Hukm ya Kishari’ah Juu ya Upasuaji wa Mapambo

 

Ufupisho wa Suali na Jawabu – 3

Suali:

Ni ipi Hukm ya Kishari’ah Juu ya Upasuaji wa Mapambo/Kufanya opersheni kwa ajili ya Mapambo,

Jibu:

Kwanza: Ikiwa sababu ya upasuaji huo ni kwa ajili ya matibabu, kwa mfano kufanya upasuaji ili urekebishe sehemu ya mwili iliyosababishwa kuharibika, mfano na maradhi, ajali au kuchomeka, au kurekebisha kasoro za kuzaliwa kama kumkata mtu aliyezaliwa na kidole kilichozidi urefu au kuvitenganisha vidole vilivyoshikana na mfano wa haya. Upasuaji aina hiyo unaruhusiwa na ushahidi wa hilo ni alivyosimulia al-Tirmidhi kutoka Arfajah ibn As’ad alisema:

“Pua yangu ilikuwa imekatika vibaya Siku ya Al-Kulab wakati wa Ujahiliya. Kwa hiyo nikatumia pua ya Wariq (shaba) ambayo ilikuwa inaisha polepole, hivyo Mtume (saw) akaniagiza nitafute mfano wa pua iliyotengezwa kwa dhahabu”

Maana ya “pua ya Wariq” ni ya shaba. Hii inaashiria kuwa upasuaji wa plastiki (plastic surgery) kwa ajili ya matibabu inaruhusiwa.

Pili: Ikiwa upasuaji huo ni kwa ajili ya kuboresha muonekano na kujirembesha na sio kwa ajili ya matibabu. Upasuaji aina hiyo hauruhusiwi na ushahidi wa hilo ni alivyosimulia al-Bukhari kupitia Alqama, alisema:

“Mwenyezi Mungu amewalaani wanawake wanaojichora tattoo (Washimat) na wanawake (Mustawshimat) walio kata nywele za uso na nyusi (Mutanammisath), na wanawake wanaotenganisha meno yao ya mbele kwa kujirembesha, wanao badilisha aliyoumba Mwenyezi Mungu.”

Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye Hekima.

Link ya Kiengereza: http://hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/qestions/jurisprudence-questions/15218.html

Chanzo: Hizb ut Tahrir Kenya

17 Shaaban 1439 Hijria

03 Mei 2018 Miladi