Msongo wa Mawazo: Adhabu ya Kiulimwengu chini ya Urasilimali.

Habari:

Nakuru, Kenya: Daktari wa Hospitali moja Mjini Nakuru aliegonga vichwa vya habari baada ya kuripotiwa kuwauwa watoto wake wawili na hatimaye naye akafariki dunia akiwa ni mwenye kupokea matibabu katika Hospital ya Nakuru level 5 alizikwa. Dkt James Mureithi alizikwa kwenye bomba la Familia huko Gilgil pamoja na watoto wake siku ya Jumanne. Mwili wa Daktari huyo ulizikwa kwenye kaburi moja huku miili ya watoto wake–mvulana na msichana wakazikwa kwenye kaburi la pamoja. Daktari huyo yasemekana aliwachoma sindano wanawe Dylan Gakara (5) na dadake Hailey Karuana (3), sindano hiyo inasemwa kwamba ilikua imechanganywa na dawa mbalimbali ikiwemo ya insulin. Baada ya kuwadunga akawaacha chumbani mwao  wakiwa taabani hadi wakakumbana na kifo chao. Baadaye naye akaelekea kwenye chumba chake na kujidunga sindano akijaribu kujiua. Kisa hicho kiliripotiwa jioni ya Septemba 18. Gakara alikufa siku septemba 23 yaani siku tatu baada ya kuwa anapokea matibabu. Wakati wa mazishi yake eneo la Mbaruk huku Gilgil, madaktari wenzake walieleza kuwa alikuwa Daktari mwenye huruma na mwenye kuwapokea wagonjwa wake vyema.

Maoni:

Huku nchi ikiamkia na habari za kutamausha za mauaji ya watoto wawili mikononi mwa mtu ambaye kisheria alikuwa awajibike katika kulinda usalama wao dhidi ya madhara ya aina yoyote yale, kunaibuka masuali mengi juu ya msingi wa Jamii ndani ya Urasilimali. Mtekelezaji wa mauaji haya alikuwa ni mtu aliepata ufanisi mkubwa kwa mujibu wa twaswira ya Urasilimali.Alikuwa ni mmiliki wa zahanati mbili za kibinafsi akiishi maisha mazuri kama mtu mwenye kiwango cha mapato ya kadri katika jamii. Kwa ghafla tu mara anasitisha uhai wake na wa watoto wake, dalili wazi ya msukosuko wa Kihisia katika nyanja zote za maisha katika jamii.

Mtu kujiua ni kitendo kiovu mkubwa seuze kuuwa familia nzima itakuwa ni uovu uso kifani nayo ni athari kubwa ya moja kwa moja ni athari ya utakelezwaji wa fikra za kilebrali za Urasilimali unaoamini tamaa za Kimada zisokua na hata chembechembe za uroho,ubinadamu na hata maadili. Kama jinsi ya Mfumo ulivyokuwa mbaya, mwanadamu anaishi katika lindi la msongo wa mawazo akikosa mafungamano yoyote na Mola wake.

Maisha yanayokosa maadili mema yatokayo kwa kwenye itikadi yenye mashibu toshelezi kinaifu kwa tatizo msingi la mwanadamu bila shaka humpelekea mtu kwenye ufahamu wa kimakosa na kumkosesha ufahamu sahihi juu ya malengo ya maisha muongoza pia kumnyima ufahamu kutambua nini furaha na mafanikio. Kwa msingi huu wa kimakosa,mwanadamu huwa muovu kiasi cha kufika hadi ya kukosa kabisa utu. Hivyo, sio ajabu kuibuka kwa matendo kama haya ya kutamausha  ya kujitoa uhai na mengine mengi, ambayo leo yamekua ni mazoea duniani. Kwa bahati mbaya kwenye mfumo ulioko hakuna suluhisho juu ya matatizo haya.

Uislamu –mfumo wa kweli unaombatana na maumbile ya mwanadamu na pekee wa kiulimwengu unaongoza wanadamu kutoka kwa kiza hadi nuru. Mfumo ambao muongozo wake na sheria zake ni suluhisho kwa matatizo yote ya kibinidamu yawe ya kijamii, Kiuchumi na kisiasa. MwenyeziMungu SWt asema:

وَمِنَ النَّاسِ مَنْ يَشْتَرِي لَهْوَ الْحَدِيثِ لِيُضِلَّ عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَيَتَّخِذَهَا هُزُوًا ۚ أُولَٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مُهِينٌ

Na katika watu yupo anayenunua maneno ya upuuzi ili kupoteza katika njia ya Mwenyezi Mungu pasipo elimu, na kuifanyia mzaha. Hao watapata adhabu ifedheheshayo

 [TMQ 31:7]

 

Enyi watu wenye akili!  hadi lini mtavumilia maovu yanayotokamana na fikra za kileberali na mfumo wake?  Wakati umewadia kwenu kutambua haja ya mabadiliko ya kimsingi –mabadiliko yatakayorudishia watu ufahamu wa maana hali ya uhai na malengo yake.

 

Imeandikwa kwa Niaba ya Ofisi kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir na

Ali Omar Albaity

Mwanachama wa Ofisi ya Habari Hizb ut-Tahrir

Kenya.