Vita dhidi ya Ufisadi vitafaulu kwa Kuuondosha Mfumo batili wa Kisekula wa Kirasilimali

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kenya hivi sasa imezama katika ufisadi mkubwa usioingia akilini wa kashfa za kifedha za mabilioni ya pesa yanayodaiwa kuibwa kutoka katika mfuko wa Ummah. Kashfa aina hii ni za kujirudia kama ilivyotokea katika utawala wa Uhuru ndani ya awamu ya kwanza ya uongozi wake. Lililochungu zaidi zinatokea wakati ambapo raia wanaumia kutokana na mafuriko, hali duni ya sekta ya elimu, afya na kwa ujumla miundo mbinu iliyoduni n.k.

Hizb ut Tahrir / Kenya, ingependa kupaza sauti yake kwa yafuatayo:

Kwanza, kashfa hizi mpya sio za kwanza kuripotiwa na hazitokuwa za mwisho; kashfa aina hii zimetokea tangu miaka 54 tokea ‘uhuru’ na zinaendelea bila kusitishwa. Hakuna kiongozi mkuu katika serikali amewahi kufungwa na lau atafungwa itakuwa ni mbinu tu ya kuwanyamazisha wanaopiga kelele. Kwani wezi wamezitia mkononi afisi za kuongoza mashtaka na mahakama.

Pili, huu mkumbo mpya wa kashfa ni kwa sababu ya mfumo wa kisekula wa kirasilimali ambao mtizamo wake juu ya maisha umejengwa juu ya manufaa (ulimbikizaji mali) ili kushibisha mahitaji ya kiwiliwili. Hivyo basi, maisha jumla ya watu yamekitwa katika mashindano ya kipuzi na ya kuendelea ya ulimbikizaji mali ili kukata kiu isiyokwisha ya utajiri kupitia kila njia wanayoweza bila kuzijali dhamana za afisi wanazofanyia kazi.

Tatu, Wakenya kwa jumla lazima wazinduke na waanze kutathmini hali zao za kutamausha na zilizofanyiwa makusudi. Pia, wajiulize hakuna njia ya kujinasua na uizi huu na machafu mengineyo katika jamii, marekebisho ya kila uchao ya sheria za mwanadamu ambazo zinaendelea kuyaumiza maisha yao kila siku?

Nne, tunawashauri watu wa Kenya hususan wanafikra na wasomi kwa moyo mkunjufu wausome Uislamu kama mfumo na uongozi mbadala wa kifikra kwa wanadamu. Katika usomi wao, wahakikishe wanafanya ulinganisho wa kifikra kati ya mfumo wa kisekula wa kirasilimali na mfumo wa Kiislamu namna inavyotatua matatizo ya wanadamu na ikiwa suluhishi hizo zilizopendekezwa zinaambatana au zinakwenda kinyume na maumbile ya mwanadamu. Uislamu kama mfumo, unapiga vita ufisadi hivyo basi unawalaani wale wote wanaojihusisha ikiwemo kutoa hongo na ufisadi. Jukumu la kupambana na ufisadi ni la kipamoja na sio la watu binafsi au tume. Uislamu umelazimisha kiongozi achukue hatua kali dhidi ya yeyote atakayejihusisha na ufisadi bila kujali cheo chake katika jamii.

Kupitia mikakati hiyo, Uislamu kwa karne kumi na tatu wakati Uislamu ulitawala nusu ya ulimwengu, ufisadi ulikuwa adimu. Pia, Khilafah ikisimama tena kwa njia ya Utume, uchafu wa ufisadi na uchafu mwengine utaondoshelewa mbali.

Hatimaye, Hizb ut Tahrir imekinai kuwa mabadiliko msingi ambayo yamependekezwa na Uislamu kama suluhisho ya majanga kama ufisadi na ubwenyenye wa kisiasa kama inavyoshuhudiwa ndani ya jamii za kisekula za kirasilimali nchini Kenya. Tungependa kuikumbusha jamii ya Kenya kwamba Mwenye Nguvu Muumba amewaridhia wale wanaojifunga na maamrisho yake na kuyaepuka makatazo yake. Kinyume na hivyo, hakuna lolote jema litakalopatikana; hivyo basi ufisadi na mengineyo ni mfano wa hayo mabaya

Shabani Mwalimu
Media Representative of Hizb ut Tahrir in Kenya

KUMB: 11 / 1439 AH

Jumatatu, 19 Ramadhan 1439 H

04/06/2018 M

 

Simu: +254 707458907

Pepe: mediarep@hizb.or.ke