Mkataba wa Kuuza Mashini kabla Kuitia Mkononi

Ufupisho wa Suali na Jawabu – 11

Suali

Nina nafasi ya sehemu na ndani yake kuna mashini yangu ya useremala. Alinijia mtu mmoja kutaka kuinunua mashini hiyo nami nikakubali kumuuzia. Baadae akaniomba nimkodishie ile sehemu ambayo hiyo mashini iko ili aweze kuifanyia kazi ikiwa mahali papo hapo. Mkataba ukafungwa kwa makubaliano hayo.Fahamu ya kwamba mashini hiyo ina uwezo wa kuondoshwa sehemu hiyo lakini ilibakishwa sehemu hiyo hiyo iliyokuwa, na pia funguo za sehemu hiyo ziko na yule mtu aliyekodishiwa sehemu hiyo na ambaye ana miliki mashini hiyo na anapata manufaa kamili ya sehemu hiyo na ana uhuru wa kuitumia sehemu hiyo bila kufanya uharibifu au kuiharibu.

Je mkataba huu kati yetu unatimiza masharti ya Shari’ah ikiwa mashini haikuondoshwa? Au mkataba huo utakuwa hauruhusiwi (batil) kwa kutoiondosha mashini na kuiwacha ndani ya sehemu hiyo ambayo mnunuzi wa mashini ameikodisha?

Jibu

Ni sharti katika kuuza kupokea kitu na kukitia mkononi, lakini hili ni katika vitu ambavyo vinapimwa kwa uzani, kipimo na idadi, mfano kununua vitambaa au chakula kama mchele au kununua machungwa au maembe kadha. Vitu kama hivyo ambavyo vina uzwa kwa kupimwa kwa uzani au vinavyopimwa kwa kipimo (futi, dhira’a) au kuuzwa kwa idadi kama machungwa n.k. Vyote hivyo vinapouzwa, hutakiwa kuondoshwa na mnunuwaji kutoka sehemu ya muuzaji. Napia kwa muuzaji, ili vitu hivyo viwe ni milki yake na kuweza kuviuza ni lazima avitie mkononi na kuvipeleka dukani kwake.

Kwa hivyo, hairuhusiwi kwa mfanyi biashara kuuza bidhaa ambayo haimiliki, yani haiko dukani kwake. Mtume (saw) alisema:

“Yeyote anayenunua chakula asikiuze mpaka akitie mkononi” [Bukhari]

Muslim amesimulia kuwa Mtume (saw) alisema:

“Yeyote anayenunua chakula, asikiuze mpaka akipime”

Iko wazi kuwa hadithi hizi zimetaja uzani na kipimo na pia imetajwa kwa ujumla katika chakula. Chakula ni ima hupimwa kwa uzani, au kwa kipimo au kwa idadi (mfano matunda). Hivyo basi, ulazima wa kuvitia mkononi ni sharti katika mkataba wa uuzaji wa vitu vyote ambavyo vina ukadiriaji wa chakula, uzani, kipimo au idadi.

Ama kuhusu vitu ambavyo havipimwi kwa uzani, kipimo au idadi, kuvitia mkononi sio sharti ya uuzaji. Mfano uuzaji wa nyumba, ardhi, wanyama n.k, kwa sababu nyumba na ardhi haziwezi kuhamishwa. Ama mnyama ni kwa mujibu wa dalili iliyosimuliwa na Bukhari kutoka kwa Ibn Umar kuwa alikuwa anamuendesha farasi aliyekuwa anasumbuwa wa Umar:

“Mtume (saw) akamwambia Umar: Niuzie. Umar akamwambia: Nimekuuzia. Mtume (saw) akamnunua na hapo hapo akamwambia Abdullah huyu ni ngamia wako, waweza kumfanya upendavyo”

Katika Hadith hii Mtume (saw) amenunua ngamia kutoka kwa Umar (ra) na kumuuzia papo hapo Abdullah (ra) bila kumtia mkononi ngamia huyo. Hivyo basi uuzaji wa wanyama na mfano wake ambao hautegemei uzani, kipimo au idadi katika kuuzwa kwake, hailazimu kuvitia mkononi kuwa ni sharti katika mkataba wa uuzaji.

Kwa sababu hizo mashini ya useremala uliyoulizia ni kama mnyama, hivyo waweza kuiuza bila kuihamisha sehemu iliyokuwa. Kwa maana nyingine mkataba wa uuzaji uko sawa ima mnunuzi ataihamisha kuipeleka kwake au kukodisha sehemu mashini iliyopo na kuibakisha papo hapo, na kuuzwa kwake kuko sawa.

 

Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye Hekima.

Link ya Kiengereza: http://hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/qestions/jurisprudence-questions/14761.html

Chanzo: Hizb ut Tahrir Kenya

25 Shaaban 1439 Hijria

11 Mei 2018 Miladi