Mfumko wa bei: Tatizo sugu ndani ya Mfumo muovu wa Kiuchumi wa Kibepari

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Wakenya wa kawaida kwa sasa wanakumbana na hali ngumu ya maisha kufuatia  ongezeko kubwa la bei ya bidhaa muhimu kama vile unga wa ngano, sukari, mkate na mafuta ya kupikia. Tatizo hili ambalo limekua ni sugu linalowaacha  wakenya taabani huku ikizingatiwa kwamba zaidi ya nusu yao wanaishi katika hali ya uchochole. Harakati ya Kiislamu ya Hizb ut-Tahrir Kenya ingependa kusema yafuatayo:-

Wakati ambapo umma unakumbana na hali hii ngumu ya kiuchumi, viongozi wamejitia hamnazo wanajihusisha na porojo za kisiasa zisizomnufaisha raia bali ni kugombania tu madaraka ili kuendelea kujitajirisha. Hali hii ya kutamausha inatokamana moja kwa moja na usimamizi duni wa kiuchumi wa serikali. Taifa la Kenya kama lilivyo taifa lolote linaloshikilia  mfumo wa kibepari unaoruhusu uchukuaji wa mikopo iliosheheni riba hali inayolazimu serikali  kutumia njia ya utozwaji mkubwa wa ushuru  karibu katika kila huduma na bidhaa ili kugharamia madeni.

Mfumuko wa bei huwa ni tatizo la mara kwa mara ndani ya mfumo wa Kibepari uliochukua mfumo wa pesa za makaratasi sizokuwa na faida halisi kwani haiwezi kubadilishwa kwa kitu chochote chenye kushika.Thamani yake huchukuliwa tu kutoka kwa ugavi na mahitaji tu. Ukosefu huu wa thamani yenye faida hufanya pesa za makaratasi kukosa thamani ya kudumu hivyo hushuka na kupanda, hali inaypotalizwa na wakiritimba kuweza kuchapisha pesa zaidi wakati wowote ule. Kwa hatua ya hiyo wao ndio wakwanza kujipatia mtaji mkubwa wa pesa zisokuwa za halali kwao, seuze husababisha mfumoko mkubwa wa bei ambao hakuna ukuaji wowote wa  mapato. Ifahamike kwamba katika mfumo wa Kibepari suala la mfumo wa bei pamoja na muundo wa kisarafu ni silaha zinazotumiwa kudhibiti usambazwaji wa bidhaa na huduma.

Uislamu una sera imara ya kisarafu iliosimama  juu ya msingi kisarafu za chuma zilizo na thamani yenye kushikika. Hapa ndio huja ule mfumo wa Dhahabu na Fedha kama thamani mbadala ya sarafu, mfumo huu hufanya usambaswaji wa sarafu kuwa imara wakati wowote hivyo mawakala wenye uchu wa kupapia mali wa sekta za fedha kutoweza kuhujumu usambazwaji wake kwa mapato ya muda mfupi. Kwa kuegemea mfumo wa dhahabu na fedha, tatizo la mfumoko wa bei huwa  mdogo ama kukosekanwa kabisa ndani ya mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu.Zaidi ya haya, Mfumo wa Kiuchumi wa Kiislamu huzingatia zaidi mikakati na sera za  kuufanya uchumi ni wenye kukua kwa kasi, hii ni kwa kupitia utumiaji mzuri wa mali ghafi  katika kuunda viwanda vitakavyoajiri watu wengi. Twasema kutekelezwa mfumo wa Kiuchumi ndani ya dola ya Khilafah kutahakikishia raia chakula cha kutosha pamoja na kutatua tatizo la kupanda kwa gharama za maisha.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari

 Hizb ut- Tahrir in Kenya