewadia kwa mwamko mapya ya Uislamu.

Tumesoma taarifa kadha wa kadha kutoka kwa maafisa wa kuu wa Amerika kwamba ni wakati sasa wa kuuzika mpangilio wa Sykes-Picot, na kuunda upya ramani ya eneo hili ili kutumikia maslahi ya Amerika. Lakini sisi twasema wakati umewadia sasa kwa waumini mukhlisina wa Umma huu kufanya kazi nasi kujishindia jaha ya kuurudisha tena Umma wa Kiislamu mahali pake panapo stahili: pa kuongoza wanadamu kutokana na mateso na giza la mfumo wa kisekula wa kirasilimali uliofeli na kuwapeleka katika nuru na rehma ya Uislamu. Tunawasihi nyote na kwa wale wanao tutazama kuungana na njia hii ya kuunganisha Umma huu katika kuifahamu dini hii pamoja na kuitisha kurudi kwa Uislamu kama mfumo kamili wa maisha.

Vile vile tunawasihi wanajeshi na maafisa mashujaa wa majeshi ya Kiislamu kuharakisha katika kupata radhi za Allah Subhannahu wa Taala, kwa kutoa nusrah kwa Hizb ut Tahrir, kama ilivyo jitokeza katika Surah Al-Anfal,

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ﴿

“Enyi mlio amini! Muitikieni Allah na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Allah huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mutakusanywa” [Al-Anfal:24]

Namalizia kwa kuwakumbusha nyote kuwa Allah (swt) Mola wa Ulimwengu ameapa, na kiapo chake ni cha kweli, kuwa dini hii itatawala, basi tufanyeni bidii sote kujishindia jaha hii ya kuwa waja mukhlisina wa Allah wanaostahiki ushindi wake.

﴾إِنَّ الَّذِينَ يُحَادُّونَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ أُولَٰئِكَ فِي الْأَذَلِّينَ * كَتَبَ اللَّهُ لَأَغْلِبَنَّ أَنَا وَرُسُلِي إِنَّ اللَّهَ قَوِيٌّ عَزِيزٌ﴿

“Hakika wale wanao mpinga Allah na Mtume wake, hao ndio miongoni mwa madhalili wa mwisho. Allah ameandika: Hapana shaka mimi na Mtume wangu tutashinda. Hakika Allah ni Mwenye nguvu, Mwenye kushinda.” [Al-Mujadalah:20-21]

Kutoka Jarida la UQAB Toleo 12