Tuongezeni Juhudi Zetu Maradufu Katika Kuifanyia Kazi Mama wa Faradhi Zote

Tarehe 28 Rajab 1439 itakuwa ni kumbukumbu ya kuondolewa kwa Khilafah. Mmoja katika watoto watukufu wa Ummah huu Kathim Qara Bakir, Jenerali wa Khilafah ya Kiuthmania, alisema, “Nimeapa kuzuia hatua zozote zitakazo chukuliwa kwa lengo la kuibadilisha nchi hii kutoka kuwa Usultan mpaka kuwa jamhuri, hata kama kujitolea muhanga huko kutakuwa ghali kiasi gani”. Mustafa Kamal msaliti, msekula alisimama dhidi ya maneno haya mazito ya jenerali huyo na kufanya kazi pasi na kuchoka kusababishia ulimwengu wa Kiislamu uhalisia mchungu yaani kuvunjwa kwa Khilafah. Tukio hili lilitokea jijini Istanbul mnamo 28 Rajab 1342 H ikiafikiana na tarehe 3 Machi, 1924 ni mojawapo ya matukio ya kuchukiza mno katika historia ya Kiislamu.

Ndio, hakika kuondolewa kwa Khilafah kulisababisha kuzuka kwa majanga ndani ya ulimwengu wa Kiislamu na ulimwengu mzima kwa jumla. Ummah huu mtukufu kwa sasa unaishi chini ya idhilali ya ufisadi wa urasilimali na unakabiliwa na ugandamizaji, ufukara na baya zaidi ni kutohukumu au kutotekeleza Sharia ya Allah, Muumba wa Ulimwengu! Kibla chetu kimegeuka na kuelekea Washington ambako maagizo na amri zinatolewa kwa ajili yetu. Ardhi zetu zinatawaliwa na Ruwaibidha ambao pamoja na mabwana zao hawaleti chochote ila fedheha. Ummah huu umo ndani ya faudha kikamilifu. Baya zaidi ni yale yanayo shuhudiwa nchini Syria kwa sasa ardhi ambayo Mtume () aliita al-Sham twahara zaidi katika ardhi za Allah, sehemu ambayo dini, Imani na usalama zinapatikana katika nyakati za mzozo. Ardhi ambayo Waislamu chini ya uongozi wa Umar (ra) ilifaulu katika kuifungua ile inayojulikana Syria ya leo na maeneo pambizoni mwake. Syria kwa sasa ni eneo linalo waka moto. Vita sasa vimefikia takriban muongo mmoja, kutokana na hisia ya unyanyasaji unaofanywa juu ya Waislamu kwa zaidi ya miongo minne chini ya katili wa kiimla wa Kibaathi Bashar al-Assad aliye mrithi babake al-Hafidh katika utekelezaji uovu. Amerika pamoja na Urusi zinashambulia kutoka angani, ardhini na baharini. Maelfu wakimemo kina mama na watoto wameuwawa. Hali nchini Syria imepelekea kutokea kwa janga la wakimbizi la viwango vikubwa mno, ambavyo havijawahi kushuhudiwa tangu Vita vya Pili vya Dunia.

