Afisi Kuu ya Habari: Kongamano la Hitimishi la Kiulimwengu kwa Amali za Kampeni ya Kumbukumbu ya Karne Moja ya Kuvunjwa kwa Khilafah 1442 H – 2021 M

بسم الله الرحمن الرحيم

Katika mwezi wa Rajab al-Muharram wa mwaka huu 1442 H – 2021 M na Kwa mnasaba wa kumbukumbu chungu ya karne moja ya wahalifu kuivunja dola ya Uislamu mnamo 28 Rajab al-Muharram 1342 Hijria sawia na tarehe 03/03/1924 M ambayo ili simamishwa na Bwana wa mitume wote Muhammad (saw), na kukomesha mfumo wa utawala wa Kiislamu (Khilafah) ulionawirisha pembe za dunia kwa karne 13 zilizopita, na chini ya uongozi wa amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah, Mwenyezi Mungu amhifadhi, Hizb ut-Tahrir aliandaa amali kubwa za umma katika nchi zote ambazo inafanya kazi ndani yake chini ya kauli mbiu:

“Katika Kumbukumbu Karne Moja ya Kuvunjwa kwa Khilafah … Isimamisheni, Enyi Waislamu.”

Ikaihitimisha kwa kongamano hili la kiulimwengu ambalo lilihudhuriwa kikundi cha mashababu wa Hizb kutoka Malaysia Mashariki hadi Uingereza Magharibi, ambao waliakisi dori yao kwa mwelekeo Umma na hitaji lake la haraka la kurudisha nguvu zake zilizoporwa na kurudisha ubwana kwa Sheria, ili kutekeleza sheria ya Mwenyezi Mungu (swt) katika ardhi yake, kupitia mfumo wa Utawala wa Kiislamu (Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume).

Jumamosi 29, Rajab Al-Muharram 1442 H sawia na 13 Machi 2021 M