Ili Qur’an Isiwe Hoja Juu Yetu

Hizi ni sifa 10 mbaya kwa wanaosoma qur’an kisha wasiifanyie kazi

Anayehifadhi Qur’an na kuisoma pasi na kufanya kazi ili itawale, anakua na hizi sifa hatari:

1- yeye haichukui qur’an kwa nguvu na anakhalifu makusudio ya Allah ya kuteremsha risala: 

Anasema qurtubiy katika kuitafsiri kauli ya Allah taa’la 

خُذُوا مَا آتَيْنَاكُم بِقُوَّةٍ﴿

(Shikeni kwa nguvu haya tuliyo kupeni)

Haya ndio makusudio ya kuteremshwa vitabu, Kufanya kazi kwa majibu wa vitabu na sio kuisoma tu kwa ulimi na kuighani..

2- Anaitupa Quraan: 

Anasema Qurtubiy: … Hakika kuitupa qur’an kwa aliyoyasema Assha’biy na ibnu uyaynah, ni qawli yake taa’la: 

(وَلَمَّا جَاۤءَهُمۡ رَسُولࣱ مِّنۡ عِندِ ٱللَّهِ مُصَدِّقࣱ لِّمَا مَعَهُمۡ نَبَذَ فَرِیقࣱ مِّنَ ٱلَّذِینَ أُوتُوا۟ ٱلۡكِتَـٰبَ كِتَـٰبَ ٱللَّهِ وَرَاۤءَ ظُهُورِهِمۡ كَأَنَّهُمۡ لَا یَعۡلَمُونَ)

[سورة البقرة 101]

(Na alipo wajia Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu, mwenye kuthibitisha yale waliyo nayo, kundi moja miongoni mwa wale walio pewa Kitabu lilitupa Kitabu cha Mwenyezi Mungu hicho nyuma ya migongo yao kama kwamba hawajui.)

3- Hakuifahamu Qur’an : 

Anasema shaykhul Islam ibnu taymiyah katika kuitafsiri kauli ya Allah taa’ala: 

(وَمِنۡهُمۡ أُمِّیُّونَ لَا یَعۡلَمُونَ ٱلۡكِتَـٰبَ إِلَّاۤ أَمَانِیَّ وَإِنۡ هُمۡ إِلَّا یَظُنُّونَ)

[سورة البقرة 78]

(Na wako miongoni mwao wasio jua kusoma; hawakijui Kitabu isipokua uongo wanao utamani, nao hawana ila ni kudhania tu.)

Sifa hii ni kwa yule asiyefahamu maneno ya Allah na kuyafanyia kazi, ye anatosheka na kuisoma qura’ni tu.

4- Anaigura Qur’an: 

Ibnul qayim ameweka idadi ya kuigura qur’an katika sampuli kadhaa:

Kuiguru katika kuitawalisha na kuhukumiana nayo katika Misingi ya dini na matagaa yake). Alfawaid ya ibnul qayim (82/1).

5- Haizingatii Qur’an wala hasimamishi Yale yaliyoteremshwa Qur’an kwa ajili yake:

Assma al-hasanul basriy : Qur’an iliteremshwa ili izingatiwe na kufanyiwa kazi. Madariju salikin (485/1).

6- Anakhalifu manhaj ya salaf (wema waliotangulia) katika kuamiliana na Qur’an: 

Asema ibnu masu’d : Tulipata uzito wa kuhifadhi matemshi yake -Alfadh- na ikawa sahali kwetu kuifanyia kazi Qur’an, na hakika waliokuja baada yetu imekua sahali kwao kuhifadhi Qur’an na ikawa uzito kwao kuifanyia kazi. 

Al-jaami’ liahkaamil Qur’an (40-1/39) 

7- Haisomi haki ya kuisomwa: 

Amepokea ibnu kathiir kutoka kwa ibnu masu’d asema: naapa na yule ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake! Hakika haki ya kuisoma Ni kuhalalisha halali yake na kuharamisha haramu yake…” Tafsir ibnu kathir (4003/1) na anasema Asshwakani : يتلونه: Wanayafanyia kazi yaliyomo katika Qur’an. (Fathul qadir (135/1).

8- Anaingia katika kauli yake Allah :

(مَثَلُ الَّذِينَ حُمِّلُوا التَّوْرَاةَ ثُمَّ لَمْ يَحْمِلُوهَا كَمَثَلِ الْحِمَارِ)

(Mfano wa walio bebeshwa Taurati kisha wasiibebe, ni mfano wa punda).

Hawakuibeba kwa maana ya kutoifanyia kazi taurati na ilihali imo mikononi mwao- wakapigiwa mfano wa punda anayebeba vitabu na hapati lolote zaidi ya uzito wa mzigo usiokua na faida. Alqurtubiy.

9- Anastahili dua ya mtume s.a w ( ثكلتك أمك) Akukose mamako kwa kifo:

Kutoka kwa ziyad bin labid asema mtume s.a.w alitaja kitu akasema: hilo ni wakati wa kutoweka elimu, nikasema : ewe mtume wa Allah vipi elimu itatoweka na ilihali sisi tunaisoma Qur’an, na kuwasomesha watoto wetu, na watoto wetu kuwasomesha watoto wao mpaka siku ya qiyama? Akasema: akukose mamako kwa kifo (ثكلتك أمك) Ziyad ijapo nakuona ni katika wenye elimu na ufahamu katika watu wa madina, je si hawa mayahudi na manaswara, wanaisoma Taurati, na injili Lakini hawafanyii kazi chochote kilicho katika vitabu vyao) ibnu maajah.

10- Qur’an itakuja kua hoja juu yake : 

Anasema mtume s.a.w : Na qur’an ni hoja kwako au juu yako) Muslim.

Maana yake iko wazi ni unufaike nayo unapoisoma na kuifanyia kazi, na lau sivyo basi ni Hoja juu yako. Sharhu nawawi kwa Muslim.

 

Ewe mola tujaalie miongoni mwa wale wanaomaliza umri wao na ubarobaro wao wakiwa wanafanya kazi ya kuitawalisha Qur’an na kuisimamisha dola yake, na kunyanyua bendera yake hivi karibuni.

 

Hizi ni dalili zilizo wazi kwa watu wote

 

Abu nizar al-shamiy