1- Kuziondoa Pesa za Haramu 2- Udanganyifu katika Biashara

Kwa: Yusuf Abu Islam

Maswali:                                                  

Assalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuhu Amiri wetu, Allah akupandishe daraja na alete ushindi wa umma huu mikononi mwako.

Nina maswali mawili:

La kwanza: katika jibu lako la swali kwa ndugu yetu kuhusiana na hisa, ulisema: ukimpa mamlaka mamako ambaye ni kafiri kuuzia hisa, ndani ya muda fulani, baada ya kujua kuwa hisa (shares) zimeharamishwa, ni lazima pia uziondoe faida za hisa zako hizo ndani ya muda fulani pia kwa kuzitumia kwa ajili ya maslahi ya Waislamu. Je, kuna dalili gali inayoashiria kuwa azitumie kwa ajili ya maslahi ya Waislamu wakati kisheria yeye siye mmiliki wa pesa hizi, iweje basi aruhusiwe kuzitumia?

La pili: nafanya kazi katika sekta ya uuzaji mboga kama mchuuzi. Nanunua kutoka sokoni ambalo liko umbali wa kilo mita arubaini kutoka mahali nilipo. Baadhi ya wakati hukuta ubovu katika bidhaa… Ni katika desturi kuwa ikiwa mmiliki wa duka la reja reja ataambiwa arudishe bidhaa iliyo haribika ataruhusiwa kurudisha kwa bei chache kuliko alivyo nunulia. Ikiwa nitarudisha bidhaa siku hiyo hiyo, gharama za usafiri zitakuwa juu kuliko hiyo bei. Je, hii ni ridhaa (indemnity) yaani tofauti baina ya bei ya bidhaa zilizo haribika na ambazo hazija haribika? Je, na ile takhfifu (discount) ambayo tunaitisha ni haramu kuichukua?

Jibu:

Wa Alaikum Assalam Wa Rahmatullah Wa Barakatuhu

Kwanza: Jibu la swali la kwanza kuhusu matumizi ya pesa za haramu:

1- Yaoneka kana kwamba ulichanganyikiwa na kudhani kuwa maneno yetu: “Ni lazima uziondoe faida za hisa zako katika muda huu wa miezi mitano na uzitumie kwa ajili ya maslahi ya Uislamu na Waislamu” yalimaanisha sadaqa, yaani, kuwa mtu atapata thawabu kwa kuzitumia pesa hizi kwa maslahi ya Waislamu, lakini kadhia sio hivyo, tume sema “ziondoe”, yaani, kama ambaye una vitu visivyo hitajika nyumbani kwako na wataka kuvitoa, bila shaka utaviweka mahali panapo stahili, yaani, hutavichukua vitu hivi na kuvitupa barabarani, na kisha kudai kuwa umeviondoa, badala yake utavichukua na kuviweka mahali panapo stahili, na hii ya maanisha kuwa utachagua mahali panapo faa zaidi kuviweka, au sio? Si itakuwa ni ukosefu wa busara kuvichukua vitu hivi vya ziada na kuvitupa barabarani na kusababisha madhara kwa watu?

Ndio maana tukasema anapaswa kuziondoa faida hizi na kuzitumia kwa maslahi ya Waislamu, na kamwe hapaswi kuzichukua pesa hizi na kwa mfano kuzitupa chini, au kuzitia katika jaa la taka! Ndugu yangu Yusuf, ni lazima aziondoe na kuziweka mahali panapo stahili. Lakini kamwe haita chukuliwa kuwa ni sadaqa kwake na kulipwa thawabu kutokana nayo. Amepokea Ahmad katika Musnad yake kutoka kwa Abdullah Ibn Mas’ood, aliye sema kuwa Mtume wa Allah (saw) amesema:

«… وَالذي نفسي بيده…لَا يَكْسِبُ عَبْدٌ مَالًا مِنْ حَرَامٍ، فَيُنْفِقَ مِنْهُ فَيُبَارَكَ لَهُ فِيهِ، وَلَا يَتَصَدَّقُ بِهِ فَيُقْبَلَ مِنْهُ، وَلَا يَتْرُكُ خَلْفَ ظَهْرِهِ إِلَّا كَانَ زَادَهُ إِلَى النَّارِ، إِنَّ اللَّهَ عَزَّ وَجَلَّ لَا يَمْحُو السَّيِّئَ بِالسَّيِّئِ، وَلَكِنْ يَمْحُو السَّيِّئَ بِالْحَسَنِ، إِنَّ الْخَبِيثَ لَا يَمْحُو الْخَبِيثَ»

“…Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake… mja hato chuma mali ya haramu kisha akaitumia kisha akabarikiwa kutokana nayo, wala hataitolea sadaqa kisha ikakubaliwa sadaqa yake, wala hato itelekeza (mali hiyo) nyuma ya mgongo wake isipokuwa itakuwa ni zawadi yake ya kumpeleka motoni. Allah ‘azza wa jalla hafuti jambo baya kwa baya, lakini hufuta jambo baya kwa zuri, hakika uovu haufuti uovu.”     