Hakika ni kwa kukosekana Khilafah ndipo taswira za umasikini, baa la njaa, ukame na la kusikitisha zaidi vita vya wenyewe kwa wenyewe vinaoneka kama nembo za Afrika. Tangu kinyang’anyiro cha wakoloni wa ulaya kwa bara la Afrika cha madini na rasilimali nyingi za bara hili katika karne ya 20, bara hili tajiri lilifanywa kuwa tu mkondo wa usambazaji kwa falume zao. Ni kinaya, kwa Donald Trump kuiita Afrika kuwa nchi za mashimo ya kinyesi. Chini ya urasilimali, kilio cha Afrika leo kiko mbali na ilipokuwa siku za nyuma. Kuiangalia kwa upesi historia ya Afrika chini ya Khilafah, ingawa si Afrika yote ilitawaliwa na Khilafah bali ni baadhi ya sehemu tu za bara hili zilizofunguliwa na Khilafah. Kufikia katikati mwa karne ya 6 mpaka karne ya 7 kwa mfano, Afrika Kaskazini ilikuwa tayari ishafunguliwa na Khilafah hivyo basi miji mikuu mingi kama Tripoli – Libya, Tunis – Tunisia ilikuwa ikidhibitiwa na Waislamu. Miji yote hii kwa ujumla ilikuwa ikijulikana kama mikoa ya Kirumi barani Afrika. Katika eneo la Mashariki mwa Afrika, mwanga wa Khilafah ulionekana wakati wa Khilafah ya Abdul Malik bin Marwan, sehemu za Somalia ya leo ikiwemo Mogadishu, zilikuwa chini ya kivuli cha Dola ya Kiislamu. Hili lilichangia kuenea kwa Uislamu katika baadhi ya miji ya mwambao wa pwani kama Mombasa, Dar es-salaam, Zanzibar, Kilwa na Msumbiji.

Kuondolewa kwa Khilafah kulimaanisha kuyafungua mafundo ya Uislamu.

Abu Umamata Al-Baahili amesimulia kuwa Mtume (saw) amesema:

ليُنْقَضَنَّ عُرَى الْإِسْلَامِ عُرْوَةً عُرْوَةً فَكُلَّمَا انْتَقَضَتْ عُرْوَةٌ تَشَبَّثَ النَّاسُ بِالَّتِي تَلِيهَا وَأَوَّلُهُنَّ نَقْضًا الْحُكْمُ وَآخِرُهُنَّ الصَّلَاةُ

Mafundo ya Uislamu yatafunguka moja baada ya moja, kila fundo moja litakapo funguka watu wataligwia fundo jengine, na fundo la kwanza kufunguka ni Hukmu na la mwisho kufunguka ni Swala

(Imeripotiwa na Hakim na Ahmed)

Ndio, kwa hakika kuwepo kwa Khilafah kuliyafanya mafundo ya Uislamu kufungika imara. Hakuna damu iliyo mwagwa pasi na hatia.

Kuendelea kuyahesabu majanga baada ya kuvunjwa Khilafah hakuta yasitisha vile vile kukumbuka kuvunjwa kwake hakupasi kuchukuliwa kama matanga bali kuwe ni kichachawizo cha Ummah kuongeza juhudi zake maradufu katika kufanya kazi ya kuisimamisha tena. Ulinganizi wa Khilafah kwa sasa unahisika ndani ya mishipa ya Waislamu kote duniani. Wamagharibi wanazipa nguvu upya juhudi zao za kuzuia kurudi kwa Khilafah. Hawana budi kujua kwamba Uislamu ni Khilafah na Khilafah ni Uislamu, ambayo Allah (swt) amewaahidi waumini Wake.

وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مِنكُمْ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِى ٱلْأَرْضِ كَمَا ٱسْتَخْلَفَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ ٱلَّذِى ٱرْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّنۢ بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا ۚ يَعْبُدُونَنِى لَا يُشْرِكُونَ بِى شَيْـًٔا ۚ وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُو۟لَٰٓئِكَ هُمُ ٱلْفَٰسِقُونَ

Allah amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia dini yao Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na wakao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.  [Nur: 55]

Ndiyo, Khilafah ni ahadi ya Allah (swt) ambayo inakuja hivi karibuni na hakuna wa kuizuia. Tunamuomba Allah (swt) katika mwezi huu mtukufu wa Rajab ambao tunakumbuka tukio hili baya na chungu la kuvunjwa kwa Khilafah kuturuzuku nguvu zaidi za kufanya kazi kwa ajili ya kuisimamisha tena kwa idhini ya Allah.

Imeandikiwa Afisi ya Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya