Mfumo wa Kiuchumi wa Kiislamu Pekee chini ya Khilafah ndio utakao nasua  Kenya na Ulimwengu kwa ujumla dhidi mitego ya uchumi wa Riba.

Habari:

Deni la Kenya lishafika Sh.8.4 Trilioni na kwa kasi linakaribia kuwa sh.9 trilioni  nab ado  serikali inanuia kuomba zaidi mikopo kama hatua yake ya kupambana na janga la Covid -19. Kiwango hiki cha deni ni zaidi ya robo tatu ya mapato jumla yote ya kiuchumi ya nchi ambayo kitaalamu hujulikana kama GDP. Kwenye ripoti  ya kimkakati wa kuinua uchumi 2020-22  inayojulikana kama Post Economic  Recovery, wizara ya fedha imedokeza kwamba kufikia Agosti 2020, tayari deni lilifikia Sh 7.06 Trilioni kiwango hiki ni asilimia 69.2 ya Pato jumla la nchi GDP. Mwezi Novemba 2020, kwenye stakabadhi yake, wizara ya fedha ikasema: “Haya kwa ujumla na deni ambalo halijalipwa la Sh1.35 trilioni linamaanisha kuna kiasi cha deni la umma la Sh8.41 trilioni dhidi ya kiwango cha mwisho cha deni kuchukuliwa cha  Sh9 trilioni, ikimaanisha kuwa serikali kwa sasa ina nafasi finyo kuendelea  kukopa zaidi, ”

Maoni

Takwimu hizi zinaelezea hali tete ya  jinsi Kenya inavyoporomoka kwenye kingo za mporomoko wa kifedha na hivi karibuni itaiwia vigumu sana kuweza kulipa mikopo yake. La kutamausha zaidi, tarakimu hizi  zinatafsiri kwamba kila raia wa Kenya pamoja na wale wanaozaliwa sasa anadaiwa takriban  Ksh 139,000. Makala moja yaliyochapishwa kwenye gazeti la  Business Daily yalitaja makadirio kuwa  kuwa kiwango cha kukimbia cha kukopa Kenya chini ya utawala wa sasa kitakuwa Sh2.5 bilioni kwa siku hadi uchaguzi ujao. Hii itamaanisha kwamba karibu asilimia 60 ya ushuru utakuwa ukigharamia ulipwaji wa madeni, hali itakayolazimu kuweko na kiasi kidogo cha fedha katika mipango ya haraka kama vile kufufua sekta ya afya inasuasua. Kuendana na ratiba hiyo ya ulipaji, serikali itatumia mfumo mkali zaidi wa ushuru – ambao unaweza kubana biashara zaidi na kudhoofisha mustakabali wa biashara nchini Kenya.

Wataalamu wa Fedha katika mfumo wa kiuchumi wa Kibepari wanasema kuwa deni sio lazima liwe na madhara kwa uchumi, ikiwa inalinganishwa na mizunguko ya biashara) inaweza kutuliza uchumi na kukuza ukuaji wa uchumi. Walakini, hawakatai ukweli kwamba riba na ulipaji mkuu wa deni ya nje hufanywa kwa pesa za kigeni ambazo hakika hupunguza akiba ya fedha za kigeni ya nchi na inaweza kushusha thamani ya sarafu ya ndani. Kwa kuongezea, sarafu dhaifu husababisha viwango vya juu vya mfumuko wa bei kwa muda mrefu kwa sababu inagharimu nchi zaidi kuagiza kile inachohitaji kwa uzalishaji na matumizi.

Sera za kikoloni za Kiliberali pamoja na taasisi za kifedha kama taasisi zinazojulikana kama Makubaliano ya Washington (kwa kuwa yalifanywa Washington DC), Sera za Marekebisho ya Miundo (SAPs) zimewekwa na mataifa ya kimagharibi  kwa nchi kama Kenya kuhakikisha ulipaji wa deni na ukarabati wa uchumi. Lakini njia ambayo imetokea imehitaji nchi masikini kupunguza matumizi kwa vitu kama afya, elimu na maendeleo, wakati ulipaji wa deni na sera zingine za uchumi zimefanywa kuwa kipaumbele. Kiuhakika ni kwamba , IMF na Benki ya Dunia wamedai kwamba mataifa masikini yapunguze kiwango cha maisha cha watu wao!

  Jinamizi la kukopa linaweza kutokomezwa katika mfumo wa uchumi ambao huangamiza kabisa mifumu yote ya kiuchumi inayojipeleka kwa misingi ya riba. Mabadiliko hayo yako katika mfumo wa uchumi wa Kiislamu; mfumo wa kipekee wa kiuchumi ambao usioruhusu kabisa riba kama msingi wake wa kiuchumi. Mfumo unaoonekana hutumia rasilimali kwa masilahi ya umma. Kwa kuongezea, hali hiyo inataka uongozi huru unaowajibika usioegemea  kuamriwa na kufanywa mateka na taasisi za kifedha za kigeni. Uongozi huo ni Khilafah- serikali huru ni sera za ndani na nje ziko huru kutoka kwa ushawishi wa kigeni. Kwa kweli ni serikali ya Khilafah ambayo itaukomboa ulimwengu wote kutoka kwa uchumi potofu wa kiliberali na kuwalinda wanadamu kutoka kwa utumwa wa kiuchumi na mabepari wenye tamaa.

Imeandikwa kwa niaba ya Afisi kuu ya Hizb ut-Tahrir na

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa vyombo vya Habari  Hizb ut-Tahrir Kenya

30/12/2020