2- Kwa taarifa zaidi, imesimuliwa wazi wazi na wanazuoni wa fiqhi kuwa mtu anapaswa kuiondoa mali ya haramu kulingana na sheria. Wame nukuu kama dalili yale yaliosimuliwa kutoka kwa Asim Ibn Kulaib kutoka kwa babake kuhusu bwana mmoja wa kianswari. Alisema: “Tulitoka na Mtume wa Allah kwenda katika mazishi, nikamuona Mtume (saw) katika kaburi akimshauri mchimba kaburi: chimba nafasi kubwa ya sehemu ya miguu na kichwa, aliporudi, alipokewa na mjakazi wa mwanamke, akamletea chakula, kisha akaweka mikono yake juu ya chakula, na watu wakafuata na kula, baba zetu wakamtazama Mtume wa Allah (saw) huku akiendelea kutafuna, Mtume (saw) akasema:

«إني أجد لحم شاة أخذت بغير إذن أهلها»

“Mimi na hisi kutoka katika nyama hii kuwa kondoo huyu alichukuliwa pasi na idhini ya wenyewe”, yule mwanamke akasema: “Ewe Mtume wa Allah, nilimtuma kwa Baqi kuninunulia kondoo lakini hakupata, kwa hivyo nikamtuma kwa jirani yangu – aliye nunua kondoo – ili aniletee ni mnunue kwa bei yake, lakini hilo halikutokea, nilitumana kwa mke wake, na yeye (mke) akaniletea kondoo huyo, Mtume (saw) akasema:

«أطعميه الأسارى»

“Walishe kondoo huyo mateka”

Katika riwaya nyengine, neno lililo tumika lilikuwa na maana pana zaidi kuliko ‘maslahi ya Waislamu’; walizungumzia kuhusiana na mas’ala jumla ya sehemu ambazo sadaqa inaweza kutumiwa kwa mfano:  kuwapa masikini au kujenga misikiti kwa sababu haya ni miongoni mwa mambo ambayo sadaqa yaweza kutumika kwayo. Hii ndio rai ya madh’habu ya Abu Hanifa: Imesimuliwa kutoka katika Hashiyat Ibn ‘Abidin (3/223), na Al-Malik katika Al Jami’ Li Ahkam Al Qur’an na Qurtubi (3/366).

Baadhi ya wanazuoni wamesema “kutumia katika njia ya Allah” maana yake ni “Jihad”. Mmoja kati ya wanaobeba rai hii ni Sheikh Al-Islam Ibn Taymiyah, ambaye amesema katika “Majmoo’ Al-Fatawa (28/401)’, ((Hata kama mtu amepata mali ya haramu mikononi mwake na hakuweza kuiregesha kwa mwenyewe kwa kutomjua, na kadhalika… basi aitumie katika njia ya Allah, hivi ndivyo inavyostahili kutumiwa. Mtu mwenye madhambi mengi tiba yake ni Jihad; na mtu ambaye ataka kujikomboa na haramu na kutubia lakini hana uwezo wa kuirudisha mali kwa wenyewe, basi na aitumie katika njia ya Allah kwa niaba ya wamiliki wake, kwani hii ndio njia ya amali njema itakayo kuwa ndio mkombozi wake kutokana na malipo ya Jihad…)). Na kuna riwaya nyengine nyingi.

Pili, jibu la swali la pili kuhusu kazi yako ya kuuza mboga, na haya ndio maneno ya swali  lako:

(Nafanya kazi katika sekta ya uuzaji mboga kama mchuuzi. Nanunua kutoka sokoni ambalo liko umbali wa kilo mita arubaini kutoka mahali nilipo. Baadhi ya wakati hukuta ubovu katika bidhaa… Ni katika desturi kuwa ikiwa mmiliki wa duka la reja reja ataambiwa arudishe bidhaa iliyo haribika ataruhusiwa kurudisha kwa bei chache kuliko alivyo nunulia. Ikiwa nitarudisha bidhaa siku hiyo hiyo, gharama za usafiri zitakuwa juu kuliko hiyo bei. Je, hii ni ridhaa (indemnity) yaani tofauti baina ya bei ya bidhaa zilizo haribika na ambazo hazija haribika? Je, na ile takhfifu (discount) ambayo tunaitisha ni haramu kuichukua?) Mwisho wa nukuu.

Jibu lake limefafanuliwa katika (kitabu cha) “Nidhamu ya Uchumi katika Uislamu” katika sura ya ‘Udanganyifu katika Biashara’ (Kitabu cha Kiigereza, ukurasa wa 210/ kitabu cha kiarabu, ukurasa 193), kinaeleza:

(… Muislamu haruhusiwi kudanganya katika bidhaa au pesa. Bali anatakikana kuonyesha dosari ilioko katika bidhaa, na kueleza udanganyifu katika pesa.  Haruhusiwi kudanganya katika bidhaa kwa lengo la kuisambaza au kuiuza kwa bei ya juu. Wala haruhusiwi kudanganya katika pesa ili ikubalike kama bei ya bidhaa. Hii ni kwa sababu kuharamishwa haya na Mtume (saw) kulikuwa kwa kukatikiwa. Ibn Majah asimulia kutoka kwa ‘Uqbah ibn ‘Amir kwamba Mtume (saw) amesema:

«المسلم أخو المسلم، ولا يحل لمسلم باع من أخيه بيعاً فيه عيب إلاّ بيّنه له»

 “Muislamu ni ndugu ya Muislamu, wala si halali kwa Muislamu kununua bidhaa yenye dosari kutoka kwa ndugu yake isipokuwa amuonyeshe dosari hiyo.”

Bukhari pia asimulia kutoka kwa Hakeem ibn Hizam kwamba Mtume (saw) amesema:

«البيّعان بالخيار ما لم يتفرقا، فإن صدقا وبينا بورك لهما في بيعهما، وإن كتما وكذبا محقت بركة بيعهما»

“Wafanyi biashara wawili (muuzaji na mnunuzi) wanakhiari (kutimiza au kuvunja mkataba wa biashara yao) kabla hawaja tengana. Ikiwa walikuwa waaminifu na wakabainisha (bidhaa na pesa) biashara yao itabarikiwa. Lakini ikiwa walificha (dosari) na kudanganya baraka ya biashara yao itaondolewa.”

Mtume (saw) asema:  «ليس منا من غش»“Si katika sisi anaye tudanganya (katika biashara)”, kama inavyosimuliwa na Ibn Majah na Abu Dawud kutoka kwa Abu Hurayrah. Yeyote atakaye pata pato kupitia ghushi au udanganyifu haitakuwa milki yake halali (kisheria), kwa sababu udanganyifu sio miongoni mwa njia za kisheria za umilikaji, bali ni katika njia za haramu za umilikaji na kwa hivyo kitu hicho (kilicho patikana kupitia udanganyifu) ni mali ya haramu (Suht). Mtume (saw) asema: «لا يدخل الجنة لحم نبت من سحت، النار أولى به»  “Nyama yoyote (mwilini mwa binadamu) iliyo mea kutokana na mali ya haramu (suht) haiingii peponi, moto ndio aula kwa nyama hiyo”, imepokewa na Ahmad kutoka kwa Jabir ibn Abdullah. Ikiwa gushi itatokea kwa bidhaa au pesa, mtu aliye danganywa ana khiari ya kuvunja mkataba au kuendelea nao. Kwa hivyo ikiwa mnunuzi atakhiari kubakia na bidhaa yenye dosari na kuchukua ridhaa, yaani, tofauti ya bei baina ya bidhaa nzima na bidhaa yenye dosari, hana haki ya kufanya hivyo, kwa sababu Mtume (saw) haku ruhusu uchukuaji wa ridhaa (indemnity); bali ilitoa khiari baina ya mambo mawili: «إن شاء أمسك، وإن شاء ردها» “Akipenda aichukue na akipenda airudishe”, kama inavyo simuliwa na Bukhari kutoka kwa Abu Hurairah.

Kwa hivyo, unapopata dosari katika bidhaa baada ya kuinunua, una khiari ya kuirudisha kwa mwenyewe na kuchukua bei uliyo nunulia, au kuikubali na kubakia nayo… lakini huwezi kubakia nayo kwa kupokea ridhaa kiasi fulani yaani tofauti ya bei kati ya bidhaa nzima na zilizo na dosari. Ama kuhusu masafa marefu yaliyopo kati yako na sokoni unako nunua bidhaa zako, haiathiri hukmu hii. Kama ilivyo katika hadith, una khiari tu ya mambo mawili: «إن شاء أمسك، وإن شاء ردها» “Akipenda aichukue na akipenda airudishe”, kama inavyo simuliwa na Bukhari kutoka kwa Abu Hurairah.

Ndugu Yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

15 Shawwal 1438 HIJRI

9/7/2017 MILADI